↧
RAIS DKT. MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA MKURUGENZI WA KITUO CHA UWEKEZAJI (TIC) BI. JULIET KAIRUKI
↧
TAASISI YA WANAUME KAZINI (MAN AT WORK) YALAANI VITENDO VYA USHOGA
Mwanzilishi wa Taasisi ya Wanaume Kazini (Man at Work), Maxwell Stansalaus akizungumza na katika mkutano Mkuu wa Wanaume uliofanyika jana na kuhudhuriwa na zaidi ya wanaume 700 ambao lengo lake ni kuwakumbusha wanaume wajibu walionao kwa familia, jamii na Taifa. Picha na Woinde Shizza, Arusha.
---
Na Woinde Shizza, Arusha---
Taasisi isiyo ya kiserikali ya Wanaume Kazini (Man at Work) imelaani vikali vitendo vya ushoga vinavyoshusha hadhi na thamani ya wanaume, hivyo wameitaka serikali kupiga vita vitendo hivyo ambavyo ni kunyume cha Maadili ya Tanzania na Afrika kwa Ujumla.
Muasisi wa Taasisi hiyo yenye makao yake jijini Arusha, Maxwell Stanslaus amesema kuwa Wanaume kazini wanapinga vikali vitendo vya ushoga kwa zaidi ya Asilimia 100% na kuwataka wanaojihusisha na vitendo hivyo kuacha Mara moja.
Maxwell alisema hayo jana katika mkutano Mkuu wa Wanaume kazini uliofanyika jijini hapa huku akisema kuwa taasisi hiyo imelenga kuhimiza wanaume kote nchini kutimiza wajibu wao na kutenda majukumu yao kama wanaume katika ngazi ya familia, jamii na taifa ili kuchochea maendeleo.
“Kwa sasa tunaona nidhamu ya serikali imerudi kutokana na Mwanaume mmoja tu Rais John Pombe Magufuli kuamua kutimiza wajibu wake hivyo basi Wanaume zaidi ya Milioni waliopo Tanzania wakiamua kutimiza majukumu yao na wajibu Tanzania itanyooka” Alisema Maxwell
Moja kati ya Wanaume waliohudhuria ni Joseph Mayagila alisema kuwa matatizo ya ushoga yanatokana na baadhi ya wanaume kujisahau na kujaribu kuwa wanawake, jukwaa hili la wanaume ni muhimu kuwakumbusha wanaume juu ya uanaume wao na kutimiza yale yanayowapasa kama wanaume.
Dokta Emmanuel Buganga ameeleza kuwa vuguvugu la wanawake kudai haki zao linatokana na baadhi ya wanaume kutotimiza wajibu wao kama wanaume wameacha majukumu yao ya kutunza familia zao na kuwa walezi na walinzi wa familia .
Mhamasishaji wa Masuala ya kijamii Samuel Sasali amesema kuwa wanaume wengi wamejisahau sana katika masuala ya malezi ya familia kwani usipomlea mtoto katika njia impasayo atakuja kukuaibisha ukubwani.
↧
↧
SUGU - FREEDOM
↧
TIGO, MGAHAWA WA SAMAKI SAMAKI WAINGIA UBIA

Meneja wa Huduma za Masoko Tigo, Olivier Prentout (kushoto) akiongea na wanahabari wakati wa kusaini mkataba wa ushirikiano wa kibiashara kati ya kampuni ya simu za mkononi ya Tigo na Mgahawa wa Samaki samaki. Kulia ni Afisa Mkuu wa Maendeleo wa Mgahawa Samaki samaki, Saum Wengert.
Kampuni ya simu inayoongoza kwa mtindo wa maisha ya kidijitali ya Tigo Tanzania, leo imeingia ubia na mgahawa ya Samaki Samaki ambao ilianzishwa tangu mwaka 2007 ukiwa na matawi matatu yaliyopo Mlimani City, City Centre na Masaki Jijini Dar es salaam, ambapo pande hizo mbili zimekubaliana kufanya kazi pamoja kwa kuleta bidhaa/huduma zao kwa wateja wa kila mmoja.
Akitangaza ubia huyo jijini Dar es salaam leo, Meneja wa Huduma za Masoko wa Tigo Oliver Prentout aliviambia vyombo vya habari kuwa ushirikiano huo ni moja ya alama ambazo zinajenga imani kwamba wateja wa Tigo ambao sasa wanaweza kujitambulisha kupitia migahawa ya Samaki Samaki
Tigo imeweka mtandao wa 4G LTE kwenye migahawa yote ya Samaki Samaki ili kuwawezesha wateja wake kufurahia intaneti ya kasi na ya haraka wakati wakila na kunywa kwenye migahawa hiyo inayouza vyakula vinavyotokana na mazao ya baharini hapa nchini.
“Tunaamini ushirikiano wetu utandelea kuonesha ni jinsi gani tumejikita kwenye kuboresha mabadiliko kwenye mtindo wa maisha ya kidijitali na kuongoza kwenye kutoa teknolojia ya kisasa na ubunifu kwa wateja wetu, alisema Meneja Mkuu wa Tigo Diego Gutierrez.
Aidha Muasisi na Mkurugenzi wa migahawa ya Samaki Samaki, Bw. Carlos Bastos alisema Samaki Samaki wanawafanyia kazi Watanzania na wameungana na Tigo ambayo ni kampuni ya simu inayooongoza kwa ubunifu nchini kuwapatia wateja wake kile ambacho wamekisubiri kwa muda mrefu kwa jinsi huduma za Tigo zilivyo hususani uzoefu kwenye mtandao wa bure na wa kasi wa intaneti. Kwa ushirikiano huu tutawapatia wateja wetu miradi mingi mipya, maboresho pamoja na ofa.
Kufanya kazi na Tigo sio kwamba kunahusu sisi kupata fedha tu, bali inahusu ni nini cha ziada tunachoweza kuwapatia wateja wetu na hali kadhalika ni kwa kiasi gani tunaweza kujifunza kufanya kazi pamoja na kampuni iliyo na uzoefu mkubwa na ya kimataifa.
Tunaweza kuwa ni mgahawa unaoongoza kwa vyakula vinavyotokan na mzao ya baharini, lakini tunapenda kufanya jambo zaidi kwa ajili ya wateja wetu.
Huduma za Tigo zinazotarajiwa kuwepo kwenye migahawa ya Samaki Samaki ni pamoja huduma ya bure ya intaneti bila nyaya (WiFi), Tigo Pesa na Tigo Music.
↧
RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AWASILI MKOANI DODOMA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma wakati akitokea mjini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Charles Kitwanga mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.
Msafara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ukielekea Dodoma kutokea mjini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU.
↧
↧
WANANCHI WA ITOBO, ITIRIMA - SIMIYU WAASWA KUZAA KWA KUFUATA UZAZI WA MPANGO
Mtaalam wa masuala ya uzazi wa mpango kutoka Marie Stopes Tanzania, Bi. Ester Meena akitoa elimu ya uzazi wa mpango kwa wananchi wa kijiji cha Itobo, Itirima - Simiyu mapema wiki iliyopita. Elimu hiyo ya uzazi wa mpango iliendana na huduma ya upimaji wa afya ikiwa ni pamoja na kutoa huduma ya uzazi wa mpango. Picha/Video na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.

