Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all 11654 articles
Browse latest View live

TANAPA YAZINDUA KAMPENI KILIMANJARO YENYE KAULIMBIU “ WEKA MLIMA SAFI, TUNZA MAZINGIRA YAKUTUNZE”

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Saidi Mecky Sadiki akiongea wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya usafi Mlima Kilimanjaro iliyokuwa na kaulimbiu “ Weka Mlima Safi, Tunza Mazingira Yakutunze” katika lango la Marangu mwishoni mwa wiki. Wengine pichani ni Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi (kati) na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Kilimanjaro Betrita Loibooki.
Wakurugenzi kutoka TANAPA wakifuatilia uzinduzi wa Kampeni ya usafi Mlima Kilimanjaro. Kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Uhifadhi Mtango Mtahiko, Mkurugenzi Utumishi na Utawala Bi. Witness Shoo, Mkurugenzi wa Mipango Dk. Ezekiel Dembe, Mkurugenzi wa Fedha Nassoro Mndeme na nyuma yake Mkurugenzi wa Utalii na Masoko Ibrahim Mussa.
Wanafunzi kutoka Chuo cha Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi Mwanza nao walishiriki katika kampeni ya usafi Mlima Kilimanjaro.
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Kilimanjaro Betrita Loibooki akiongea wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Usafi Mlima Kilimanjaro.
Baadhi ya wadau walioshiriki kampeni ya usafi Mlima Kilimanjaro.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Saidi Mecky Sadiki akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa TANAPA pamoja na wadau kutoka Kampuni mbalimbali za mawakala wa utalii kutoka Kilimanjaro na Arusha wanaoshiriki Kampeni maalum ya usafi Mlima Kilimanjaro.
Idadi kubwa ya wadau wa sekta ya utalii walishirikiana vema na TANAPA kusafisha Mlima Kilimanjaro.
Wageni waalikwa wakivaa ‘gloves’ kabla ya kuanza zoezi la usafi.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Saidi Mecky Sadiki akiokota uchafu wa taka ngumu wakati wa kampeni ya usafi Mlima Kilimanjaro.
Meneja Mawasiliano wa TANAPA Pascal Shelutete akiokota uchafu wa taka ngumu wakati wa kampeni ya usafi Mlima Kilimanjaro.
Mazingira safi yataendelea kuufanya Mlima Kilimanjaro kutiririsha maji kwa wingi zaidi.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

AFISA UCHAGUZI HALMASHAURI YA SERENGETI AHUKUMIWA MIAKA SABA JELA

$
0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA.
AFISA uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Mkoani Mara Bw.  Julius Bujabhi Makwasa amehukumiwa kifungo cha Miaka 7 jela baada ya kupatikana na hatia ya Makosa 34 yakiwepo ya Rushwa.

Mnamo mwaka 2013 Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoani Mara ilimfikisha katika Mahakama ya Wilaya ya Serengeti Afisa uchaguzi wa Halmashauri hiyo Bwana Julius Bujabhi Makwasa na wenzake wawili wakishitakiwa kwa makosa thelathini na manne yakiwemo ya matumizi mabaya ya fedha za umma, kuisababishia hasara Halmashauri ya Serengeti, kusaidia kutenda kosa, kughushi na kutumia nyaraka kumdanganya mwajiri wao.

Washitakiwa wengine katika shauri hilo la uhujumu Uchumi E.C.C 130/2013 lililokuwa likisikilizwa na Hakimu wa Mahakama hiyo Mheshimiwa Ismail Emanuel Ngaile,  walikuwa  Bi Scola Daudi Mosi ambaye ni mtunza kumbukumbu wa Halmashauri hiyo na Bwana Dickson Julius Makwasa ambaye ni mtoto wa mshitakiwa wa kwanza.

Ilidaiwa na mwendesha mashitaka wa TAKUKURU Wakili Martin Makani mbele ya mheshimiwa Ngaile kwamba mshitakiwa wa kwanza Julius Makwasa  ambaye majukumu yake yalikuwa pamoja na kuviteketeza vifaa vya uchaguzi muda wa uchaguzi unapopita na mshitakiwa wa pili Scola Mossy ambaye  majukumu yake ni pamoja kusimamia kumbukumbu zinazoingia na zinazotoka nje ya Halmashauri hiyo,  kwa nafasi zao hizo,  walikuwa na jukumu la kuharibu nyaraka za uchaguzi mkuu wa Octoba 2010 kama ilivyokuwa imeelekezwa na Tume ya Taifa ya uchaguzi. 

Katika kutekeleza jukumu hilo ilielezwa kwamba, waliandaa majina ya vibarua na kuingiza majina hewa ishirini na tano (25) kuonyesha kwamba majina hayo hewa pia yalishiriki  kuchimba mashimo, kusomba nyaraka hizo za uchaguzi na kuzipeleka kwenye mashimo kisha kuziteketeza kwa moto hivyo kustahili malipo. 

Katika udanganyifu huo ilielezwa kwamba, mshitakiwa wa kwanza na wa pili waliweza kuandaa nyaraka za kuipotosha Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti na kuwawezesha kujipatia jumla ya shilingi million tatu laki nane na elfu hamsini (Tsh 3,850,000/=) kwa kutumia nyaraka kumdanganya mwajiri .

Aidha katika mashitaka hayo, mshitakiwa wa tatu Dickson Makwasa ambaye ni mtoto wa mshitakiwa wa kwanza yeye alishitakiwa kwa kosa moja la kusaidia kutenda kosa kwa maelekezo ya baba yake Julius Bujabhi Makwasa, ambapo ilielezwa na upande wa mashitaka kuwa alielekezwa na baba yake kutafuta na alitafuta wanafunzi wenzake na kuwapeleka ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti kwa mtunza fedha na huko walitakiwa kutia sahihi mbele ya majina hewa yaliyokuwa yameorodheshwa  kisha kulipwa fedha zilizoainishwa kwa kila jina kama kwamba ni wao walifanya kazi ya kuteketeza vifaa hivyo vya uchaguzi. 

