Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all 11654 articles
Browse latest View live

TAHAFE YATANGAZA TAASISI 31 ZITAKAZO PELEKA MAHUJAJI KWENDA KUHIJI MAKKA

$
0
0
Mwenyekiti wa Shirikisho la Taasisi za Hijja Tanzania (TAHAFE), Sheikh Abdallah Khalid (katikati), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kuhusu mchakato wa kwenda kuhiji mwaka huu 2016. Kushoto ni Katibu wa Taasisi hiyo, Dk. Ahmed Twaha na kulia ni Mjumbe, Hassan Ali.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.

Na Dotto Mwaibale

OFISI Kuu ya Hijja ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imezitangaza taasisi 31 zilizokidhi vigezo vya kupeleka mahujaji kwenda kuhiji kwa mwaka 2016.

Hayo yalibainishwa na Mwenyekiti wa Shirikisho la Taasisi za Hijja Tanzania (TAHAFE) Sheikh Abdallah Khalid wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana.

Alisema shughuli zote za utekelezaji wa ibada ya Hijja na Umra hapa nchini zinasimamiwa, kuratibiwa na kuendeshwa chini ya uongozi wa Biita inayoundwa na Shirikisho la Taasisi za Hijja Tanzania (Tahefa) na Umoja wa Taasisi za Hijja Zanzibar (Utahiza).

Alisema gharama za mahuja kwa mwaka huu kutoka nchi kwenda kuhiji ni dola 3400 hadi 4700 na kuwa malipo ya huduma stahili yanapaswa kupitia benki zilizoanishwa na Wizara ya Hijja Saudia Arabia.

Sheikh Khalidi alisema taasisi zote zinatakiwa kuwapima afya mahujaji watarajiwa mapema kuanzia Agosti 8 au kabla ya hapo na kujaza fomu maalumu zitakazotolewa na Biita na kuingizwa kwenye mtandao.

MBUNGE ROSE TWELVE KUWANUFAISHA WANAWAKE WA MKOANI IRINGA

$
0
0
 Mbunge wa viti maalum mkoa wa Rose Twelve akifurahi jambo na wakinamama wenye ulemavu.

Na Fredy Mgunda, Iringa

Wananchi mkoani iringa wanatarajia kunufaika na muungano wa wabunge watatu vijana wa viti maalum kwa lengo kubadilishana uzoefu wa kuwaletea maendeleo wanawake wa mkoa huu.

Akizungumza na blog hii Mbunge wa viti maalum mkoa wa Rose Twelve alisema wameamua kuungana ili kubadilisha mfumo wa utawala na kuondoa ufanyaji wa kazi kwa mazoea sambamba na kuwasaidia wananchi wanaowatumikia.

“Unajua kuwa changamoto na matatizo ya wanawake kwa asilimia kubwa zinafanana hivyo najifunza kwa wenzangu wanatatuaje changamoto hizo ili na mimi niweze kutatua matatizo ya wanawake wa mkoani iringa na waendelee kufanya maendeleo huku wakiwa hawana changamoto nyingi”alisema Rose

Aidha rose aliongeza kwa kusema kuwa kiongozi bora ni Yule aliyetari kujifunza ili aweze kupata ujuzi wa kuwasaidia wananchi kwa kuwapa mbinu wananchi za kuwaletea maendeleo.

Rose alisema amejipanga kuwekeza kwenye elimu ili kuwapa wanawake fursa ya kuwapa ya kuwawezesha kunufaika na mfuko wa mbunge anaotarajia kuuanzisha.

“Nitatoa milioni hamsini kila mwaka kwa umoja wa wanawake wa ccm UWT mkoani hivyo lazima nitafute njia mbadala ya kuwapa elimu ya kuzitumia hizo pesa ili ziwanufaishe kwa kuwaletea maendeleo”.alisema Rose

Lakini Rose alisema kuwa atataufa wataalamu wa mafunzo mbalimbali ili wanawake wa mkoa wa iringa wapate elimu ya ujasiliamali na kuokoa pesa ambazo zimekuwa zikipotea.

Nitatafuta wadau mbalimbali wachangie mfuko wangu wa mbunge kwa lengo la kuwasaidia wanawake ambao hawana mitaji ya kujiendesha maisha yao.alisema Rose

Amemalizia kwa kuwataka wakazi wa Iringa kufanya kazi kwa bidii ili kuleta maendeleo binafsi na taifa kwa ujumla.

MTOTO WA KITANZANIA ASHIRIKI KATIKA FILAMU YA KIMAREKANI

$
0
0
Tasnia ya filamu Tanzania inazidi kukua kwa kasi, si tu nyumbani hata nje ya nchi watanzania wanazidi kungara.

Safari hii mtoto wa watanzania wenzetu aitwaye Evan Byarushengo amabahatika kupata nafasi ya kushiriki katika filamu ya kimarekani iitwayo THE REAL MVP: The Wanda Durant Story.

Filamu hii inajaribu kuonyesha jinsi mama wa mchezaji nyota wa mpira wa kikapu Kevin Durant alivyohangaika kuwakuza watoto wake mpaka kufikia kuwa mastaa. Evan anaigiza kama Kevin Durant akiwa mtoto wa miaka 7. Waigizaji wakuu wa filamu hii ni pamoja na Cassandra Freeman anayeigiza kama mama Evan; Pauletta Washington (mke wake Denzel Washington) ambaye anaigiza kama bibi yake Evan na wengine wengi. 
Juu, katika clip mojawapo Evan akifanya mazoezi ya kucheza mpira wa kikapu. Nyuma ni director wa filamu George Nelson na wasaidizi wake. 
Juu, Evan akiwa anaongea na bibi yake (Pauletta) na mtoto anayeigiza kama kaka yake Kevin aitwaye Tony. 
Juu Evan(aliyechuchumaa) akipitia script mbele ya wenzake. 
Evan na mwenzake mwishoni walipata bahati ya kuonana na mama yake Kevin ambaye stori ya filamu inamuigiza.
Unaweza kuona clips za hiyo movie kupitia links hizi za youtube. 


Kwa walio Marekani na Canada, movie hiyo itaonyeshwa siku ya Ijumaa na Jmosi kupitia Lifetime Channel 8/7c

Tuendelee kumwombea mtanzania mwenzetu aende mbele zaidi ili tuzidi kuipeperusha bendera yetu. Evan amefanya audition nyingi kwahiyo Mungu akipenda ataonekana kwenye matangazo ya kibiashara na filamu zaidi. 