Wananchi wa kijiji cha Itobo, Itirima - Simiyu wakipatiwa elimu ya uzazi wa mpango.

Mtaalam wa masuala ya uzazi wa mpango kutoka Marie Stopes Tanzania, Bi. Ester Meena akitoa elimu ya uzazi wa mpango kwa wananchi wa kijiji cha Itobo, Itirima.
---
Na Cathbert Kajuna - Itirima, Simiyu.
Wananchi wa Kijiji cha Itobo, Itirima - Simiyu wameaswa kuachana na mila za kuzaa watoto wasio kuwa na idadi ili kuepusha taifa lenye wategemezi wengi.
Akizungumza katika mafunzo ya Uzazi wa Mpango yaliyotolewa wiki iliyopita na Mtaalam wa masuala ya uzazi wa mpango kutoka Marie Stopes Tanzania, Bi. Ester Meena alisema kuwa kuna haja ya wazazi hasa waishio vijinini kuacha dhana ya kuzaa ovyo kama wanyama bila mpangilio jambo linalowafanya kuendea kuwa maskini.
"Nawaasa wananchi wa Kijiji cha Mitobo kuache mila potofu za kuzaa kila mwaka mimba kila mwaka mtoto maana mtakosa kuwa na maendeleo, nnakuta mtu anawatoto 10 - 15 jambo linalopelekea kuwa omba omba kwa vile atashindwa kuwahudumia," alisema Meena.
Bi. Meena aliwashukuru wananchi wa Kijiji cha Mitobo kwa kuweza kujitokeza kwa wingi kupata elimu ya uzazi wa mpango.
Akiongea mara baada ya kumaliza mafunzo hayo Bi. Ester Meena alisema kuwa muitikio wa wananchi katika kupata elimu ya uzazi wa mpango umekuwa mkubwa jambo linaloleta faraja kwa vile linaweza kupunguza idadi ya watu.
↧
CAG AONEKANA KUPOTOSHA BUNGE; BOHARI YA DAWA (MSD) YASEMA HAKUNA DAWA NA VIFAA TIBA VILIVYOPO NJIANI KUELEKEA MUHIMBILI
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu akionesha moja ya nyaraka inayoonesha upelekaji wa dawa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam leo, wakati akitoa ufafanuzi kuhusu dawa za shilingi bilioni mbili kuwa njiani kutoka MSD Keko kwenda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili tangu mwaka 2012.
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu (kulia), akizungumza katika mkutano huo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala, Victoria Elangwa na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Sako Mwakalobo.
Ofisa Uhusiano Mkuu wa MSD, Etty Kusiluka (kulia), akizungumza katika mkutano huo wakati akimkaribisha Mkurugenzi Mkuu wa MSD (kushoto), kuzungumza na wanahabari. Katikati ni Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja na Shughuli za Kanda, Terry Edward.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Mkutano na wanahabari ukiendelea
Na Dotto Mwaibale
BOHARI ya Dawa (MSD) imetoa ufafanuzi kuhusu dawa za sh.bilioni mbili kuwa njiani kutoka Bohari ya Dawa ya Keko kwenda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili tangu mwaka 2012.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu alisema hakuna dawa ambazo ziko njiani tangu mwaka 2012 kutoka Bohari ya Dawa kwenda Muhimbili kama ilivyodaiwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Bungeni.
Bwanakunu alisema kuwa ripoti ya CAG ilionesha dawa na vifaa tiba vyenye thamani ya sh.bilioni 2.03 havikuwa vimefika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili tangu Mei 2012 licha ya kuonekana kwenye ankara 23 na Bohari ya Dawa.
"Tunapenda kutoa ufafanuzi kuwa ankara hizo sio kwamba dawa hazikufika hospitalini hapo, bali hazikuonekana kwenye vitabu vya kupokelea mali vya Hospitali ya Muhimbili" alisema Bwanakunu.
Alisema kwamba baada ya kupitia nyaraka zake, Bohari ya Dawa mpaka sasa imefanikiwa kupata uthibitisho wa hati za kupelekea mali za dawa na vifaa tiba vyote vilivyopokelewa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambavyo ni pamoja na dawa za figo na moyo ambazo zilikwishapelekwa Muhimbili.
Aliongeza kuwa pamoja na juhudi za MSD imewasiliana na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ili kuainisha taarifa za kwenye ankara na shehena ya dawa na vifaa tiba vilivyopelekwa hospitalini hapo kwani utaratibu wa kupeleka na kukabidhi dawa hospitalini unamlazimu mpokeaji kusaini ankara ya kupeleka mali ambazo zote zipo MSD.
Akitolea ufafanuzi kuhusu picha zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii za gari aina ya lori lenye herufi "MSD" na kutoa maelezo kuwa ni gari la MSD amesema nembo inayoonekana kwenye gari hilo siyo ya Bohari ya Dawa.
Katika ripoti ya CAG ilionesha kwamba madawa na vifaa tiba ambavyo havikupokelewa kwa muda mrefu kutoka MSD vilikuwa vyenye thamani ya sh.bilioni 2.03 ambapo katika hali ya haikutajiwa kuchukua zaidi ya wiki moja kufikishwa sehemu husika ukizingatia ofisi zao ziko Dar es Salaam.
↧
KONGAMANO YA DICOTA 2016 DALLAS, TEXAS LAENDELEA TENA IJUMAA
Bwn. Lunda Asumani akitoa maelekezo kwa wadau mbalimbali waliokuja kuongea kwenye kongamano la DICOTA 2016 linalofanyika Dalaas, Texas nchini Mrekani. Picha na Vijimambo/Kwanza production.
Rais wa DICOTA Ndaga Mwakabuta akielezea malengo ya DICOTA kwenye kongamano la DICOTA 2016 lililofanyika siku ya Ijumaa April 29, 2016 katika hotel ya Hyatt Regency.
Bob Townsend concel member wa mji wa Richardson, Texas akiongea machche.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Wilson Masilingi akisoma hotuba ya Mhe. Rais John Pombe Magufuli kwa Diaspora.
Balozi Anisa Mbega Mkuu wa kitengo cha Diaspora Wizara ya mambo ya nje, Ushirikiano Afika Mashariki , Kikanda na Kimataifa akisoma hotuba ujumbe kutoka Wizara hiyo.
CHINI NI JUMUIYA BAADHI YA VIONGOZI WA JUMUIYA ZA WATANZANIA USA
↧
MBATIA AMUONGOZA MKURUGENZI WA IDARA YA MAAFA NCHINI KUTEMBELEA MAENEO YALIYOATHIRIKA KWA MAFURIKO