Hata hivyo baada ya kupokea fedha hizo wanafunzi hao walitakiwa wazikabidhi kwa mshitakiwa wa tatu na wakazikabidhi, ambaye naye alimkabidhi mshitakiwa wa kwanza ambaye ni baba yake. 

Baada ya mahakama kupitia ushahidi uliowasilishwa na upande wa mashitaka na ule wa utetezi iliridhika kwamba mshitakiwa wa kwanza alitenda makosa yote (33) aliyoshitakiwa nayo na hivyo kuhukumiwa kifungo, kulipa faini ya shillingi millioni tano (Tsh.5,000,000/=) au kifungo jela miaka saba na kurejesha fedha jumla ya shilingi million tatu, laki nane na hamsini elfu ( 3,850,000/=) hasara aliyoisababishia Serikali, alishindwa kulipa fedha hizo na kupelekwa jela kuanza kutumikia kifungo. 

Mshitakiwa wa pili alionekana hana hatia hivyo mahakama ilimuachia huru, kwa upande wa mshitakiwa wa tatu ambaye kosa lake lilikuwa kusaidia kutenda kosa kwa maelekezo ya baba yake alipatikana na hatia ya kosa hilo na alihukumiwa kulipa faini ya shilingi million moja (TSH.1000,000/=) au kwenda jela miaka mitatu, aliweza kulipa fedha hizo na akaepuka kifungo.

TAKUKURU Mkoa wa Mara inatoa mwito kwa wazazi hasa walio kwenye utumishi wa umma kuacha tabia ya kuwashirikisha watoto katika kufanikisha vitendo vya uvunjaji wa sheria, kwa kuwa kuendelea kufanya hivyo kutapelekea kujenga jamii ya kihalifu kutokana na vijana kuiga tabia za kihalifu zinazoonyeshwa kwao na wazazi.
  
IMETOLEWA NA
HOLLE J. MAKUNGU MKUU WA TAKUKURU(M)MARA
25 APRILL 2016.

CHEKA UNENEPE; HIVI NDOA ZETU ZIMEFIKIA HUKU?

$
0
0
Maongezi kati ya mwanamume? mmoja hivi na Inspekta wa polisi:

MWANAUME: Mke wangu amepotea, alienda shopping siku ya pili hii hajarudi na simu yake haipatikani.

INSPEKTA: Mkeo ana urefu gani?

MWANAUME: Sijawahi kumcheki

INSPEKTA: Mwembamba au mnene?

MWANAUME: Sio mwembamba anaweza kuwa ni mnene.

INSPEKTA: Rangi ya macho yake je?

MWANAUME: Sijawahi kumuangalia.

INSPEKTA: Rangi ya nywele zake je?

MWANAUME: Hubadilisha mara kwa mara.

INSPEKTA: Alikiwa amevaa nini mara ya mwisho kuonana nae.

MWANAUME: Sijui sina ukakika, sijui alivaa gauni au suti!?

INSPEKTA: Alikuwa akiendesha gari?

MWANAUME: Ndio!

INSPEKTA: Rangi ya gari je?

MWANAUME: Toyota Rav4 nyeusi A8, ikiwa na lita 21 za mafuta, injini yenye uwezo wa 333 horsepower, imetengenezwa mwaka 2008. Pia injini yake ni ukubwa wa 1289 CC, ina spidi 8 za tiptronic automatic transmission na muundo wa analojia.

Chasisi yake iko Low, uwezo wa For wheel drive, ina GPS with hardly music system Inside.

Pia taa za mbele ni muundo wa LED ambapo zinauwezo wa kufyonza mwanga ulio mbele yake na ina mkwaruzo kidogo kwenye mlango wa dereva na....na. Niliinunua kwa gharama sana na....(akaanza kulia)

INSPEKTA: Usilie kiongozi, tutalipata gari lako.

Unafikiri huyu alikuwa akitafuta nini mke wake au gari lake?

BENKI YA CRDB YATANGAZA AJIRA KWA KIDATO CHA SITA JITEGEMEE JKT SHULE YA SEKONDARIBENKI

$
0
0
 Meneja wa Huduma Mbadala wa Benki ya CRDB,  Joseph Wite (katikati), akimkabidhi Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari ya Jitegemee JKT, Brigedia Jenerali mstaafu Lawrence Magere (kushoto), hundi yenye thamani ya sh.milioni 2.5 kwa ajili ya kusaidia kujenga mifumo ya maji shuleni hapo katika Mahafali ya 22 ya kidato cha sita yaliyofanyika Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkuu wa Shule hiyo, Luteni Kanali Robert Kessy.
 Wazazi na walezi wa wanafunzi hao wakiwa kwenye mahafali hayo.
Viongozi mbalimbali wakiwa na mgeni rasmi wakielekea ukumbini.
Maandamano ya wanafunzi hao yakielekea ukumbini.
Wimbo wa Taifa ukiimbwa.
Bendi  ya JKT ikitumbuiza.
Wimbo maalumu wa shule ukiimbwa.
Wanafunzi wa kidato cha sita wakiwa kwenye mahafali hayo.
Burudani zikiwa zimepamba moto.
Mkuu wa Shule, Luteni Kanali, Robert Kessy akizungumza kwenye mahafali hayo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari ya Jitegemee JKT, Brigedia Jenerali mstaafu Lawrence Magere akizungumza kwenye mahafali hayo.
 Meneja wa Huduma Mbadala wa Benki ya CRDB,  Joseph Wite (katikati), akizungumza katika mahafali hayo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Shule, Brigedia Jenerali mstaafu Lawrence Magere (kushoto), akimkabidhi hundi iliyotolewa na CRDB, Mkuu wa shule hiyo, Luteni Kanali Robert Kessy.
Mkuu wa Shule akimkabishi cheki hiyo, Meja Rehema  Wanjara Msarifu wa Shule. Wengine kutoka kulia ni Makamu Mkuu wa Shule hiyo na Utawala, Kapteni Benitho na Mjumbe wa Bodi ya Shule, Sebastian Inosh.
Kwaito likiwa limepamba moto.