Asante sana,

Dr. Philomena Ishengoma & Godfrey Byarushengo
Wazazi wa Evan

BILIONI 6 ZA RAIS DK. JOHN MAGUFULI KUNUNULIA MADAWATI ZAIBUA MAJIPU JESHINI

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Edosama Wood,  Research Center cha Kinyerezi jijini Dar es Salaam, Edward Maduhu (katikati), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, akidai kutapeliwa na maofisa wa jeshi la Magereza na Kujenga Taifa (JKT), katika utengenezaji wa madawati ya bei nafuu kama Rais Dk. John Magufuli alivyoagiza.

Maduhu akiwaonesha waandishi wa habari picha mbalimbali walizopiga na maofisa wa majeshi hayo walipofika kufanya kikao na uongozi wa kiwanda hicho.
Maduhu akionesha madawati yanayotengenezwa na kiwanda chake.
Moja ya mashine zinazotumika kutengeneza samani mbalimbali katika kiwanda hicho.

Na Dotto Mwaibale

SHILINGI bilioni 6 zizotengwa na Rais Dk. John Magufuli kwa ajili ya utengenezaji wa madawati zimeibua majipu katika Jeshi la Magereza na Kujenga Taifa (JKT), kwa kudaiwa kumtapeli Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Edosama Wood,  Research Center cha Kinyerezi jijini Dar es Salaam, Edward Maduhu katika utengenezaji wa madawati.

 Maduhu  amezilalamikia taasisi hizo za jeshi akidai zimemtapeli katika kazi ya kutengeneza madawati hayo baada ya kukubaliana kufanya ushirikiano wa kazi hiyo kufuatia wao kuelemewa.

Maduhu alitoa lawama hizo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kutapelewa na majeshi hayo waliofika kiwandani kwake kuomba ubia wa kushirikiana kutengeneza madawati ya bei nafuu kama alivyoagiza Rais.

Hata hivyo, Mkuu wa Kiwanda cha Magereza, ACP Ismail Mlawa, alisema baada ya serikali kutoa ‘order ya kutengeneza madawati hao, taasisi hizo mbili ziliunda timu maalumu ya kutengeneza madawati hayo.

Alisema, baada ya kuunda timu hiyo, walikubaliana kuzunguka kwenye viwanda mbalimbali nchini kwa ajili ya kuangalia vifaa na sampuli ya utengenezaji wa madawati hayo ili yaweze kuwa katika ubora unaokubalika.

Alisema, kutokana na hali hiyo, timu hiyo ilikwenda kwenye viwanda mbalimbali kikiwamo hicho cha Edosama kwa lengo la kuangalia upatikanaji wa vifaa na si vinginevyo.

“Tulienda kwenye viwanda zaidi ya vinne kikiwamo cha Edosama, lengo ni kuangalia namna ya upatikanaji wa ‘material’ (vifaa) vya kutengeneza madawati pamoja na kufanya ‘window shoping’ lakini katika viwanda vyote hivyo, hakuna hata kimoja tulichoingia nacho mkataba wa kutengeneza madawati kwa sababu hatukuwa na mamlaka ya kufanya hivyo mpaka tutakapowasilisha taarifa kwa viongozi wetu,”alisema Mlawa.

Aliongeza, baada ya kuona wanavyotengeneza madawati hao, walilazimika kuwasilisha taarifa hiyo kwa viongozi wao ili waweze kujadiliana kuhusiana na suala la utengenezaji wa madawati hao.

Maduhu alisema Aprili 12 mwaka huu walipigiwa simu na maofisa wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Jeshi la Magereza ambao walifika katika kiwanda chao na kufanyanao vikao vinne kuanzia Aprili 12 na 15 mwaka huu.

Alisema maofisa wa majeshi hayo walioshiriki vikao hivyo ni Kanali Wanyancha na Tendwa Mahunnah wote kutoka JKT na ASP Mlawa pamoja na ofisa mwingine wa Jeshi la Magereza ambaye jina lake halikupatikana.

Maduhu alisema kwamba katika kikao hicho jumla walikuwa saba pamoja na maofisa wa kiwanda hicho na kuwa katika kikao hicho walifanikiwa kupiga picha za mnato, kurekodi mazungumzo yote.

Aliongeza kuwa katika kikao hicho maofisa hao wa jeshi waliwaeleza kuwa wamefika kiwandani hapo baada ya kushindwa bei ya madawati iliyotolewa na Rais ya sh. 50,000 kwa kila dawati kwani gharama zao za kutengeneza dawati moja ni zaidi ya sh. 78,000.

Alisema kwamba katika kikao hicho walikubaliana kiwanda hicho kipewe kazi ya kusambaza vyuma vya miguu ya madawati hayo vyenye ukubwa wa inchi 1x1-1.5 mm vikiwa vimepakwa rangi.

Maduhu alisema baada ya kukubaliana walianza kuwapa teknojia ya utengenezaji wa madawati hayo huku wakiendelea kuandika hadi waliporidhika na gharama ya kutengeneza dawati moja kwa sh. 38,000 na sh. 40,000 kwa teknolojia ya kiwanda hicho.

Alisema baada ya kupata teknolojia hiyo walikata mawasiliano na kila walipokuwa wakiwapigia simu walikuwa hawapokei.

Alisema kiwanda hicho kimetumia zaidi ya sh.bilioni moja kwa ajili ya utafiti wa miaka mitano kwa kutembea viwanda katika nchi 17 ili kujifunza teknolojia hiyo na kuwa wao wamekuwa wa kwanza kubuni aina mpya za madawati hapa nchini.

RAIS DKT. MAGUFULI AZUNGUMZA NA WANACHI MBALIMBALI ALIPOKUWA SAFARINI KUTOKEA DODOMA KUELEKEA ARUSHA

$
0
0

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia na mamia ya wakazi wa Babati Mkoani Manyara waliomsimamisha wakati akitokea Dodoma kuelekea mjini Arusha.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akinunua karanga kutoka kwa mjasiriamali mara baada ya kuwahutubia mamia ya wakazi wa Babati mkoani Manyara waliojitokeza katika eneo la Stendi ya Mabasi ya Babati Mkoani Manyara.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia na mamia ya wakazi wa Magugu mkoani Manyara wakati akielekea  Mkoani Arusha.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wafanyabiashara wa Stendi ya Mabasi ya Singida wakati alipokuwa njiania kuelekea Arusha.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wakazi wa Endasak mkoani Manyara wakati akitokea Dodoma kuelekea Arusha kwa njia ya barabara.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Dareda mkoani Manyara waliojitokeza kumsalimia wakati akitokea Dodoma kuelekea mkoani Arusha. PICHA NA IKULU.