Mbunge wa jimbo la Vunjo ,James Mbatia akitoa maelekezo mara baada ya kutembelea baadhi ya maeneo yaliyoathirika kwa mafuriko.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
↧
↧
KAMBI TIBA YA GSM NA MOI: OPARESHENI 55 ZA VICHWA VIKUBWA ZAFANIKIWA BUGANDO
Jumla ya watoto 55 wamenatarajiwa kufanyiwa upasuaji katika kambi ya tiba ya watoto wenye kichwa kikubwa na mgongo wazi, iliyowekwa katika hospitali ya Bugando jijini Mwanza siku nne mfululizo, kufuatia tatizo la kichwa kikubwa walilozaliwa nalo, chini ya udhamini wa taasisi ya GSM Foundation. Zoezi litakalofanyika katika mikoa mitano ikiwa ni awamu ya kwanza kati ya nne zinazotarajiwa kufanyika Tanzania nzima.
Akiongea wakati wa kufunga kambi hiyo rasmi jioni ya leo, Daktari Bingwa wa upasuaji na mifupa kutoka Taasisi ya Mifupa MOI, Dk Othman Kiloloma(Pichani Juu) ambaye pia ni mratibu wa kambi hiyo aliishukuru taasisi ya GSM kwa kuamua kulichukua tatizo hilo ambalo ameliita kuwa ni kubwa ukilinganisha na jinsi linavyochukuliwa na jamii ya watanzania.
Dk Kiloloma aliwaambia wanahabari kwamba jumla ya watoto 2000 huzaliwa na vichwa vikubwa katika kanda ya Ziwa peke yake, na mtaalamu wa kuhudumia wagonjwa wa namna hii ni mmoja tu ambapo pia kwa Tanzania nzima, wataalamu wa upasuaji wa watoto wenye vichwa vikubwa wako tisa tu.
Cha kusikitisha ni kwamba kati ya hao, ni wachache sana hurudi kwa ajili ya matibabu bali wengi wao hufariki kwa kufichwa ndani na wazazi wao aidha kwa imani za kishirikina ama kushindwa kwa wazazi kumudu gharama za matibabu.
Mpaka jioni ya leo, ambayo ni siku ya nne tangu kuanza kwa kambi hii, jumla ya watoto 55 walikuwa wameshafanyiwa upasuaji, ambapo siku ya kwanza, walifanyiwa watoto 16, siku ya pili wakafanyiwa watoto 17, siku ya tatu wakafanyiwa watoto 12, na leo wamefanyiwa watoto 10.
Mratibu huyo ambaye pia ni Naibu Mkurugenzi wa Taasisi ya Mifupa na Upasuaji (MOI), Dk Othman Kiloloma, amebainisha kwamba changamoto kubwa inayotokea kwa jamii linapokuja suala la watoto wenye vichwa vukubwa na mgongo wazi ni gharama za upasuaji, ambapo gharama ya upasuaji kwa mtoto mmoja ni kati ya shilingi laki saba za kitanzania mpaka Milioni moja.
"Watoto wengi huzaliwa katika mazingira duni na wazazi wasiokuwa na nguvu ya kiuchumi, hali inayosababisha wengi wao kuwaficha ndani huku wakiwahusisha na imani za kishirikina", alifafanua Dk Kiloloma.
Dk Kiloloma amesema zaidi ya watoto 4000 huzaliwa kila mwaka wakiwa na tatizo la kichwa kikubwa, lakini wanaorudi Hospitali kwa ajili ya tiba nhawazidi laki nne, swali kubwa ambalo jamii hujiuliza ni kuhusiana na watoto ambao hawafiki hospitalini huishia wapi?
Kwa upande wake, Halfan Kiwamba, Afisa Mawasiliano wa Taasisi ya GSM Foundation ambao ndio washamini wakuu wa kambi hizo amesema, taasisi yake imeamua kuokoa maisha y watoto hao ambao ni nguvukazi ya taifa la kesho na inalifanya hilo ikiwa ni moja ya mikakati yake katika kurudisha fadhila kwa jamii ya kitanzania ambao ni wateja wakubwa wa bidhaa za GSM. Kiwamba amesema taasisi yake ina lengo la kuhakikisha kwamba wananchi wa Tanzania hasa watoto ambao ni wa taifa ya kesho wanao msingi wa nguvu kazi kwa ajili ya maisha yao ambapo vitu vikubwa ni elimu boira pamoja na Afya.
Kwa upande wake Meneja wa Taasisi ya GSM Shannon Kiwamba amesema wakati mwingine ni vigumu kuingia katika maisha ya kila mwananchi na kumsaidia mahitaji yake, lakini akiwa na uhakika wa Afya na elimu anaweza kwenda mbali akijumlisha na jitihada zake.
Hivyo amewaomba watanzania kujitokeza wanaposikia taasisi yake inatoa huduma ili kufaidika nayo.
Kambi ya tiba ya GSM inaondoka kesho juijini Mwanza kuelekea Shinyanga ambapo itaweka kambi kwa siku tatu.
↧
WAFANYAKAZI WA MFUKO WA PENSHENI WA PPF WASHIRIKI SHEREHE ZA MEI MOSI MKOA WA DAR ES SALAAM
Baadhi ya Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni PPF, wakiwa katika maandamano wakipita mbele ya mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (hayupo pichani) wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) zilizofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, leo. Picha na Mafoto Blog.

↧
BWANA SAMWEL MILEGO AFUNGA NDOA NA BI. FLORIDA KAHATANO JIJINI DAR

Bwana harusi Samwel Milego na Bi. Florida Kahatano wakionyesha vyeti vyao mara baada ya kumaliza kufunga ndoa yao takatifu Jerusalem church of God lililoko Yombo Vituka jijini Dar es Salaam Jumamosi Aprili 30, 2016. PICHA ZOTE NA CATHBERT KAJUNA WA KAJUNASON BLOG.

Bwana harusi Samwel Milego akimvalisha pete Bibi harusi Florida Kahatano wakati wakifunga ndoa takatifu Jerusalem church of God lililoko Yombo Vituka jijini Dar es Salaam Jumamosi Aprili 30, 2016.

Bwana harusi Samwel Milego akila kiapo mbele ya mkewe Bi. Florida Kahatano wakati wakifunga ndoa takatifu Jerusalem church of God lililoko Yombo Vituka jijini Dar es Salaam Jumamosi Aprili 30, 2016.

Bibi harusi Florida Kahatano akimvalisha pete mumewe Samwel Milego wakati wakifunga ndoa takatifu Jerusalem church of God lililoko Yombo Vituka jijini Dar es Salaam Jumamosi Aprili 30, 2016.

Wachungaji wa kanisa la Jerusalem church of God lililoko Yombo Vituka jijini Dar es Salaam wakiwaombea Bwana harusi Samwel Milego na mkewe Bi. Florida Kahatano mara baada ya kufunga.