Hapa mwanafunzi Khalifa Chege aliyekuwa namba moja katika masomo akikabidhiwa zawadi.
Mwanafunzi Ibrahim Pazi aliyeshika nafasi ya pili katika masomo akikabidhiwa zawadi.




Dotto Mwaibale

BENKI ya CRDB imetangaza ajira kwa wanafunzi wa kidato cha sita katika Shule ya Sekondari ya Jitegemee JKT watakao pata divisheni one ya pointi tatu baada ya kufanya mtihani wa taifa.

Ofa hiyo ilitolewa na Meneja wa huduma mbadala wa Benki ya CRDB Joseph Wite kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa benki hiyo Dk. Charles Kimei katika mahafali ya 22 yaliyofanyika shuleni hapo Dar es Salaam jana.

Katika hatua nyingine Wite amewataka wanafunzi hao kutumia fursa ya ajira katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kwani uwezekano upo endapo watafanya bidii katika masomo yao.

Alisema ni wakati wa vijana kuchangamkia fursa za ajira katika jumuiya ya Afrika Mashariki ili kuweza kufikia malengo na kuondokana na dhana ya kwamba hakuna ajira nchini.

"Pamoja na kwamba vijana wengi wanahofia kuajiriwa nje ya nchini kutokana na mambo mbalimbali ikiwemo kuogopa kwamba hawawezi kukidhi vigezo lakini mimi napenda kuwatoa hofu hiyo kwamba hata kama kiingereza huwezi kiswahili utashindwa kufundisha,"alisema Wite.

Aliwataka wanafunzi hao kuhakikisha kwamba wanajiepusha na matendo mabaya  ambayo yatapelekea kujiunga na madawa ya kulevya na kuhatarisha maisha yao.

Alisema mtu anapojiunga na madawa ya kulevya ana uwezekano mkubwa wa kupata magonjwa ya kuambukiza ikiwemo ukimwi.

"Janga la ukimwi halichagui mwenye nacho au asiye nacho ukicheza unahatarisha maisha hivyo ni vyena mjihadhari nalo ili muweze kufikia malengo,"alisema.

Hata hivyo aliendelea kusema kuwa benki hiyo inachangia  kwa kutambua asilimia moja ya faida wanayoipata kwa mwaka kwa sekta zinazopewa ikiwemo elimu na afya.

Pia alisema benki hiyo itaisaidia shule hiyo milioni 2.5 kwa ajili ya kuboresha mfumo wa maji safi.
 Mkuu wa Shule hiyo Luteni Kanali Robert Kessy alisema wanafunzi wanaohitimu katika mahafali hayo ya 22 ni 558.

Alisema wamewalea wanafunzi hao  katika maadili mazuri pamoja na kuwafundisha nyezo zote hivyo wanatarajia kwamba watafanya vizuri na kuwa mabalozi wazuri katika jamii.

Mmoja ya wazazi waliohudhuria mahafali hayo Hamisa Athumani aliipongeza shule hiyo kwa kufundisha masomo ya ukakamavu kwani yamewajengea uwezo wa kujiamini na kuwa na nidhamu.

PAULINA MGENI: NAHITAJI MENEJA WA KUSIMAMIA KAZI ZANGU ZA UREMBO

$
0
0
paulina
Paulina Mgeni ndio Miss Utalii Mkoa wa Iringa mwaka 2013 mpaka sasa kabla mashindano hayo hayaja simamishwa; ila kwasasa anafanya kazi za mitindo akiwa kama Mwanamitindo (Model), lakini anahitaji meneja wa kusimamia kazi zake hizo za Urembo (Modeling).
Paulina Mgeni ni Mwanamitindo (Model) anaefanya kazi za urembo na maonesho ya mitindo kwa kujitegemea yeye mwenyewe hayupo chini ya kampuni yoyote wala chini ya lebo ya mtu yeyete, japokua amekuwa akifanya shoo nyingi kwa kushirikiana na baadhi ya makampuni na wabuni mbalili, kwasasa anatafuta Meneja wa kuwa anamsimamia kazi zake.
Mwaka 2013 Paulina alikuwa Miss Utalii mkoa wa Iringa, akafanikiwa kuingia ngazi ya Taifa na kupata tuzo ya the Best Model of Tanzania, pamoja na kuwa Balozi wa models Tanzania; amefanikiwakufanya maonesho (shows) mbali mbali hapa Tanzania na nje ya Tanzania.
p2
Mwanamitindo Paulina Mgeni akiwa katika pozi.

Paulina amefanya kazi na wabunifu mbali mbali (designers) kama vile Asia Idalus, Kurwa Mkwandule, Adam Zanzibar house, Wolta Di Maria n.k.

Maonesho (shows) makubwa ambayo amefanya ni Zanzibar fashion house mwaka 2014 na yale East Africa Fashion Week jijini Nairobi –Kenya akiwa na makeke internasional, maonesho hayo yalifanyika mwezi 3 tarehe 29 mwaka 2016.

Hivyo kwa yeyote atakaehitaji kuwa meneja wa mrembo huyu kwa ajili ya kusimamia kazi zake unaweza kuwasiliana nae kwa namba +255 716 66 66 96 au kwa barua pepe mgenipaulina3@gmail.com
p3
Paulina Leonard akiwa katika maonesho Zanzibar, Fashion House.
Paulina Mgeni (wa kwanza kulia) akiwa katika maonesho ya East AfricaFashion Week jijini Nairobi mwezi 3 mwaka 2016

Paulina akiwa katika show ya Lady in RED jijini Dar es Salaam.