UN NA EU WAFURAHISHWA NA MIRADI WALIYOIFADHILI JIJINI MWANZA

$
0
0
RC Mwanza, John Mongella
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella (kulia) akisalimiana na kumkaribisha ofisini kwake Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez aliyeambatana na Mkuu wa Idara ya Siasa, Mawasiliano ya Umoja wa Ulaya, Luana Reale (katikati) walipowasili jijini Mwanza kabla ya ziara ya kukagua miradi inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa pamoja na Umoja wa Ulaya.
MRATIBU Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini, Alvaro Rodriguez pamoja na Mkuu wa Idara ya Siasa, Mawasiliano ya Umoja wa Ulaya, Luana Reale, wamesema wameridhishwa na miradi inayofadhili maeneo kadhaa jijini Mwanza.
Wakizungumza baada ya kutembelea Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (Mwauwasa), Hospitali ya Rufaa Bugando (BMC), Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT) na Radio ya Kijamii (Saut), walisema utekelezaji wa miradi hiyo imewatia hamasa kubwa.
Awali akizungumza katika ofisi za Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Mwauwasa), Mkurugenzi Mtendaji wa mamlaka hiyo, Anthony Sanga, alisema mradi unaoendelea sasa wa kusambaza maji safi utakapokamilika utaweza kuwafikia wakazi 54,000 badala ya 23,000 wa sasa.
Sanga alisema mradi huo utakapokamilika Mei mwaka huu, utawafikia wakazi kwa asilimia 90 badala ya 68 za sasa.

“Mradi ukishakamilika utafanikisha makusanyo ya Sh. Bilioni 1.4 kwa mwezi badala ya kukusanya Sh. milioni 316 za sasa kwa mwezi, ukiwa na matanki ya ujazo wa lita 33,400,” alisema Sanga.

Akizungumzia hilo, Rodriguez alisema baada ya kushuhudia miradi hiyo ukiwamo wa maji taka chini ya ufadhili wa EU, amefurahishwa na hali ya miradi hiyo.

“Timu yetu imetembelea Mwauwasa na kushuhudia miradi hiyo inayofadhiliwa na Jumuiya ya Ulaya kwa ajili ya huduma ya maji kwa wananchi, pia tumeenda kuangalia chanzo cha maji na yanapowekwa maji taka,” alisema Rodriguez.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa Bugando, Prof. Kien Mteta, alishukuru UN na EU kwa miradi hiyo na kuja kushuhudia ufadhili wao.

“Ufadhili umelenga katika mambo matatu, moja kwenye maabara ambako vilinunuliwa vifaa vya mbalimbali vikiwamo vya kutambua kansa, pili vifaa vya mionzi kwa ajili kutambua vyanzo vya magonjwa,” alisema Prof. Mteta.

Aidha, alisema pia wafadhili hao walitembelea kitengo cha kutoa matibabu ya mionzi ya kansa, ambacho kinawafunza baadhi ya watumishi wake na upatikanaji wa mashine.
Luana Reale, EU Tanzania
Mkuu wa Idara ya Siasa, Mawasiliano ya Umoja wa Ulaya, Luana Reale (katikati) akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella mara baada ya kuwasili ofisini kwake mwishoni mwa wiki.
Hospitali ya Bungando yenye uwezo wa vitanda 950 iliyoanzishwa mwaka 1972 ni miongoni mwa hospitali nne kubwa nchini ambazo hutoa tiba maalumu ikihudumia watu milioni 16 katika mikoa minane ya kanda ya ziwa.

Hospitali hii inatoa tiba ya ugonjwa wa saratani kwa mifumo miwili. Moja kwa kutumia onkolojia au patholojia na tiba kwa kutumia mionzi.

Toka mwaka 2000 hospitali ya Bugando imekuwa ikifanyakazi kwa karibu na kampuni ya kitaliano ya TISSON ASSOCIATION ili kuboresha huduma zake patholiojia na pia kuanza kutibu kansa mwaka 2009.

Wataliano wamewezesha kufundishwa kwa wataalamu wa patholojia na onkolojia ya tiba, vifaa tiba, dawa na kuwezesha ziara za za kifundi za watu wa patholojia na utafiti.

Uangalizi wa wagonjwa wa kansa na matibabu yao ulianza mwaka 2009 na kuelezwa kuwa kwa mwaka wagonjwa 3500 wa kansa huangaliwa.

Huduma ya uangalizi ni pamoja na kufanya utambuzi, upasuaji na utoaji wa tiba ya kemo.
Hoyce Temu
Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akitoa utambulisho wa ujumbe alioambatana nao kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella.

Hata hivyo wagonjwa wanaohitaji huduma ya mionzi hukatiwa rufaa hospitali ya kansa ya Ocean (ORCI).

Kutokana na kuzidiwa kwa hospitali ya Ocean Road katika tiba ya mionzi, serikali iliamua kutanua huduma zake na kuzifikisha Bugando.

Ili kuwezesha haja ya serikali taasisi ya nguvu za atomiki duniani na ile ya hapa nchini kupitia mpango wa ushirikiano wa kiufundi walianzisha miradi kadha yenye lengo la kuwezesha huduma yenye tija kwa wagonjwa wa kansa.