Bwana harusi Samwel Milego akisaini katika cheti huku akishuhudiwa na mkewe Bi. Florida Kahatano mara baada ya kufunga ndoa takatifu Jerusalem church of God lililoko Yombo Vituka jijini Dar es Salaam Jumamosi Aprili 30, 2016.

Mchungaji wa Jerusalem church of God lililoko Yombo Vituka jijini Dar es Salaam akimkabidhi cheti Bwana harusi Samwel Milego huku akisindikizwa na msimamizi wake Bw. Donald Byakwaga.

Mchungaji wa Jerusalem church of God lililoko Yombo Vituka jijini Dar es Salaam akimkabidhi cheti Bibi harusi Florida Kahatano ambaye alikuwa na msimamizi wake Bi. Celina Donald.

Wazazi wakiwapongeza watoto wao mara baada ya kumaliza kufunga ndoa.

Baba wa Bibi Harusi Florida, Bw. Kahatano akiwa na mkewe wakitoa kibali cha mwanae kufunga ndoa na Bw. Samwel Milego.
Bwana harusi Samwel Milego (kushoto) akisindikizwa na msimamizi wake Bw. Donald Byakwaga kuingia Jerusalem church of God lililoko Yombo Vituka jijini Dar es Salaam Jumamosi Aprili 30, 2016.
Bibi harusi Florida Kahatano akiingia kanisani.
Watu waliohudhuria ibada.
Bwana harusi Samwel Milego na Bi. Florida Kahatano akitoka kanisani kwa nderemo na vifijo.
Bwana harusi Samwel Milego na Bi. Florida Kahatano wakiwa katika nyuso za furaha.
↧
MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI, WCF, WASHIRIKI SHEREHE ZA MEI MOSI KWA MARA YA KWANZA
Baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, WCF, wakishiriki matembezi ya kilele cha siku ya Wafanyakazi Duniani (May day), hapa matembezi yakiwa barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam, Mei 1,
2016.
2016.
NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said.
Wafanyakazi wa WCF wakipita mbele ya jukwaa kuu la uwanja wa Uhuruwakati wa matembezi ya kilele cha siku ya wafanyakazi Duniani
Matembezi yakiwa yameingia Uwanja wa Uhuru
Matembezi yakipita barabara ya Chang'ombe
Matembezi yakiendelea barabara ya Chang'ombe
Matembezi yakiwa barabara ya Uwanaja wa Taifa
Baadhi ya wafanyakazi wakiwa kwenye matembezi hayo, hapa nibarabara ya Chang'ombe
Baadhi ya wafanyakazi wa WCF, wakimsikiliza mwenzao aliyevaat-shirtyenye ujumbe maalum wa Mfuko huo “WCF inatoa Fidia Stahiki kwa Wafanyakazi wote wa Sekta ya Ummana Binafsi”.
Mkuu wa Mkoa wa Dar esSalaam, Mh. Paul Makonda, (kulia), akiteta jambo na kiongozi wa Shirikisho la Wafanyakazi mkoa wa Dar es Salaam, wakati wa kilele cha May Day uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa WCF wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukamilisha matembezi hayo kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa WCF wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukamilisha matembezi hayo kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
↧
↧
RAIS DKT. MAGUFULI AHUTUBIA WAFANYAKAZI KATIKA KILELE CHA MAADHIMISHO YA SHEREHE ZA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI ZILIZOFANYIKA KITAIFA MKOANI DODOMA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia mamia ya Wafanyakazi katika kilele cha Maadhimisho ya Sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani zulizofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameshikana mikono na viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi TUCTA wakati wakiimba wimbo wa Mshikamano Daima katika kilele cha Maadhimisho ya Sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma .
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi kombe la ushindi wa jumla kwa Rais wa TUCTA Gratian Mukoba katika kilele cha Maadhimisho ya Sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Cheti cha Mfanyakazi bora kutoka Ofisi ya Rais Ikulu Ndugu Peter Chisunga katika kilele cha Maadhimisho ya Sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia namna ya uokozi katika majanga mablimbali yanayotokea Migodini nje ya uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia jinsi mzani unavyofanyakazi katika banda la maonesho la Mamlaka ya Bandari Tanzania TPA nje ya uwanja wa Jamhuri Mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiifurahi picha yake ya kuchoraalipokabidhiwa wakati anakagua mabanda ya Maonesho katika katika kilele cha Maadhimisho ya Sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniania zilizofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Jamhuri Mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza maelezo kutoka kwenye banda la mamlaka ya udhibiti wa mifuko ya hifadhi ya jamii SSRA mjini Dodoma .
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza maelezo kutoka kwenye banda la Wakala wa Afya na Usalama mahala pa kazi OSHA mkoani Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Wafanyakazi wa Tanzania TUCTA Ndugu Nicholas Mgaya mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Jamhuri Mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa TUCTA Gratian Mukoba wakati alipowasili katika katika viwanja vya Jamhuri Mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wazee wa mkoa wa Dodoma mara baada ya kuhutubia katika kilele cha Maadhimisho hayo ya siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika Kitaifa Mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono kuagana na mamia ya wafanyakazi katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
Sehemu ndogo ikionesha wafanyakazi waliojitokeza katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma katika kilele cha sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika Kitaifa Mkoani Dodoma. PICHA NA IKULU
↧
MRADI WA KUKUZA TEKNOLOJIA KUPITIA WATOTO XPRIZE WAZINDULIWA DODOMA

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Simon Msanjila (kulia) akitoa hotuba ya ufunguzi wa mradi wa kukuza teknolojia kupitia watoto XPRIZE uliofanyika mjini Dodoma mwishoni mwa wiki. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mwandamizi wa Uendeshaji kutoka Taasisi ya XPRIZE, Matt Keller, Kaimu Mkurugezi wa Elimu ya Msingi wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Kassim Kaoneka na Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bi. Zulmira Rodrigues. (Picha na Modewjiblog)
Kwa kutambua uwezo walionao watoto katika kubuni vitu mbalimbali, Taasisi ya XPRIZE iliyo na makazi yake nchini Marekani, imezindua mradi wa XPRIZE nchini ambao utahusisha watoto ambao hawapo shuleni ukiwa na malengo ya kukuza teknolojia ya dunia kwa kutumia uwezo walionao watoto wa miaka 5-12.
Akielezea mradi huo, Mkurugenzi Mwandamizi wa Uendeshaji kutoka Taasisi ya XPRIZE, Matt Keller, alisema kuwa wameanzisha mradi huo kwa kutambua uwezo ambao wanao watoto na kama wakiwezeshwa wanauwezo wa kufanya mambo makubwa.
Alisema dunia ina watoto wengi ambao hawapo shuleni kwa sababu mbalimbali na hivyo mradi huo utakwenda kufanyika kupitia watoto ambao hawapo mashuleni na watawapatia vifaa mbalimbali ili waweze kupimwa uwezo wao katika kazi zinazohusiana na teknolojia.
“Dunia ina watoto Milioni 57 ambao hawapo shuleni tutawatumia kama hao kwa sababu tunaamini watoto wanaweza kufanya mambo mengi lakini wanachohitaji ni kuwezeshwa ili waweze kukamilisha mambo wanayofanya,” alisema Keller.
Nae Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Zulmira Rodrigues alisema kuwa ni muda muafaka kwa watoto kusaidiwa kupata elimu kwa njia ya kiteknolojia hasa kwa wakati uliopo ambao teknolojia inatumika zaidi katika kurahisisha kazi mbalimbali.
Alisema ni muhimu kwa Tanzania kuanza kutumia mifumo ya teknolojia hasa katika kipindi hiki ambacho nchi ipo katika hatua za kuelekea uchumi wa kati kwani kwa kufanya hivyo itaweza kurahisha kufikiwa malengo kwa muda muafaka ambao umepangwa.
“Ni wakati kwa watoto kupata elimu ya teknolojia, haijalishi hayupo shuleni kwa kipindi hiki teknolojia inatumika zaidi na hii itasaidia wakati huu ambao nchi (Tanzania) inakwenda katika uchumi wa kati,” alisema Bi. Rodrigues.