Mwanamitindo Paulina Mgeni katika photo shoot.

RAIS DKT. MAGUFULI AWACHAGUA KAMISHNA MKUU WA JESHI LA ZIMAMOTO NA MTENDAJI MKUU WA HOSPITALI YA MKAPA - DODOMA

$
0
0

PROF. MBARAWA ATOA WIKI MBILI BARABARA YA MORROCO - MWENGE

$
0
0
Mafundi wa kampuni ya Estim Construction wakiendelea na Ujenzi wa barabara ya Mwenge –Morocco KM 4.3 ambayo ni sehemu ya Barabara ya Morocco –Mwenge-Tegeta.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS akimuonyesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kazi ya ujenzi wa mifereji pembezoni mwa Barabara ya Morocco-Mwenge inavyoendelea.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS Eng.Patric Mfugale kuhusu kukamilika kwa upanuzi wa barabara ya Morocco-Mwenge KM 4.3.
--
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa ametoa wiki mbili kwa mkandarasi ESTIM Construction anayejenga barabara ya Bagamoyo, Sehemu ya Morroco-Mwenge kilomita 4.3 kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo.

Akizungumza mara baada ya kukagua barabara hiyo, Prof. Mbarawa amesema baada ya wiki mbili barabara hiyo itafunguliwa kwa ajili ya matumizi ili kupunguza msongamano wa magari yanayoingia na kutoka katikati ya jijini.

“Hakikisheni barabara hii inakamilika ndani ya wiki mbili, ili msongamano wa magari yanatoingia na kutoka katika ya jiji upungue, na hivyo kuiunganisha vizuri barabara hii na ile ya Mwenge-Tegeta”. Amesema Waziri Prof. Mbarawa.

Aidha amewataka waananchi na madereva wanaotumia barabara hiyo kulinda mazingira kwa kuepuka vitendo vya kumwaga mafuta kwenye barabara hiyo na kutupa takataka zinazosababisha mifereji iliyo pembezoni mwa barabara kuzipa na kuharibu barabara hiyo.

“Nawataka watumiaji wa barabara, kuzingatia matumizi sahihi ya barabara, tunawekeza fedha nyingi katika ujenzi wa barabara mijini ili kuondoa msongamano hivyo zingatieni matumizi sahihi ya barabara ili zidumu kwa muda mrefu”. Amesema Prof. Mbarawa.

Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) Eng. Patrick Mfugale amemhakikishia Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kuwa ili kupunguza msongamano ujenzi wa barabara hiyo umelazimika kuweka sehemu maalum za watembea kwa miguu kutokana na wingi wa watumiaji wa barabara hiyo katika sehemu hiyo na kupanua maingilio ya barabara ili kurahisisha magari kutoka na kuingia katika barabara hiyo.

Eng. Mfugale amesema zaidi ya magari 15,000 yanakadiriwa kuwa yatapita katika barabara itakapokamilikana hivyo kupunguza msongamano mkubwa uliokuwepo katika eneo hilo.

Takribani shilingi bilioni 4 zinatarajiwa kutumika katika ujenzi huo na hivyo kuiunganisha barabara ya Mwenge-Morroco na ile ya Mwenge-Tegeta.

WAZEE WASIOJIWEZA KITUO CHA BUKUMBI MWANZA WAIOMBA SERIKALI KUIMALISHA HUDUMA ZA AFYA KITUONI KWAO

$
0
0
Wauguzi wa zahanati ya kituo cha ustawi wa Jamii cha Bukumbi kijiji cha Kigongo kata ya Idetemya wilayani Misungwi mkoani Mwanza wakiwaongoza waandishi wa habari wa jiji la Mwanza na Dar es Salaam waliofika kuwatembelea wazee wanaoishi katika kituo hicho kujua jinsi wanavyoishi na kuwa kutambua suala la uzazi wa mpango. Ziara hiyo ya waandishi wa habari iliyofanyika wiki iliyopita iliratibiwa na taasisi inayojishuhulisha na ongezeko la idadi ya watu na uzazi wa mpango (TCDAA) wakishirikiana na Marie Stopes Tanzania. Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
Wazee wa kituo cha ustawi wa Jamii cha Bukumbi kijiji cha Kigongo kata ya Idetemya wilayani Misungwi mkoani Mwanza wakiendelea na kazi za mikono.
Mmiliki wa Blog ya Kajunason akimsaidia kusuka kikapu mmoja ya wazee anayelelewa katika kituo hicho.
Moja ya nyumba wanayoishi wazee hao.
Waandishi wa habari wa jiji la Mwanza na Dar es Salaam waliotembelea Wazee wa kituo cha ustawi wa Jamii cha Bukumbi wakifanya mahojiano ili kujua changamoto mbali mbali zinazowakabili ambapo wazee hao walisema jambo kubwa linalowaumiza kicha ni upatikanaji wa matibabu katika zahanati yao jambo linalowafanya wengine kuishi na maradhi kwa muda mrefu.
Waaandishi wakiendelea kufanya mahojiano na Wazee wa kituo cha ustawi wa Jamii cha Bukumbi.
Ofisa Mfawizi wa Makao ya wazee wasiojiweza, Michael Bundala akifanya mahojiano na waandishi wa habari ambapo katika mahojiano hayo alielezea kuwa kuna changamoto nyingi za kuishi na wazee hawa kama kiongozi kwa vile wazee wamekuwa wakorofi mno na kuona siwatendei haki katika maamuzi ambayo nimekuwa nikiyatoa ikiwemo katika ugawaji wa vyakula. 
---
Na Cathbert Kajuna - Mwanza.