Mashirika ya Umoja wa Mataifa ambayo yanachangia miradi hiyo imekuwa ikisaidia serikali ya Tanzania kuwezesha tiba ya mionzi katika hospitali ya Bugando.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella akiwa kwenye mazungumzo na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez aliyeambatana na Mkuu wa Idara ya Siasa, Mawasiliano ya Umoja wa Ulaya, Luana Reale katika ziara maalum ya kukagua miradi mbalimbali inayofadhiliwa na UN pamoja na EU jijini humo.
Alvaro Rodriguez
Kutoka kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza CP. Clodwig Mtweve, Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella pamoja na Mkuu wa Idara ya Siasa, Mawasiliano ya Umoja wa Ulaya, Luana Reale wakiwa wameshilikilia kuhamasisha utekelezaji wa malengo mapya ya maendeleo endelevu (SDGs) ambayo yamewafikia wakazi wa jiji la Mwanza.
Luana Reale
Mkuu wa Idara ya Siasa, Mawasiliano ya Umoja wa Ulaya, Luana Reale akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Mwauwasa) mara baada ya kuwasili katika ofisi hizo jijini Mwanza.
Eng. Anthony Sanga
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Mwauwasa), Mhandisi Anthony Sanga, akitoa 'power point presentation' ya maendeleo ya mradi wa maji unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya jijini Mwanza kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, Mkuu wa Idara ya Siasa, Mawasiliano ya Umoja wa Ulaya, Luana Reale aliyeambatana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez.
Anthony Sanga
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Mwauwasa), Mhandisi Anthony Sanga akitoa maelezo ya mradi kwa ugeni ulioambata na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella.
Mwauwasa 1
Maji yakiwa kwenye hatua ya kutakatishwa ili yawe salama kwa watumiaji.
Godadi Mgwatu
Mhandisi wa ubora wa maji Mwauwasa, Godadi Mgwatu akitoa maelezo kwa mgeni ugeni huo ulioambatana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella kukagua mradi wa maji wa Mwauwasa jijini Mwanza.
Mhandisi, Anthony Sanga-Mwauwasa Mwanza
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Mwauwasa), Mhandisi Anthony Sanga akitoa maelezo kwa ugeni huo ya namna ya maji yanavyochujwa na kusafisha kwa kutumia mtambo maalum uliopo mbele yao. (Picha zaidi za ziara hii Bofya hapa)

MAKATIBU WAKUU WA VYAMA VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA WAKUTANA NCHINI ZIMBABWEMAKATIBU WAKUU WA VYAMA VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA WAKUTANA NCHINI ZIMBABWE

$
0
0
 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana akitoa mada kwenye Kongamano la siku Nne la Makatibu Wakuu wa vilivyokuwa Vyama vya Ukombozi Kusini mwa Afrika. Kongamano hilo linafanyika Victoria Falls Zimbambwe lilianza tarehe 4 – 8 Mei, 2016. Vyama hivyo ni ANC ya Afrika Kusini, FRELIMO ya Msumbiji, MPLA ya Angola, SWAPO Party ya Namibia na CCM ya Tanzania.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana akimpongeza Katibu Mtendaji Mkuu wa ZANU-PF Ndugu Ignatius Morgen Chombo kwa kufanikisha Kongamano la Makatibu Wakuu wa vilivyokuwa Vyama vya Ukombozi Kusini mwa Afrika na anaeshuhudia katikati ni Katibu Mkuu wa FRELIMO Ndugu Eliseu Machava. Kongamano hilo linafanyika Victoria Falls, Zimbabwe tarehe 4 – 8 Mei 2016
Picha ya pamoja ya Makatibu Wakuu wa vilivyokuwa Vyama vya Ukombozi Kusini mwa Afrika(FLM) wanaoshiriki Kongamano la siku Nne la kutafakari uimarishaji na uendelezaji wa ushirikiano wao na namna ya kukabiliana na changamoto walizonazo. Kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa ANC ya Afrika Kusini Ndugu Ndugu Gwede Mantashe, Katibu Mkuu wa FRELIMO ya Msumbiji Ndugu Eliseu Machava, Katibu Mkuu wa CCM ya Tanzania Ndugu Abdulrahaman Kinana, Makamu Waziri wa Uhusiano wa Kimataifa wa Chama cha Kikomnisti cha China (CPC) Ndugu Guo Yezhou, Katibu Mtendaji Mkuu wa ZANU-PF ya Zimbabwe Ndugu Ignatius Morgen Chombo, Katibu Mkuu wa MPLA ya Angola Ndugu Juliao Mateus Paulo na Katibu Mkuu wa SWAPO Party ya Namibia Ndugu Nangolo Mbumba. Kongamano hilo linafanyika Victoria Falls, Zimbabwe tarehe 4 – 8 Mei 2016.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana akibadilishana mawazo na Katibu Mkuu wa ANC ya Afrika Kusini, Ndugu Gwede Mantashe kwenye Kongamano la Makatibu Wakuu wa vilivyokuwa Vyama vya Ukombozi Kusini mwa Afrika(FLM) linalofanyika Victoria Falls, Zimbabwe tarehe 4 – 8 Mei 2016

WATUMISHI WA MAHAKAMA MKOANI MWANZA WA WAAHIDI UFANISI KATIKA UTENDAJI KAZI

$
0
0
Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika MISA tawi la Tanzania, Simon Berege, akifafanua jambo wakati wa Mafunzo Maalumu kwa Watumishi wa Mahakama za Mkoa wa Mwanza yanayofanyika Jijini Mwanza.

Mafunzo hayo yanawajumuisha watumishi wa Mahakama ambao ni pamoja na Mahakimu, Watunza Kumbukumbu pamoja na
Maafisa Utumishi wa Mahakama ambapo 
yalianza jana na yanafikia tamati hii leo. Yalifunguliwa na Mhe.Robert Vicent Makaramba ambae ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza.

Mafunzo hayo yamehusisha Mada mbalimbali ikiwemo "Maana ya Uhuru wa Kupata Taarifa, Huduma kwa Wateja na Mbinu za kuwasiliana kwa Watumishi wa Mahakama, Mfumo wa Kisheria wa Haki ya kupata Taarifa, Taasisi za Umma na Upatikanaji wa Taarifa na Namna ya Kutoa na Kupata Taarifa pamoja na mijadala mbalimbali ".

Washiriki wa mafunzo hayo wamesema wanatarajia kuongeza ufanisi zaidi katika kuwahudumia wateja (wananchi) wanaofika mahakamani kwa ajili ya huduma mbalimbali kama lengo la mafunzo hayo ambayo yameandaliwa na MISA tawi la Tanzania chini ya Ufadhiri wa Shirika la misaada la Ujerumani FES linavyohimiza juu ya umuhimu wa umma kupata taarifa mbalimbali za kimahakama bila vikwazo vyovyote.
Washiriki wa Mafunzo Maalumu kwa Watumishi wa Mahakama za Mkoa wa Mwanza wakiwa katika majadiliko wakati wa mafunzo hayo.
Washiriki wa Mafunzo Maalumu kwa Watumishi wa Mahakama za Mkoa wa Mwanza wakiwa katika majadiliko wakati wa mafunzo hayo.
Washiriki wa Mafunzo Maalumu kwa Watumishi wa Mahakama za Mkoa wa Mwanza wakiwa katika majadiliko wakati wa mafunzo hayo.
Washiriki wa Mafunzo Maalumu kwa Watumishi wa Mahakama za Mkoa wa Mwanza wakiwa katika majadiliko wakati wa mafunzo hayo.
Washiriki wa Mafunzo Maalumu kwa Watumishi wa Mahakama za Mkoa wa Mwanza wakiwa katika majadiliko wakati wa mafunzo hayo.
Kushoto ni Mkufunzi wa Mafunzo hayo, Wakili na Mwanahabari James Marenga, Katikati ni Thandie Mfikwa ambae ni Kaimu Mtendaji wa Mahakama Mwanza, Kulia ni Mwezeshaji wa Mafunzo, Deodatus Balile ambae ni Mhariri Mtendaji Jamhuri Media na Mtaalamu wa Mawasiliano ya Umma.
Soma Zaidi HAPA Kuhusu Mafunzo Hayo.