Nae Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Prof. Simon Msanjila alisema kuwa serikali imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali ili kuwawezesha watoto kupata elimu ya teknolojia lakini inakuwa ni ngumu kufikia malengo hayo yenyewe hivyo ni tumaini lao mradi huo utafanikiwa.
Alisema ni muhimu kwa watoto kupatiwa elimu ya teknolojia kwa dunia ya sasa na serikali ipo tayari kushirikiana nao kwa pamoja ili mradi huo uweze kufanyika kama jinsi umevyopangwa na Taasisi ya XPRIZE ambao ndiyo waanzilishi wa mradi huo ambao unataraji pia kufanyika nchi mbalimbali duniani.
“Unaposema dunia inakuwa kijiji ina maana unazungumza kuhusu teknolojia kutokana na kusogeza kila jambo karibu na kwa haraka ni ngumu kwa serikali kufanya yenyewe lakini wanapopattikana watu wanaosaidia inakuwa vizuri na pia inasaidia kukuza teknolojia nchini,” alisema Prof. Msanjila.
Nae Afisa Mradi wa Elimu wa UNESCO, Faith Shayo alisema mradi huo nchini utaanza kwa majaribio katika makundi 200 kutoka mkoa wa Tanga katika wilaya ya Lushoro, Korogwe, Muheza, Pangani, Mkinga, Handeni na Kilindi na mkoa wa Arusha utafanyika katika wilaya ya Ngorongoro ambapo watoto hao watapatiwa simu zilizo na muundo wa tablet na sola za kuchajia na watatumia 'tablet' kwa kusoma, kuandika na kuhesabu na baada ya hapo watakuwa wakichaguliwa kutokana na uwezo binafsi.

Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bi. Zulmira Rodrigues akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa Mradi wa XPRIZE uliofanyika mjini Dodoma mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Kaimu Mkurugezi wa Elimu ya Msingi wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Kassim Kaoneka. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Prof. Simon Msanjila.

Naibu wa Programu kutoka Shirika la Chakula Duniani (WFP) nchini, Marina Negroponte (kulia) akizungumzia nafasi ya Shirika lake katika utekelezaji wa mradi wa XPRIZE katika hafla fupi ya uzinduzi wa mradi huo iliyofanyika mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.

Pichani juu na chini ni Mkurugenzi Mwandamizi wa Mafunzo kutoka Taasisi ya XPRIZE, Matt Keller akizungumzia malengo ya mradi huo wakati wa hafla fupi ya uzinduzi iliyofanyika mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.

Kutoka kulia ni Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Zulmira Rodrigues, Kaimu Mkurugezi wa Elimu ya Msingi wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Kassim Kaoneka, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Prof. Simon Msanjila wakifuatilia kwa umakini 'power point presentation' ya jinsi mradi huo utakavyotekelezeka nchini.

Afisa Mradi wa Elimu wa UNESCO, Faith Shayo akizungumzia utekelezaji wa mradi huo wa kukuza teknolojia kupitia watoto XPRIZE na wadau watakaoshirikiana nao katika kutekeleza.

Kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugezi wa Elimu ya Msingi wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Kassim Kaoneka, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Prof. Simon Msanjila, Mkurugenzi wa Elimu ya Msingi kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Sarah Mlaki, waandishi wa habari pamoja na wadau wa sekta elimu waliohudhuria uzinduzi huo, mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.

Naibu wa Programu wa Shirika la Chakula Duniani (WFP) nchini, Marina Negroponte akiandika mambo muhimu kwenye uzinduzi wa mradi wa XPRIZE.

Afisa mradi wa Elimu wa Unesco, Dar es Salaam, Faith Shayo akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mwandamizi wa Uendeshaji kutoka Taasisi ya XPRIZE, Matt Keller wakati wa uzinduzi wa mradi wa XPRIZE uliofanyika mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.

Baadhi ya wadau wa sekta ya elimu, waandishi wa habari na viongozi kutoka Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi waliohudhuria uzinduzi huo uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Hoteli ya Veta, mjini Dodoma.

Baadhi ya wageni waalikwa wakibadilishana mawazo kwenye uzinduzi wa mradi wa XPRIZE uliofanyika mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.

Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Simon Msanjila akiagana na Mkurugenzi Mwandamizi wa Uendeshaji kutoka Taasisi ya XPRIZE, Matt Keller....Kulia Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Zulmira Rodrigues na kushoto ni Makamu wa Rais anayeshughulikia uendeshaji wa XPRIZE Foundation, Joel Carnes.
↧
KAMPUNI YA PUMA ENERGY TANZANIA YATANGAZA WASHINDI WA SHINDANO LA KAMPENI YA USALAMA BARABARANI KWA SHULE ZA MSINGI
KAMPUNI ya Puma Energy Tanzania yawakabidhi zawadi washindi wa shindano la kampeni ya Usalama barabarani lililoshindanisha shule sita za jijini Dar es Salaam ambazo ni Maweni, Kimara Baruti, Oysterbay, Gongolamboto Jeshini na Mji Mwema.
Ndoto kubwa ya kampuni ya Puma Energy Tanzania katika kuhakikisha usalama wa wanafunzi wakati wa kuvuka barabara ni kushirikisha shule zote za msingi Tanzania ili kuhakikisha watoto wako salama na ajali za barabarani.
hayo yamesemwa na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Energy Tanzania, Philippe Corsalrtti wakati akizungumza na wanafunzi wa shule za Msingi sita za jijini Dar es Salaam katika wa hafla fupi ya kutafuta mshindi na kumtangaza kutokana na mchoro alioutoa kama unahamasisha uasalama barabarani.
Nae Kamishina Msaidizi wa Polisi(ACP), Fortunatus Musilimu
amewaasa madereva watakiwa kufuata sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajali na madhara yanayojitokeza barabarani hasa wakiona wanafunzi wanavuka barabara, ikiwa takwimu za mwaka 2015 zinaonyesha kuwa wanafunzi 78 walipoteza na majeruhi 191 katika matukio tofauti hapa nchini
Maeneo hatari sana kwa wanafunzi kwa jijini la Dar es Salaam amesema kuwa ni Lumumba, Mikumi, Mtambani, Boko-Basihaya Bunju na Kongowe.
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Energy Tanzania, Philippe Corsalrtti akizungumza katika hafla ya kuwatangaza washindi wa kampeni ya Uasalama barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi zilizopo jijini Dar es Salaam. Shindano hilo lililoshirikisha shule sita za jijini Dar es Salaam kama, Shule ya Msingi Maweni, Kimara Baruti, Oysterbay, Gongolamboto Jeshini na Mji Mwema. Katika shindano hilo shule ya Msingi Gongolamboto Jeshini iliyopo manispaa ya Ilala iliibuka mshindi kwa kuwa na wanafunzi wawili kwa kufanikiwa kuchora mchoro unaoweza kutoa tahadhari katika usalama barabarani.
Mkurugenzi wa Afrika wa kampuni ya AMENDI, Tom Bishop akizungumza katika hafla ya kuwakabidhi washindi wa shindano la kampeni ya usalama barabarani lililoandaliwa na kampuni ya Puma Enegy Tanzania jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Kamishina Msaidizi wa Polisi(ACP), Fortunatus Musilimu akizungumza na wanafunzi wa shule sita za jijini Dar es Salaam katika kutangaza mshindi wa shindano la Kapeni ya Usalama barabaranu kwa shule za msingi na kutangaza mshindi wa shindano hilo lililofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Kauli mbiu ya kuwalinda watoto na ajali za barabarani ambayo ni "Kwa pamoja hatutaki ajali tunataka kuishi na maendeleo" alisema Kamishina Msaidizi wa Polisi(ACP) huyo.![]()

Baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi za jijini Dar es Salaam wakiwa katika hafla ya kuwatafuta washindi wa shindano la kampeni ya usalama barabarani kwa shule za msingi iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.![]()

Meza kuu wakiwa katika hafla ya kuwatafuta na kuwakabidhi washindi wa shindano la kampeni ya Usalama barabarani kwa shule za msingi sita za jijini Dra es Salaam.
Mwalimu akiwaelezea wanafunzi wake igizo la jinsi ya kuepukana na ajali za barabarani.
Mshehereshaji akiwasaidia wanafunzi kuimba wimbo wa kuhamasisha usalama barabarani wakati wanafunzi wanavuka barabara.
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Energy Tanzania, Philippe Corsalrtti na Kamishina Msaidizi wa Polisi(ACP), Fortunatus Musilimu wakiangalia picha kwaajili ya kupata picha inayoonyesha ujumbe wa kampeni ya usalama barabarani kwa shule za msingi sita za jijini Dar es Salaam.
Kamishina Msaidizi wa Polisi(ACP), Fortunatus Musilimu akionyesha picha ya mshindi wa tatu katika shindano la Kampeni ya Usalama Barabarani kwa shule za msingi shindano lililodhaminiwa na kampuni ya Puma Energy Tanzania. Mshindi wa Tatu ni Shaib Abdala darasa la 5 wa shule ya msingi, Gongolamboto Jeshini. kushoto aliyeshika begi ni Meneja Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Energy Tanzania, Philippe Corsalrtti.
Kamishina Msaidizi wa Polisi(ACP), Fortunatus Musilimu akionyesha picha ya mshindi wa pili katika shindano la kuchora mchoro unaotoa taarifa ya usalama barabarani, Abdala Husein wa shule ya msingi Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Mshindi wa Kwanza wa shindano la Kampeni ya usalama Barabarani kwa shule za Msingi, Christina Christopher Darasa la Saba Shule ya Msingi, Gongolamboto Jeshini akisaidiwa kutembea mara baada ya kutangazwa ndiye aliyechora mchoro mzuri zaidi ya wengine na kutangazwa kuwa mshindi wa shindano hilo na kupata mfano wa hundi ya shilingi milioni mbili kwaajili ya vitabu vya shule anayesoma.
Kamishina Msaidizi wa Polisi(ACP), Fortunatus Musilimu akionyesha mchoro wa Mwanafunzi Christina Christopher wa Darasa la saba shule ya Msingi Gongolamboto Jeshini (aliyeshika kikombe) mara baada ya kuibuka mshindi katika shindano lililoandaliwa na kampuni ya mafuta ya Puma Energy Tanzania lililofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Energy Tanzania, Philippe Corsalrtti akimkabidhi mwalimu wa shule ya Msingi ya ongolamboto Jeshini, Hashim Kalya akipokea mfano wa hundi ya shilingi milioni mbili mara baada ya wanafunzi wa Darasa la saba wa shule hiyo Christina Christopher Kushoto mbele aliyeshika kombe ambaye ni mshindi wa kwanza wa shindano la Usalama barabarani kwa shule za Msingi.
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Energy Tanzania, Philippe Corsalrtti na Kamishina Msaidizi wa Polisi(ACP), Fortunatus Musilimu wakiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa manispaa ya Ilala na Kinondoni pamoja na wanafunzi walioshinda katika shindano la usaama barabarani kwa shule za msingi za jijini Dar es Salaam.
↧
NASI FT SHAA - NIKILEWA
↧
↧
MKUU WA WILAYA YA KINONDONI APOKEA MSAADA WA MADAWATI KUTOKA LAPF
Mkuu wa wilaya na Mwenyekiti wa kamati ya Huduma, uchumi na elimu Diwani Tungaraza akipokea madawati kutoka kwa mkurugenzi wa mawasiliano wa LAPF.
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mhe. Ally Hapi leo hii amepokea madawati 124 kutoka kwa mfuko wa jamii wa LAPF kama mchango wao kupunguza kero ya madawati kwa shule za manispaa ya Kinondoni. Hafla hiyo ya makabidhiano imefanyika leo mbele ya ofisi ya mkururugenzi wa manispaa ya Kinondoni.
Akiongea wakati akikabidhi madawati hayo mkurugenzi wa Mawasiliano James Mlowe amesema wameteua manispaa hii kuwapa msaada wa madawati kwa kuwa wafanyakazi wa wilaya ya Kinondoni wamekuwa niwafanyakazi wanaoongoza kuleta michango kwa wakati ukilinganisha na halmashauri zingine.
↧
MBUNGE ABDALLAH ULEGA ADHAMIRIA KULIKOMBOA JIMBO LA MKURANGA KIMAENDELEO

Mbunge wa jimbo la Mkuranga Mh. Abdallah Ulega akichangia Bajeti ya Serikai katika Mpango pili wa wa miaka mitano ijayo wakati wa vikao vya bunge la bajeti linaloendelea mjini Dodoma hivi karibuni.