Wazee wanaoishi katika kituo cha ustawi wa Jamii cha Bukumbi kijiji cha Kigongo kata ya Idetemya wilayani Misungwi mkoani Mwanza wanaiomba Serikali kuwapatia huduma za afya katika Zahanati ya kituo chao.
 
Wazee hao wanaeleza kwamba changamoto hizo katika ziara ya waandishi wa habari wa jiji la Mwanza na Dar es Salaam waliounganishwa pamoja na kuratibiwa na taasisi inayojishuhulisha na ongezeko la idadi ya watu na uzazi wa mpango (TCDAA) na Marie Stopes Tanzania.
 
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wazee hao wanasema katika zahanati hiyo hakuna dawa na wanapoumwa wanalazimika kununua dawa.
 
Mwenyekiti wa kambi hiyo, Helen Emmanuel anasema wanakabiliwa na changamoto mbalimbali za huduma ya afya pamoja na wenzao wasiojiweza kufukuzwa kambini.
 
"Tunapofika katika zahanati hii daktari anatupima vizuri lakini hakuna dawa hivyo anatuandikia kwenye karatasi anatuambia tukanunue.
 
"Kwakweli hii ni changamoto kubwa sana kwetu kwasababu wakati mwingine tunapoandikiwa dawa hela ya kununulia tunakosa hali inayosababisha tunaendelea kuumia kutokana na kwamba afya zetu ndio hizi na hatuna sehemu ya kujipatia kipato" alisema Heleni.
 
Pia alisema kwa sasa wapo wazee 78 katika kambi hiyo lakini wapo walemavu wenzao saba ambao wameambiwa wahame kambini waende vijijini wakati hawana uwezo.
 
"Kwakweli inaumiza sana kwasababu hawana uwezo wa kujitafutia pia mimi sina uwezo wa kuwasaidia kwasababu mimi mwenyewe ni mlemavu ,"alisema.
 
Ofisa Mfawizi wa Makao ya wazee wasiojiweza,Michael Bundala alisema hapa kambini tuna watoto 17 ambao wazazi wao wako humu kambini na wengine waliotimiza miaka 18 tuliwapunguza na kuwatengea eneo kwa ajili ya makazi na tusingefanya hivyo tungekuwa zaidi ya 800 kwasababu wengine wanapeana mimba wenyewe kwa wenyewe.
 
Naye Mwenyekiti wa kijiji cha Kigongo Kata ya Idetemya, Sebastian Kisumu alisema ipo changamoto ya vijana wa nje kuwapa mimba wasichana wa kambi hiyo.
 
Alisema wapo wataalamu mbalimbali mambo wanafika katika kambi hiyo kutoa elimu ya uzazi wa mpango lakini wengi wao hawaipokei hali inayosababisha kuwa na idadi kubwa ya watoto ambao hawana baba.

MKURUGENZI MKUU WA MAMLAKA YA ELIMU TANZANIA AZUNGUMZA NA WANAFUNZI SHULE YA SEKONDARI YA WASICHANA WERUWERU

$
0
0


Wahitimu wa kidato cha sita katika shule ya sekondari ya Wasichana ya Weruweru wakiimba wakati wakielekea ukumbini kwa ajili ya kuanza rasmi kwa sherehe ya kuwaaga.
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Weruweru Rosemery Tarimo akimuongoza mgeni rasmi katika mahafali ya 31 ya kidato cha sita ,Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania ,Joel Raulant (kulia) wakati wakielekea ukumbini kwa ajili ya sherehe za mahafali hayo.
Mgeni rasmi katika mahafali ya 31 katika shule ya sekondari ya Wasichana ya Weruweru ,Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania,Joel Raulant akiingia ukumbini pamoja na Mkuu wa shule hiyo Rosemery Tarimo.
Mgeni rasmi ,Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania,Joel Raulant na wageni wengine wakiwa wamesimama wakifuatilia wimbo wa shule hiyo wakati ukiimbwa na wanafunzi katika mahafali hayo.
Wanafunzi wanaohitimu kidato cha sita katika shule ya sekondari ya Wasichana ya Weruweru wakiimba wimbo wa shule.
Walimu na watumishi wengine wa shule hiyo wakifuatilia sherehe ya mahafali hayo.
Mkuu wa shule ya Sekondari ya Wasichana ya Weruweru,Rosemery Tarimo akitoa taarifa ya shule hiyo kwa mgeni rasmi wakati wa mahafali hayo ya 31 ambapo jumla ya wanafunzi 390 wamehitimu.
Wahitimu wakifuatilia taarifa ya shule hiyo iliyokuwa ikitolewa na Mkuu wa shule hiyo ,Rosemery Tarimo.
Wanafunzi wanaohitimu kidato cha sita katika shule hiyo wakisoma risala mbele ya mgeni rasmi.
Mzazi mualikwa ,Jaji Amir Mruma akizungumza kwa niaba ya wazazi wenye watoto wanaosoma katika shule hiyo.
Mgeni rasmi katika mahafali ya 31 ya kidato cha sita katika shule ya sekondari ya Wasichana ya Weruweru ,Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania ,Joel Raulent akitoa hotuba yake wakati wa mahafali hayo.
Mgeni rasmi katika mahafali hayo,Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania,Joel Raulent akitunuku vyeti kwa wahitimu 390 wa kidato cha sita katika shule hiyo.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

MKURUGENZI WA TCRA NA BODI YAKE WAPIGWA MWELEKA

$
0
0

RAIS MAGUFULI AFANYA KIKAO NA WATENDAJI WA WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO, FEDHA NA MIPANGO, TRA, BENKI KUU, TAKUKURU NA TCRA

$
0
0
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongoza kikao cha kazi na watendaji wa serikali wakiwemo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John Kijazi, pamoja na ma-Katibu wakuu Wizara ya Mawasiliano Profesa Faustine Kamuzora, Katibu Mkuu Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile, Naibu Katibu Mkuu Fedha na Mipango Mhe Dottoa James, Gavana wa Benki Kuu Profesa Benno Ndulu, Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Alphayo Kidata, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Kamishna Valentino Mlowola pamoja na uongozzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na watendaji wengine. PICHA NA IKULU

MJANE WA BABA WA TAIFA, MAMA MARIA ATEMBELEA DARAJA LA NYERERE KIGAMBONI

$
0
0
Mama Maria Nyerere, Mjane wa Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, akiwa na mwanae Mhe. Makongoro Nyerere na msaidizi wake akifurahia mandhari wakati walipotembelea Daraja la Nyerere Kigamboni jijini Dar es salaam.