NAIBU SPIKA ACKSON AFUNGUA SEMINA KWA WABUNGE YA UELEWA WA HAKI ZA WATU WENYE ULEMAVU

$
0
0
 Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Wenye Ulemavu), Dk Abdallah Possi (kulia), akiwasilisha mada katika semina ya Wabunge kukuza na kuimarisha usawa wa watu wenye ulemavu nchini, kwenye Ukumbi wa Bunge wa Msekwa mjini Dodoma jana. Kutoka kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Bukene, Seleman Zedi (CCM) na Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson akifungua semina hiyo
 Baadhi ya wabunge wakihudhuria kwenye semina hiyo
 Zedi akiongoza majadiliana wakati wa semina hiyo

JK AMUWAKILISHA RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI MAZISHI YA LUCY KIBAKI NCHINI KENYA

$
0
0
Mwili wa mke wa aliyekuwa rais wa Kenya Mwai kibaki, mama Lucy Kibaki ukiwasili kwa hapo jana katika eneo la Bunge la Odhaya kaunti ya Njeri, mjini Nairobi nchini Kenya.


Rais Mstaafu wa Tanzania Dkt Jakaya Kikwete akisalimiana na Rais Mstaafu wa Kenya Mh.Mwai Kibaki kufuatia kufiwa na mke wake mpendwa Mama Lucy Kibaki mjini Nairobi,nchini Kenya anaeshuhudia kulia ni Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta.

Naibu Rais wa Kenya Mh.William Rutto na Mkewe wakimfariji Rais Mstaafu wa Kenya Mh. Mwai Kibaki wakati wa mazishi ya Mkewe Lucy Kibaki yaliyofanyika jana katika eneo la Bunge la Odhaya kaunti ya Njeri,mjini Nairobi nchini Kenya,Pichani shoto ni Rais Mstaafu awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Kikwete akishuhudia tukio hilo.
Rais wa Kenya Mh Uhuru Kenyatta akizungumza jambo na Rais Mstaafu wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Jakaya Kikwete wakati wa mazishi ya Mama Lucy Kibaki hapo jana mjini Nairobi,kulia ni mke wa Rais Uhuru Kenyatta, Bi Margaret Kenyatta. 
Rais Mstaafu wa Kenya, Mh.Mwai Kibaki akiweka udogo kwenye kaburi la Mke wake Mama Lucy Kibaki, wakati wa mazishi yaliyofanyika hapo jana katika eneo la Bunge la Odhaya kaunti ya Njeri, mjini Nairobi nchini Kenya.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta pamoja na Mkewe Margaret Kenyatta wakiweka udogo kwenye kaburi la mke wa aliyekuwa rais wa Kenya Mwai kibaki, mama Lucy Kibaki. Mazishi hayo yamefanyika jana katika eneo la Bunge la Odhaya kaunti ya Njeri, mjini Nairobi nchini Kenya. 
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta pamoja na Mkewe Margaret Kenyatta wakiweka shada la maua kwenye kaburi la mke wa aliyekuwa rais wa Kenya Mwai kibaki , mama Lucy Kibaki .Mazishi hayo yamefanyika jana katika eneo la Bunge la Odhaya kaunti ya Njeri,mjini Nairobi nchini Kenya,ambapo nchini Tanzania iliwakilishwa na Rais Mstaafu wa awamu ya nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Jakaya Kikwete kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.
---
Rais Mstaafu wa Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania Jakaya Kikwete amekuwa miongoni mwa viongozi wa ngazi za juu katika ukanda wa Jumuia ya Afrika Mashariki kuhudhuria hafla ya mazishi ya aliyekuwa mama wa Taifa la Kenya Bi Lucy Kibaki aliyefariki akiwa na miaka 82.

Marehemu Lucy Kibaki ametajwa na wanaomjua kama kiongozi aliyetetea mazingira safi ya kifamilia na alikuwa tayari kufanya kila jambo kuhifadhi utu na wema katika familia.

Kikwete ambaye aliwasilisha ujumbe wa Rais John Pombe Magufuli alisema kifo cha mama Lucy kibaki kimetokea wakati mchango wake ukiwa bado unahitajika katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na Naibu wake William Ruto waliohudhuria mazishi ya Bi Kibaki eneo la Bunge la Odhaya kaunti ya Njeri wamemtaja marehemu kama kiongozi aliyekuwa tayari kuhudumia taifa la Kenya.

RAIS DKT. MAGUFULI ATUNUKU KAMISHENI MAAFISA WAPYA 586 KATIKA CHUO CHA MAAFISA WAPYA WA JESHI LA WANANCHI MONDULI

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride kabla ya kutunuku Kamisheni kwa Maafisa Wapya 586 wa jeshi la Wananchi wa Tanzania kundi la 58/15 katika chuo cha kijeshi cha Monduli TMA mkoani Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akitunuku kamisheni kwa maafisa wapya 586 wa jeshi la Wananchi wa Tanzania kundi la 58/15 katika chuo cha Mafunzo ya kijeshi cha Monduli TMA mkoani Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Afisa Mpya wa cheo cha Luteni Usu, Nasra Rashid ambaye alifanya vizuri zaidi kuliko Maafisa Wanafunzi wanawake katika chuo cha kijeshi cha Monduli TMA mkoani Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya wananchi General Davis Mwamunyange mara baada ya kuwasili kwenye chuo cha Mafunzo Kijeshi cha Monduli TMA mkoani Arusha.
Maafisa Wanafunzi wakipita kwa mwendo wa haraka mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli kabla ya kutuniwa Kamisheni .
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Monduli TMA Meja Jenerali Paul Peter Massao kabla ya kutunuku Kamisheni kwa Maafisa Wapya 586 katika chuo hicho cha Monduli.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa wapya aliowatunuku Kamisheni katika cha Mafunzo Kijeshi cha Monduli TMA mkoani Arusha. Wengine katika picha ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya wananchi Jeneral Davis Mwamunyange , Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Monduli TMA Meja Jenerali Paul Peter Massao, Waziri wa Ulinzi Dkt. Hussein Mwinyi pamoja na Maafisa wa ngazi za juu katika Jeshi la Ulinzi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi wa Ngarenaro waliomsimamisha wakati akitokea kwenye chuo cha Mafunzo ya Kijenshi cha Monduli mkoani Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akitembea kikakamavu mara baada ya kutoka kukagua gwaride katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Monduli TMA mkoani Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo wakati akizungumza na wanaanchi wa kona ya Mbauda mkoani Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Mkuu wa majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Monduli mara baada ya kutazama picha za Majenerali wastaafu waliongoza Jeshi la Wananchi katika miaka ya nyuma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wakazi wa Kona ya Nairobi eneo la Arusha Tech mara baada ya kutoka kutunuku Kamisheni kwa maafisa Wapya katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Monduli mkoani Arusha. PICHA NA IKULU




























