Mbunge wa jimbo la Mkuranga Mh. Abdallah Ulega akiendelea na uchangiaji wa hoja katika Mpango huo wa pili wa Maendeleo wa miaka mitano ijayo.

Mbunge wa jimbo la Mkuranga Mh. Abdallah Ulega akizindua kisima cha maji Mkamba katika jimbo lake la Mkuranga mkoani Pwani.
---
SERIKALI ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt.John Magufuli imedhamiria kuwa Serikali ya mageuzi ya Viwanda ukilinganisha na zilizotangulia.
Rais Dkt.Magufuli hata katika kampeni zake za uchaguzi 2015 wakati akipita kuomba kura alisisitiza dhamira ya Serikali ya kujenga uchumi wa Viwanda.
Wakati Serikali ikisisitiza kujenga uchumi wa Viwanda huku ikipata sapoti kupitia Ilani ya Chama cha Mapinduzi wabunge nao katika kuunga mkono hilo kila mmoja amekuwa na kiu ya Jimbo lake kuwa la mfano katika eneo hilo.
Abdallah Ulega ni Mbunge wa Jimbo la Mkuranga lililopo Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani kwa upande wake tangu achaguliwe na wananchi wake ameonesha dhamira na kiu ya kutaka kuwakomboa wananchi wake Kwa kutaka jimbo hilo kuwa na viwanda.
Anasema kuwa lazima wao kama wawakilishi wa wananchi Kwa maana ya wabunge wanaotokana na Chama cha Mapinduzi CCM wapokee Kwa mikono miwili mageuzi haya kwani wameahidi hivyo lazima watende.
Ulega anasema kuwa Jimbo la Mkuranga ni kubwa na linarutuba ya kutosha hivyo anakaribisha wawekezaji kuingia na kukubali Kuwekeza viwanda vidogovidogo na vikubwa katika kilimo hasa cha mazao mbalimbali Kwa ajili ya maendeleo ya watu wake.
Anasema kuwa kuna jitihada kama Mbunge amekuwa akizifanya za kuhakikisha kwamba jimbo lake ni miongoni mwa majimbo ambayo yanafaidika na mikakati ya Serikali ya kutaka mageuzi ya viwanda.
"Kimsingi jimbo langu la Mkuranga ni kubwa kama nilivyosema na uzuri zaidi lina ardhi nzuri sana na ndiyo maana naombawahisani na wawekezaji wa ndani kujitokeza kuja Kuwekeza na zaidi kijenga viwanda."anasema ulega
Anasema kuwa kutokana na utajili wa Ardhi yenye rutuba wanaweza kujenga viwanda vya kusindika mazao lakini pia kwa sababu eneo lao ni kubwa basi hata viwanda vya kubangua korosho na kujengwa Kwa viwanda hivyo kutasaidia kuleta ajira katika eneo hilo.
Anasisitiza kuwa ndio maana wakati akichangia mpango wa wa maendeleo wa Serikali Kwa miaka mitano ameomba Serikali na wahisani kujitokeza Mkuranga lakini Kwa upande wa Serikali kuiweka Mkuranga kuwa sehemu yenye hitaji la ujenzi wa viwanda.
Anasema amebainisha wazi kiu ya wananchi wa jimbo lake la kutaka maendeleo na ajira hivyo bila kuwepo na viwanda hakuna ajira inayoweza kuwepo na zaidi vijana watazidi kulaumu serikali yao.
"Nimesema wazi kuwa Mkuranga kuna matatizo ya miundombinu mbalimbali ikiwamo barabara.Maji .kilimo na mambo mengine na katika baadhi ya maeneo haya nashukuru baadhi ya marafiki wameitikia mwito wangu na wameweza kusaidia katika kichimba visima ambapo wananchi wangu wameaza kupata Maji safi na salama."anasema Ulega
Anasema kuwa anawashukuru African Foundation Reflection Kwa kuonesha moyo wa kusaidia na juhudi hizo zote zimetokana na jitihada zake za kutaka kuona siku moja Mkuranga inakuwa ya kutolea mfano tofauti na ilivyo sasa.
Aidha katika mpango huo wa maendeleo Kwa miaka mitano Kwa Serikali ameomba kujengewa barabara Kutoka Kisiju hadi Mkuranga Kwa kiwango cha lami kwani barabara hiyo ni muhimu Kwa wananchi wa wilaya hiyo lakini hata wale wanaotoka Mafia.
Pia anasema katika mpango mpango wa pili wa maendeleo wa miaka mitano Kuhusu maendeleo ya miundombinu nchini na hapo aliangalia wilaya ya Mafia kwa sababu pale kuna bandari na watu wake pia ndiyo wazalishaji wakubwa wa korosho na samaki.
Anasema kuwa pia kwenye kata yake ya mbezi kwaniaba ya wananchi wake wa Mkuranga wangeishauri Serikali kuwa eneo la viwanda ili wananchi wake wawe sehemu ya uzalishaji wake.
Aidha Ulega anazungumzia suala la kuondoa kero ya uhaba wa upatikani wa Maji katika jimbo hilo ambapo Serikali ingefanya bidii ya kutoa maji hayo kutoka katika mto rufiji kupitia kibiti hadi kufika Mkuranga na hatimaye Dar es Salaam.
Anasema haiwezekani Kwa miaka nenda rudi tatizo la Maji halipatiwi ufumbuzi wakati Mkuranga inapitiwa kwa karibu na Mto Rufiji ambapo mikakati madhubuti ya kuleta Maji ikifanyika tatizo hilo litabaki kuwa historia katika eneo hilo.
Anasema tatizo la ajira Kwa vijana ni kubwa mno hivyo wanashukuru Serikali Kwa kutambua umuhimu wa kutilia mkazo uazishwaji na ufufuaji wa viwanda kwani eneo hilo ndilo linaweza kuwa.msaada Kwa vijana kuweza kupata ajira.
"Mimi kama Mbunge wao kama nilivyosema awali nitaendelea kupambana na kufanya kila linalowezekana Kwa kuhakikisha Mkuranga inakuwa sehemu ya viwanda na naendelea kitoa rai Kwa wawekezaji kuchangamkia Ardhi yetu Kwa kujenga viwanda vingi ili vijana wangu wapate ajira."anasema
Anaongeza kuwa mkuranga ilisahaulika mno pamoja kwamba ni miongoni mwa wilaya za siku nyingi lakini imekuwa nyuma kimaendeleo hivyo niwakati mwafaka wa kushirikiana Kwa pamoja Kwa ajili ya maendeleo.
Anasema kuwa wananchi wake waendelee kumuombea Kwa Mungu na wazidi kudumisha Umoja na mshikamano ili Kwa pamoja wapambane Kwa lengo la kuona jimbo la mkuranga linakuwa la mfano.
Akizungumzia kilimo cha korosho anasema kuwa pamoja na zao hilo kuwa ndio zao linalotegemewa kuendesha maisha ya wananchi wake lakini bado kwasababu ya ukosefu wa kuwepo Kwa viwanda hususani vya ubanguaji kunafanya pasiwepo na tija sana wanayoipata wananchi wake katika kilimo hicho.
Anasema kuwa kutokana na hali hiyo ana kazi kubwa ya kuendelea kuzungumza na watu mbalimbali ili kuleta ushawishi wa kukubali Kuwekeza kwenye ujenzi wa viwanda hivyo.
Pia akizungumzia Elimu anasema anatambua changamoto zilizopo katika eneo hilo hivyo amedhamiria Kwa dhati Kwa kushirikiana na Halmashauri wanaongeza hamasa Kwa wanafunzi ili waweze kufanya vema katika masomo yao na hatimaye kuweza kupata wataalamu wa baadae.
"Najua kuna Changamoto ya madawati na hili tunalishugulikia Kwa kushirikiana na kamati mbalimbali za Shule,wazazi,pamoja na walimu ili kuona namna ya kukabiliana na tatizo hilo na hata uchakavu wa majengo ."anasema Ulega.