Mama Maria, ambae hakujali mvua kubwa iliyokuwa inanyesha, alionekana mwenye furaha kufika darajani hapo kwani ndoto ya miaka  mingi iliyoanzishwa na hayati mumewe imetimia. Pia alimshukuru sana Dkt John Pombe Joseph Magufuli kwa kuagiza daraja lipewe jina la Mwalimu na siyo yeye, jambo ambalo amesema limemfariji sana kwani vizazi vya sasa na vijavyo vitamkumbuka mwasisi wa Taifa.
Mama Maria Nyerere na Mwanae, Mh. Makongoro Nyerere wakimbelea eneo la Daraja hilo.
---
Mke wa Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Maria Nyerere ametembelea Daraja la Nyerere linalounganisha eneo la Kigambaoni na Kurasini Jijini Dar es salaam na kuipongeza serikali na wananchi wote wa Tanzania kwa kufanikisha ujenzi wa Daraja hilo kubwa na la kisasa kwa nchi za Afrika ya Mashariki na Kati.

Mama Maria Nyerere aliyeongozana na Mwanae Mheshimiwa Makongolo Nyerere amesema kukamilika kwa daraja hilo ambalo ujenzi wake umegharimu shilingi Bilioni 254.12 kumekamilisha mpango wa miaka mingi ulioanzishwa na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyekuwa na nia ya kujenga daraja katika eneo hilo la mkondo wa bahari lakini kwa sababu ya ufinyu wa bajeti haikuwezekana.

Aidha, Mama Maria Nyerere amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuamua Daraja hilo liitwe Daraja la Nyerere kwa heshimu ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, na amebainisha kuwa uamuzi huo utaviwezesha vizazi vijavyo kutambua juhudi zilizofanywa na mmewe katika ujenzi wa nchi.

"Mimi ninamshukuru sana Rais kwa maana ilikuwa lipewe jina lake, lakini yeye Mungu akamjaalia akasema kwamba hapana tukumbuke tulikotoka, kwa hiyo najisikia vizuri sana, na familia nayo inajisikia vizuri sana, lakini zaidi na watanzania wanajisikia vizuri sana, kwa maana watakuwa wanaulizana Nyerere alikuwa ni nani?" Amesisitiza Mama Maria Nyerere.

Daraja la Nyerere lenye urefu wa meta 680, upana wa meta 3.2, njia sita za magari na barabara unganishi zenye urefu wa kilometa 2.5, lilifunguliwa na Rais wa awamu ya tano

Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 19 Aprili, 2016 na linakuwa kiunganishi muhimu kati ya Kigamboni na katikati ya Jiji la Dar es salaam.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
27 Aprili, 2016

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AKUTANA NA UONGOZI WA BARAZA LA TAWLA NA UONGOZI WA SKAUT LEO

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na uongozi wa Baraza la Wanachama wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) wakati Uongozi huo ulipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Dar es salaam leo April 27,2016 kwa lengo la kumpongeza na pamoja na kumuelezea malengo na mikakati ya kiutendaji ya Chama hicho.
Makamu wa Rais Mhe. Samia akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Baraza la TAWLA.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Baadhi ya Wawakilishi na Wanachama wa Chama cha SKAUT Nchini wakati ujumbe wa wawakilishi hao ulipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Dar es salaam leo April 27,2016 kwa ajili ya kumuelezea Makamu wa Rais shuhuli zao za kiutendaji hasa katika kutoa mafunzo mbalimbali kwa Mtoto wa kike.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, na Katibu Mkuu Kiongozi Baolozi Peter Kijazi Baada ya kuapishwa Makatibu wa Mikoa leo April 27,2016 Ikulu Dar es salaam. (Picha na OMR).
---
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema kazi kubwa ya Chama Cha Skauti wa Kike nchini hivi sasa ni kuhakikisha kinarejesha heshima ya mwanamke katika jamii.

Samia ametoa kauli hiyo leo alipokuwa akizungumza na baadhi ya wanachama wa chama hicho waliofika ofisi kwake Ikulu kwa ajili ya kuelezea shughuli zao katika kusaidia watoto wa kike waweze kujitambua na hatimaye kulitumikia Taifa.

Alisema pamoja na chama hicho kinafundisha kujenga ujasiri na kuwa huru kwa mtoto wa kike lakini kuna haja ya kukumbushana umuhimu wa kuzingatia mila na desturi nzuri zilizopo katika matendo yao ili kurejesha heshima ya mwanamke.

"Sasa hivi utakuta binti kavaa kipanti kinambana hasa, anazunguka barabarani huku na kule, mwenyewe anajiona yuko sawa...hicho ni kinyume kabisa na maadili yetu, mila na desturi zetu za kiafrika tumeziacha kabisa." alisema Makamu wa Rais.

Aidha alisema katika enzi hizi za utandawazi kumekuwa na urushwaji wa mambo yasiyo na maadili katika mitandao jambo ambalo mtoto wa kike anaweza kuutumia uhuru huo kwa kufanya mambo kinyume na mila na desturi.