TIGO YASHIRIKIANA NA MADEREVA WA BODABODA UKEREWE

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Joseph Mkirikiti, akihutubia madereva bodaboda wa wilaya yake jana wakati wa uzinduzi wa ushirikiano wa madereva hao na mtandao wa Tigo kwa ajili ya utendaji wao wa kutoa huduma ya usafiri ,Wa pili toka kulia ni Mkurugenzi wa Tigo  Kanda ya ziwa, Ali Maswanya na Mkurugenzi wa Mikakati wa Tigo Kobbina Awuah(kulia).
Mkurugenzi wa Kanda ya ziwa wa mtandao wa Tigo Ali Maswanya, akizungumza wakati wa kuzindua ushirikiano wao na madereva Bodaboda Wilaya ya Ukerewe jana, kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Joseph Mkirikiti na Mkurugenzi wa Mikakati wa Tigo Kobbina Awuah(kulia)
Madereva Bodaboda Wilaya ya Ukerewe Mkoani Mwanza, wakinyoosha mikono juu kuashilia kuzinduliwa kwa umoja wao na Mtandao wa Tigo, kwenye hafla iliyofanyika juzi.

RAIS DKT MAGUFULI ASHIRIKI IBADA YA JUMAPILI YA KUPAA KWA BWANA KATIKA PAROKIA YA TOLEO LA BWANA JIMBO LA ARUSHA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimia waumini aliposhiriki ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha leo Mei 8, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimia waumini aliposhiriki ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha leo Mei 8, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimia waumini aliposhiriki ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha leo Mei 8, 2016.
 Sehemu ya waumini wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli alipokuwa akiwasalimia  aliposhiriki ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha leo Mei 8, 2016.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimia na wanakwaya  aliposhiriki ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha leo Mei 8, 2016.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimia baadhi ya watawa aliposhiriki ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha leo Mei 8, 2016.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimia baadhi ya watawa aliposhiriki ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha leo Mei 8, 2016.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimia baadhi ya watawa aliposhiriki ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha leo Mei 8, 2016.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiagana na Padri Kiongozi Peter Pinto baada ya kushiriki ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha leo Mei 8, 2016. Kulia ni Pdr. Germin Longio na kushoto kwake ni Padri  wasaidizi Prosper Tesha na Furchong James Luis
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na vijana wa altari katika  ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha leo Mei 8, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akishiriki katika  ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha leo Mei 8, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akishiriki katika  ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha leo Mei 8, 2016.
 Sehemu ya waumini wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli alipokuwa akiwsalimia  aliposhiriki ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha leo Mei 8, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akishiriki katika  ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha leo Mei 8, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akishiriki katika  ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha leo Mei 8, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akishiriki katika  ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha leo Mei 8, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipokea zawadi ya Rozari  kutoka kwa Padri Kiongozi Peter Pinto  aliposhiriki ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha leo Mei 8, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akishukuru baada ya kupokea zawadi ya Rozari kutoka kwa Padri Kiongozi Peter Pinto  aliposhiriki ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha leo Mei 8, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipokea zawadi ya Biblia Takatifu kutoka kwa Padri Kiongozi Peter Pinto  aliposhiriki ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha leo Mei 8, 2016.

PICHA NA IKULU.

BENKI YA AZANIA YATOA MSAADA WA MILIONI 5 KWA WAZAZI HOSPITALI YA RUFAA YA AMANA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

Mkurugenzi wa Mikakati na Biashara wa Benki ya Azania, Mwanahiba Mzee (kulia), kwa niaba ya mkurugenzi mkuu wa benki hiyo, akimkabidhi kiongozi wa wagonjwa wa ndani wa Hospitali ya Rufaa ya Amana, Francis Yango (kushoto), dawa na vifaa vya usafi vyenye thamani ya sh.milioni 5 vilivyotolewa na benki hiyo ikiwa ni kuadhimisha siku ya wanawake Dar es Salaam leo asubuhi. Wapili kulia ni Muuguzi wa zamu,Getrude Massawe na  Antusa Lasway.
Wafanyakazi wa benki ya Azania wakiwa mbele ya vifaa na dawa walivyotoa msaada kwa Hospitali hiyo.
Makabidhiano zaidi ya msaada huo ukitolewa.
Vifaa hivyo vikipelekwa kwa walengwa.
Mkurugenzi wa Mikakati na Biashara wa Benki ya Azania, Mwanahiba Mzee (kushoto), akimkabidhi dawa za meno na sabuni, Judith Kimei katika wodi ya wazazi. Kulia ni Muuguzi wa zamu Antusa Lasway.
Ofisa wa benki hiyo, Neema Tumsifu akimjulia hali mtoto aliyezaliwa katika wodi hiyo.

Na Dotto Mwaibale

BENKI ya Azania imetoa msaada wa dawa na vifaa vya usafi vyenye thamani ya sh. milioni 5 wodi ya Wazazi katika Hospitali ya Rufaa ya Amani Ilala jijini Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo wakati wa kukabidhi msaada huo Dar es Salaam leo asubuhi, Mkurugenzi wa Mikakati na Biashara, Mwanahiba Mzee alisema kila mara benki hiyo imejiwekea utaratibu wa kusaidia jamii kulingana na ratiba yao ambapo mwaka huu waliona ni vema msaada huo waupeleke Hospitali hiyo.

Alisema mwaka katika kusherehekea sikukuu ya wanawake waliona ni vema kutoa msaada hasa katika wodi ya wajawazito ukizingia kuwa sikukuu hiyo inawahusu.