Anahitimisha Kwa kuwataka wananchi wa Mkuranga kila mmoja kujielekeza katika kuzalisha Mali huku wakienda na Kauli mbiu ya Rais Dkt.Magufuli ya Hapa Kazi Tu.
↧
AIRTEL YATOA FURSA ZA AJIRA KWA WANAFUNZI KATIKA VYUO VIKUU MBALIMBALI NCHINI
Meneja Rasilimali watu wa Airtel, Bi, Gabriella Kaisi (kulia) akiwapongeza James Kwayu (katikati) na Abubakar Nassor ambao ni wanafunzi wa vyuo waliofaidika na aiira katika kampuni ya Airtel kupitia ushirikiano kati ya Airtel na chama cha wanafunzi vyuoni Tanzania AIESEC wenye lengo la kuwawezesha vijana walioko vyuoni kupata ajira katika makampuni mbalimbali kila mwaka.

Meneja Rasilimali watu wa Airtel , Bi, Gabriella Kaisi akimkabithi cheti cha pongezi Abubakar Nassor baada ya kufaulu mitihani na kuajiriwa na Airtel katika kitengo cha huduma kwa wateja kupitia ushirikiano kati ya Airtel na AIESEC Tanzania (chama cha wanafunzi vyuoni) wenye lengo la kuwawezesha vijana waliokoa vyuoni kupata ajira katika makampuni mbalimbali kila mwaka.
Meneja Rasilimali watu wa Airtel , Gabriella Kaisi akimkabithi cheti cha pongezi James Kwayu baada ya kufaulu mitihani na kuajiriwa na Airtel katika kitengo cha huduma kwa wateja kupitia ushirikiano kati ya Airtel na AIESEC Tanzania (chama cha wanafunzi vyuoni) wenye lengo la kuwawezesha vijana waliokoa vyuoni kupata ajira katika katika makampuni mbalimbali kila mwaka
Meneja Rasilimali watu wa Airtel , Gabriella Kaisi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na James Kwayu na Abubakar Nassor ambao ni wanafunzi wa vyuo waliofaidika na ajira kupitia ushirikiano kati ya Airtel na AIESEC Tanzania (chama cha wanafunzi vyuoni) wenye lengo la kuwawezesha vijana waliokoa vyuoni kupata ajira katika makampuni mbalimbali kila mwaka.
---
*Airtel yatoa ajira kwa wanafunzi wenye vipaji katika vyuo vikuu
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imedhamini kongamano la ajira kwa vijana wa chuo kikuu linaloandaliwa na AIESEC Tanzania lenye lengo la kuwaweka pamoja waajiri (makapuni) na waajiriwa watarajiwa (wanafunzi) kwa lengo la kuwapatia Fursa zitakazowasaidia katika kuendesha shughuli za kiuchumi.
Kila Mwaka AIESEC huandaa kongamano la ajira kwa vijana linaloshirikisha wanafunzi zaidi ya 1500 kutoka katika vyuo vikuu mbalimbali nchini. Kuanzia mwaka jana Airtel imejikita na kushiriki katika kongamano hilo ikiwa ni sehemu ya kuendeleza dhamira yake ya kuwawezesha vijana wanaohitimu vyuoni kupata ajira.
Akiongea kuhusu mpango huo, Meneja Rasilimali watu wa Airtel , Gabriella Kaisi alisema”Tunayofuraha kuwa sehemu ya mpango huu kwa kushirikiana AIESEC Tanzania lengo likiwa ni kuwafikia na kuwaajiri vijana wenye vipaji kutoka katika vyuo vikuu mbalimbali nchini. Tunaamini kila kijana ana nafasi ya kufikia ndoto zake na ndio mana tunatoa fursa kwa vijana kufanya kazi pamoja nasi.
Mwaka jana tuliwawezesha vijana watatu wahitimu kutoka vyuo vikuu vya IFM pamoja na chuo kikuu cha Dar es salaam kupata ajira katika ofisi zetu za Airtel. Vijana hao ni pamoja na Abubakar Nassor ambaye anafanya kazi katika kitengo cha masoko James Kwayu yuko katika kitengo cha Huduma kwa wateja na Gerald Msafiri anafanya kazi katika kitengo cha mauzo.
Vijana hawa watapata nafasi ya kwenda kufanya kazi nje ya nchi katika makao makuu ya Airtel nchini Kenya na India kwa muda wa mienzi miwili kuanzia mwezi wa Mei hadi Julai 2016. Watakaporudi watapangia kufanya katika vitengo tofauti ili kupata uzoefu na mwanga zaidi aliongeza Kaisi
Akiongea kuhusu program hiyo, moja kati ya waliofaidika na mpango katika kitengo cha masoko, Abubakar Nassor alisema” najisikia furaha kuwa mwanachama wa AIESEC Tanzania kwani kumeniwezesha kupata fursa hii adimu ya ajira, uzoefu katika kazi na nafasi ya kujifunza katika kampuni kubwa ya simu duniani. Nimejipanga vyema kujifunza zaidi katika miezi 2 nitakayokuwa nchini India na Nairobi, nahaidi kuitumia fursa hii vyema ili kuweza kuzifikia ndoto zangu
Mwaka huu Airtel imejipanga kuendelea kuwafikia vijana wengi zaidi kwa kutoa ajira kwa vijana wengine watano ambao watafanya vizuri na kufaulu mitihani mbalimbali inayoendelea kwa sasa. Airtel itatangaza majina ya wanafunzi wengine watakaofudhu na kuchaguliwa kwa mwaka huu mara baada ya hatua za uajiri zitakapokamilika.