Alisema pamoja na kwamba Tanzania inapingwa na mataifa makubwa kwa kupitisha sheria ya makosa ya mtandao lakini bado chama hicho kina kazi kubwa ya kusaidia jitihada za serikali katika kulea watoto wa kike kimaadili. 

"Nyinyi Girl Guide mna hiyo kazi ya kusaidia kuwalea watoto wa kike waliojengeka vizuri kimaadili na wanazingatia mila na desturi," alidokeza Samia

Makamu wa Rais alikitaka chama hicho pia kuandaa miradi kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa vyoo bora mashuleni kulingana na mahitaji ya watoto wa kike na hivyo kuwawezesha kuhudhuria masomo siku zote bila kukosa kama ilivyo kwa wavulana.

Mwenyekiti wa chama hicho, Matilda Balawa alimshukuru Makamu wa Rais kwa kukubali kuwa mwanachama na kupongeza utendaji wa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli.

WAZIRI MKUU, MAJALIWA AKUTANA NA WAZIRI WA WA VIWANDA NA BIASHARA WA SINGAPORE

$
0
0

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Biashara na Viwanda wa  Singapore, Dkt. Koh Poh Koon (kulia kwake) na ujumbe wake, Ofisini kwake bungeni mjini Dodoma Aprili 27, 2016. Kulia ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana  na Waziri wa Biashara na Viwanda wa  Singapore, Dkt. Koh Poh Koon (kulia) na ujumbe wake kabla ya mazungumzo yao , Ofisini kwake bungeni mjini Dodoma Aprili 27, 2016.
 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

PROGRAMU YA FURSA KWA WATOTO YAZINDULIWA DAR, LENGO KUBORESHA ELIMU YA AWALI

$
0
0
_MG_9991
Na Rabi Hume.
Kwa kutambua umuhimu wa elimu kwa watoto ambao ndiyo watakuja kuwa viongozi wa baadae nchini, programu mpya inayofahamika kama Fursa Kwa Watoto imezinduliwa leo ikiwa na malengo ya kuboresha elimu kwa watoto wanaoanza elimu ya awali ili kuwafanya kuwa na uwezo pindi wanapoanza elimu ya shule ya msingi.
Akizungumzia programu hiyo, Mratibu wa Elimu ya Awali kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo, Clarence Mwinuka amesema kuwa kabla ya kuletwa kwa programu hiyo kulikuwa na matatizo ambayo yakikabili elimu ya awali hivyo kuwafanya wanafunzi wanaomaliza elimu hiyo kutokuwa na uwezo wa kutosha kuanza elimu ya msingi.
Amesema kupitia programu hiyo ambayo kwa kuanzia itafanyika Mwanza na Moshi ambapo itafanyika kwa miaka miwili na baada ya hapo watawachunguza watoto hao kama watakuwa wamekuwa na uwezo wa kutosha kwa ajili ya kujiunga na elimu ya msingi.
“Kila mtoto anatakiwa kuanzia elimu ya awali na kupitia programu hii walimu watapewa mafunzo, vifaa vitatolewa na kuwatengenezea mazingira mazuri ya kuwapa motisha alafu baada ya programu kumalizika tutaona matokeo yakoje,” amesema Mwinuka.
DSC_0902
Mratibu wa Elimu ya Awali kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo, Clarence Mwinuka akizungumzia hali ya elimu ya awali ilivyo nchini na mafanikio yanayoweza kupatikana kutokana na programu hiyo. (Picha zote na Rabi Hume wa MoDewjiBlog)
Nae Mtendaji Mkuu wa Dubai Cares ambao dhiyo wadhamini wa programu hiyo, Tariq Al Gurg amesema wameamua kudhamini programu hiyo nchini ili kusaidia kukuza elimu nchini.
Amesema Falme za Kiarabu imekuwa nchi ambayo inashirikiana na Tanzania katika mambo mbalimbali na hivyo wanaamini programu hiyo itakuwa na matokeo mazuri na kuwafanya wanafunzi wanaoingia kuanza elimu ya msingi kuwa na uwezo wa kutosha.
“Tumesaidia programu hii ili kuboresha elimu ya Tanzania ambayo itafanyika mpaka 2018, tuna tumaini itafanikiwa,” amesema Gurg.
DSC_0822
Mtendaji Mkuu wa Dubai Cares, Tariq Al Gurg akizungummzia udhamini wao kwa programu hiyo na matarajio yao. Kushoto ni Meneja Programu wa Dubai Cares, Saeed Alissmaily.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Shirika la Crossfire nchini ambayo inahusika maendeleo ya elimu kwa watoto, Graig Ferla amesema ni jambo zuri kuwekeza katika elimu ya watoto kwa ajili ya matokeo mazuri ya baadae kwa kuanzia darasani hadi katika maisha ya kawaida.
DSC_0862
Mkurugenzi wa Shirika la Crossfire nchini, Graig Ferla akizungumzia jinsi programu hivyo inaweza kufanikiwa nchini na umuhimu wa kuwekeza katika elimu kwa kuanza na elimu ya awali. Kulia ni Meneja Programu wa Dubai Cares, Saeed Alissmaily na Mtendaji Mkuu wa Dubai Cares, Tariq Al Gurg
DSC_0878
Mkuu wa Elimu kutoka Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), Cecilia Baldeh akizungumzia umuhimu wa kuwa na mipango wa kuboresha elimu nchini hasa kutokana na kuwa na waziri ambaye yupo tayari kuona hilo likifanyika. Kushoto ni Mratibu wa Elimu ya Awali kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo, Clarence Mwinuka na Mtendaji Mkuu wa Dubai Cares, Tariq Al Gurg.
_MG_9991
Uzinduzi wa programu ya Fursa Kwa Watoto ukifanyika.
DSC_0899
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka Tanzania na Falme za Kiarabu (UAE) waliohudhuria mkutano wa uzinduzi wa programu hiyo.

MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM, PAUL MAKONDA AFUNGUA MKUTANO WA CHAMA CHA MAAFISA KUMBUKUMBU NA TAARIFA ZA AFYA TANZANIA

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,  Paul Makonda akifungua, Mkutano wa Watunza kumbukumbu Jijini Dar es Salaam leo.
 (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
 Mshauri Mkuu wa Chama cha wataalamu hao na Afisa kumbukumbu na Taarifa za Afya Mwandamizi wa  Hospitali ya Taifa Muhimbili, Geofrey Semu akizungumza na washiriki hao kabla ya kufunguliwa Mkutano huo  na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ambapo mkutano huo unatarajiwa kufungwa kesho na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
 Baadhi ya washiriki
 Baadhi ya washiriki kutoka Mikoa Mbalimbali Tanzania wakisikiliza kwa makini wakati wa Mkuu wa Mkoa Paul Makonda alipokua akizungumza leo Jijini Dar es Salaam
 Baadhi ya washiriki wenyeji katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na wageni kutoka Mikoa mbalimbali Tanzania wakisikiliza kwa umakini
  Baadhi ya washiriki  toka Mikoa Mbalimbali wakimsiliza Mkuu wa Mkoa Paul Mamonda (hayupo pichani) na mwenyeji mwenyeji wao, Elizabeth Mlindoko (wa pili kulia) kutoka  Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu Muhimbili (MOI).

HARRY KITILYA NA WENZAKE WAFUTIWA SHTAKA MOJA, DHAMANA YAGONGA MWAMBA, KESI KUSOMWA TENA APRIL 29, 2016

$
0
0
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mstaafu, Harry Kitilya (kushoto) akiwa na waliokuwa Wafanyakazi wa Benki ya StanBic Tanzania,  Sioi Sumari (katikati) na Shose Sinare, wakiwa Mahakam ya Hakimu Mkazi Kisutu, Jijini Dar es salaam.

Washitakiwa hao wanaokabiriwa na mastaka nane likiwemo la utakatishaji Fedha kiasi cha Dola za Marekani milioni 6, ili kufanikisha mkopo kutoka Benki ya Stanbic kwenda Serikalini, walifikishwa Mahakamani hapo leo kusikiliza keshi yao, na walifanikiwa kufutiwa Shitaka moja la kutakatisha Fedha kati ya nane yaliyokuwa yakiwakabili, ambapo Washitakiwa hao walisomewa kufutwa kwa shitaka hilo kwa madai ya kukosa Vidhibitisho.

Aidha mpaka mtandao huu unatoka Mahakamani hapo Mawakili walikuwa bado wakihangaikia kupata dhamana baada ya kufutiwa shitaka hilo lililokuwa na kikwazo kikubwa cha dhamana.

Baada ya kufutiwa shitaka hilo, DPP aliwasilisha hati ya mapendekezo ya kukata rufaa ya kupinga uamuzi wa kufuta shitaka namba nane la utakatishaji Fedha linalowakabili watuhumiwa hao, ambapo zoezi la dhamana liligonga mwamba na Washitakiwa hao wamerudishwa rumande.

HISTORIA YA MAREHEMU PAPA WEMBA

$
0
0

RAIS DKT. MAGUFULI AWAAPISHA MAKATIBU TAWALA WAPYA WA MIKOA 10 IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Ndugu Jumanne Abdallah Sagini kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Ndugu Selestine Muhochi Gesimba kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Ndugu Amantius Casmiri Msole kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Ndugu Zuberi Mhina Samataba kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Thea Medard Ntara kuwa katibu Tawala wa mkoa wa Tabora, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Ndugu Richard Nkingwa Kwitega kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Eng. Aisha Salim Amour kuwa Katibu Tawala wa mkoa wa Kilimanjaro, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Eng. Zena Ahmed Said kuwa Katibu Tawala wa mkoa wa Tanga, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Ndugu Albert Gabriel Msovela kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Angelina Mageni Lutambi kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida, ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Makatibu Tawala wapya wa Mikoa 10 mara baada ya Kuwaapisha. Kulia kwake ni Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan na Kushoto kwake ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Makatibu Tawala wapya mara baada ya kupiga nao picha ya pamoja Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya Habari Ikulu jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John Kijazi.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John Kijazi mara baada ya kumaliza kuwaapisha Makatibu Tawala wa mikoa 10 Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU.

SERIKALI YATOA UFAFANUZI SERA YA ELIMU BURE

$
0
0
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako, amewataka walimu na maafisa elimu kusimamia vyema majukumu yao na kuhakikisha utoaji elimu bora kwa wanafunzi ili kupata wataalamu watakaolisaidia taifa.

Waziri Ndalichako, ameyasema hayo Jijini Arusha, alipokutana na wakuu wa shule,maafisa elimu na watendaji wakuu wa idara za elimu ambapo amesisitiza nidhamu ili kusaidia matokea mazuri na ya haraka ya kuboresha elimu nchini.

Waziri Ndalichako, amesema kuwa wataalamu mbalimbali ambao wanahitajia katika idara mbalimbali katika kukuza maendeleo wote wanahitaji zaidi mchango wa sekta ya elimu katika kuwapata wataalamu hao.

Aidha katika ziara aliyoifanya katika mkoa huo wa Arusha, Waziri Ndalichako, ametoa ufafanuzi zaidi wa sera ya elimu bure ambapo amesema kuwa wazazi bado wanajukumu la kushirikiana na serikali katika kuwasadia watoto kupata elimu bora.

Prof. Ndalichako amesema serikali haijawazuia wananchi wanaotaka kuchangia sekta ya elimu kutokana na changamoto zilizopo lakini haiko tayari kuona mwanafunzi anarudishwa nyumbani kwa sababu ya michango ya aina hiyo.
Viewing all 11654 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>