"Tumetoa msaada wa dawa mbalimbali kama dettol, spiritis, mabomba ya sindano, micoprostol, vitamini k na nyingine nyingi pamoja na vifaa vya usafi kama vile mifagio, sabuni na dawa za mswaki" alisema Mzee.

Kiongozi wa wagonjwa wa ndani wa Hospitali hiyo, Francis Yango akizungumza wakati wa kupokea msaada huo kwa niaba ya Mganga Mkuu, Shadrack Shimwela aliishukuru benki hiyo na kuwataka wadau wengine kujitokeza kusaidia.

"Tunawashukuru sana Azania Bank Ltd kwa msaada wenu lakini tunawaomba muende mbele zaidi kama mtaweza mtujengee walau wodi ambayo itaingiza walau vitanda 30 na wodi hiyo muandike jina la benki yenu kwani changamoto kubwa tulionayo kwa sasa licha ya kuwa na vitanda vya kutosha tuna uhaba wa wodi" alisema Yango.

MTANGAZAJI WA CNN RICHARD QUEST AFURAHISHWA NA VIVUTIO VUA UTALII TANZANIA KATIKA MAONESHO YA INDABA

$
0
0
Kwa mara nyingine tena Tanzania inashiriki katika onesho la kimataifa la Utalii la INDABA yanayofanyika huko Afrika Kusini maonesho hayo yalianza jana tarehe 7 Mei na yanatarajiwa kumalizika tarehe 9 Mei, 2016. jijini Durdan, Bodi ya Utalii (TTB) ndio waratibu wa onesho kwa upande wa Tanzania. Katika onesho hili TTB inashirki pamoja na taasisi za TANAPA na Mamlaka na Hifadhi ya Ngorongoro pamoja na makampuni mbalimbali binafsi Zaidi ya 30 ya sekta ya Utalii.

Katika siku yake ya kwanza Banda la Tanzania limetembelewa na wadau wengi wakiwemo watalii, waandishi wa habari za utalii, mawakala wa Utalii nk. Miongoni mwa watu mashuhuri waliotembelea Banda la Tanzania ni Mwandishi maarufu na mtangazaji wa Kimataifa kutoka Shirika la habari la CNN la Marekani Bwana Richard Quest ambaye alifurahishwa na vivutio vua utalii nchini Tanzania mara baada ya kupata maelezo kutoka kwa Maofisa wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB.
A05Mkurugenzi wa Masoko kutoka Bodi ya Utalii Tanzania TTB Bwa Philip Sebastian akimuonyesha jambo Mwandishi maarufu na mtangazaji wa Kimataifa kutoka Shirika la habari la CNN la Marekani Bwana Richard Quest wakati alipotembelea katika banda la Tanzania katika maonesho ya kimataifa ya Utalii Indaba jijini Durban nchini Afrika Kusini.
A3Mkurugenzi wa Masoko kutoka Bodi ya Utalii Tanzania TTB Bwa Philip Sebastian akimpa maelezo kuhusu vivutio vya utalii nchini Tanzania Mwandishi maarufu na mtangazaji wa Kimataifa kutoka Shirika la habari la CNN la Marekani Bwana Richard Quest wakati alipotembelea katika banda la Tanzania katika maonesho ya kimataifa ya Utalii Indaba jijini Durban nchini Afrika Kusini Katikati ni Bi Devotha Mdachi Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB.
A4A5 
Baadhi ya wagenimbalimbali waliotembelea katika banda la Tanzania katika maonesho ya Utalii ya Indaba yanayofanyika katika jiji la Durban nchini Afrika Kusini.
A1Mkurugenzi wa Masoko kutoka Bodi ya Utalii Tanzania TTB Bwa Philip Sebastian na Bi. Devotha Mdachi Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB. wakiwa na mmoja wa wageni aliyetembelea katika banda la Tanzania katika maonesho ya kimataifa ya Utalii Indaba jijini Durban nchini Afrika Kusini Katikati ni
A2 
Baadhi ya wageni wakipata taarifa mbalimbali kutoka katika banda la Tanzania.
A7 
Wageni mbalimbali wakiwa katika banda la Tanzania.

WANAMUZIKI WA NYIMBO ZA INJILI WAJIUNGA NA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA (NHIF)

$
0
0
 Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa, kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,  Joyce Hagu (wa pili kushoto), akimkabidhi Katibu wa Chama cha Muziki wa Injili Tanzania (Chamuita), Stellah Joel, kadi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),  katika hafla ya uzinduzi wa huduma hiyo kwa waimbaji wa nyimbo za injili uliofanyika Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto ni Mlezi wa chama hicho, Askofu Dk. Rejoyce Ndalima na Rais wa chama hicho, Ado Novemba.
 Hapa mwimbaji nguli wa nyimbo za injili Mzee Kitenzogu Makassy akikabidhiwa kadi yake baada ya kujiunga na NHIF.
 Burudani kutoka Kwaya ya Victorious Station ya Mwananyamala ikiendelea.
 Wanakwaya wakibadilishana mawazo katika uzinduzi huo.
 Burudani zikiendelea.
 Waimbaji wa kwaya ya Kanisa la Nabii Flora la Salasala wakitoa burudani.
 Wanakwaya ya Ukombozi ya Kanisa la Anglikana Tegeta wakionesha umahiri wa kumtukuza mungu kwa kuimba.
 Muonekano wa meza kuu katika uzinduzi huo.
 Ushuhuda ukitolewa kuhusu Mungu anavyowatendea watu wake miujuzi.
 Mlezi wa chama hicho, Askofu Dk. Rejoyce Ndalima (kushoto), akiwa ameketi na mgeni rasmi mama Joyce Hagu.
 Maofisa wa NHIF kutoka Wilaya ya Kinondoni wakiwa tayari kuwandikisha wanachama wapa katika uzinduzi huo. Kutoka kulia ni Derick Ndyetabula, Margaret Malangalila na Dk.Fortunatus Salala.
 Mchungaji David Nyanda ambaye ni muimbaji (wa pili kulia), akionesha manjonjo wakati akitoa burudani kwa kuimba katika uzinduzi huo.
 Katibu wa Chama cha Muziki wa Injili Tanzania (Chamuita), Stellah Joel akizungumza kwenye uzinduzi huo.
 Waimbaji na maofisa wa NHIF kutoka Kinondoni wakifuatilia uzinduzi huo.
 Rais wa Chamuita, Ado Novemba akizungumza kwenye uzinduzi huo.
 Furaha na shangwe zikiendelea katika uzinduzi huo watu wote mikono juuu.
 Meneja wa NHIF Wilaya ya Kinondoni, Constantine Makala akitoa darasa kuhusu faida za kujiunga na NHIF na jinsi ya kujiunga.
 Dk.Fortunatus Salala wa NHIF akizungumza kwenye uzinduzi huo.
 Mmoja wa waimbaji wa nyimbo za injili akielezea jinsi alivyonufaika na mfuko huo baada ya kujiunga miezi miwili iliyopita pamoja na mke wake.
 Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa, kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,  Joyce Hagu (kushoto), akionesha kadi za wanachama hao baada ya kuzizindua. Kulia ni Maadam Ruti Mwamfupe.

WABUNGE JAMES MBATIA NA JOSEPH SELASINI WATEMBELEA WAHANGA WA MAAFA YALIYOTOKANA NA MVUA ROMBO

$
0
0
Wabunge James Mbatia (Jimbo la Vunjo ) na Joseph Selasini wakiwa ofisini kwa Mkuu wa wilaya ya Rombo Lembris Kipuyo wakimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Maafa nchini Brigedia Jenerali Mbazi Msuya alipofika kutembelea wahanga wa mvua zilizonyesha hivi karibuni na kusababisha maafa.
Mbunge wa Jimbo la Rombo Joseph Selasini (kulia) akijaribu kutoa maelezo namna ambavyo wakazi wa kijiji cha Manda juu wilyani humo walivyo pata maafa yaliyotokana na kunyesha kwa mvua kubwa Aprili 24 na 25 mwaka huu.
Mbunge wa Jimbo la Vunjo ,James Mbatia akitoa pole kwa wakazi wa kijiji cha Manda juu wilayani alipokua akielekea kujionea namna ambavyo baadhi ya familia zilivyo athirika na mvua katika kjiji hicho na mtoto mmoja kupoteza maisha baada ya kifusi kuporomoka na kuangusha nyumba aliyokuwemo.
Mbunge wa Jimbo la Rombo ,Joseph Selasini (kushoto) akiongozana na Mkuu wa wilaya ya Rombo, Lembris Kupuyo wakielekea kuijionea athari ya mvua hizo.
Mbunge Mbatia akizungumza jambo mara baada ya kufika katika eneo lililokuwa na nyumba iliyobomoka baada ya kuporomokewa na kifusi na kusababisha kifo cha mtoto mmoja katika kijiji cha Manda juu wilayani Rombo.
Baadhi ya majirani wa familia iliyopoteza mtoto katika kijiji cha Manda wilayani Rombo baada ya nyumba aliyokuwemo mtoto kuporomokewa na kifusi kutokana na mvua kubwa zilizonyesha hivi karibuni.
Sehemu ya mabaki ya nyumba iliyoanguka.
Eneo la Shamba la Migomba kama linavyoonekana baada ya kifusi kuporomoka .
Mbunge wa Jimbo Rombo, Joseph Selasini akizungumza jambo wakati vongozi wakifika eneo hilo kujionea hali halisi.
Baadhi ya viongozi walioambatana na wabunge hao wakijaribu kupanda kwenda kujionea hali halisi ya athari zilizotokana na mvua hizo.
Watoto wakionekana wakiwa wamesimama kwa juu sehemu ambayo ni hatari kwa usalama wao hasa kutokana na maeneo mengi ya muinuko katika eneo hilo udongo kuanza kuporomoka.
Mbunge wa Jimbo la Vunjo, James Mbatia akitoa tahadhari kwa wananchi wanaoendelea kusihi katika maeneo hayo huku akiutaka uongozi wa kijiji ,kata na wilaya kuhakikisha hakuna familia inaendele kuishi maeneo hayo hadi pale mvua zitakapo koma.
Viongozi pamoja na wananchi katika eneo hilo wakifanya sala kabla ya kuondoka katika eneo hilo.
Viongozi waliofika katika kijiji hicho wakiondoka eneo la tukio.
Sehemu ya nyumba zilizo athirika hivi ndivyo ilivyoonekana.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

ELIMU BURE MKOMBOZI KWA WATOTO WA KIKE - WAZIRI UMMY MWALIMU

$
0
0

TANZIA: ANKAL MICHUZI AFIWA NA MWANAE

$
0
0
Ankal Issa Michuzi anasikitika kutangaza kifo cha mwanae Maggid Muhidin kilichotokea jana Jumapili huko Durban, Afrika Kusini, alikokuwa masomoni.

Mipango ya kuusafirisha mwili wa marehemu inafanywa, msiba utakuwa Tabata Mawenzi jijini Dar es salaam ambako ratiba ya mazishi itatoka mara tu baada ya mwili kuwasili.

Habari ziwafikie ndugu, jamaa, majirani na marafiki popote pale walipo.

Innalillah wa inna ilayhi raajiun.

FASTJET YACHUKUA UBINGWA WA BONANZA LA FASTJET SPORT EXTRA

$
0
0
Wachezaji wa Timu ya fastjet (wenye jezi nyeusi) wakichuana na wachezaji wa timu ya Diamond Trust Bank(DTB) wakati wa mashindano ya bonanza la fastjet sports Extra katika viwanja vya TCC Chang’ombe, Dar es Salaam hivi karibuni
Wachezaji wa Timu ya fastjet (wenye jezi nyeusi) wakichuana na wachezaji wa timu ya Diamond Trust Bank(DTB) wakati wa mashindano ya bonanza la fastjet sports Extra katika viwanja vya TCC Chang’ombe, Dar es Salaam hivi karibuni
Wachezaji wa Timu ya fastjet wakisheherekea ushindi waliopata dhidi ya timu ya Diamond Trust Bank(DTB) kwenye  mashindano ya bonanza la fastjet sports Extra yaliyofanyika katika viwanja vya TCC Chang’ombe, Dar es Salaam hivi karibun
Afisa Masoko na Mawasiliano wa fastjet, Lucy Mbogoro akionyesha cheti kilichozawadiwa kwa timu ya fastjet kama mshindi wa mashindano ya bonanza la fastjet sports Extra yaliyofanyika katika viwanja vya TCC Chang’ombe, Dar es Salaam hivi karibuni
Afisa Masoko na Mawasiliano wa fastjet, Lucy Mbogoro akionyesha cheti kilichozawadiwa kwa timu ya fastjet kama mshindi wa mashindano ya bonanza la fastjet sports Extra yaliyofanyika katika viwanja vya TCC Chang’ombe, Dar es Salaam hivi karibuni.
Viewing all 11654 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>