Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all 11654 articles
Browse latest View live

PICHA LUKUKI ZA MATUKIO BUNGENI DODOMA

$
0
0
 Mbunge wa Jimbo la Ulanga, Goodluck Mlinga ambaye alisababisha wabunge wanawake wa upinzani kutoka bungeni wiki iliyopita kwa madai ya kuwadhalilisha,akichangia hoja bungeni Dodoma jana, ambapo alieleza kwamba amekuwa akipata vitisho lakini ana imani Jeshi la Wananchi Tanzania lililowasambatisha waasi wa DRC Congo M23 litamlinda. PICHA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG.
 Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema akichangia hoja bungeni wakati wa kujadili Bajeti ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
 Wabunge wakiingia bungeni Dodoma  leo.
 Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba akijibu maswali yaliyoulizwa na wabunge
 Mwigulu Nchemba akijadiliana jambo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye.
 Waziri wa  Nchi Ofisi ya Ofisi ya Rais (Tamisemi), George Simbachawene (kushoto) akijadiliana jambo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), Angelah Kairuki (kulia) pamoja na Naibu wake, Seleman Jaffo bungeni Dodoma.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalim akiwasilisha makadilio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka 2016/2017 bungeni Dodoma leo
 Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea (Chadema), kushoto, akizungumza na Mbunge wa Hanang, Dk. Mary Nagu kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma.
 Mbunge wa Viti Maalum, Kiteto Koshuma akichangia wakati wa kujadili Bajeti ya Wizara ya Afya
 Mbunge wa Kigoma Kusini, Husna Mwilima na Waziri wa Fedha na Mipango wakiingia bungeni.
 Mbunge wa Viti Maalum, Catherine Magige akiingia bungeni Dodoma
 Mbunge wa Jimbo la Mlimba, Suzan Kiwanga (Chadema) akiwahi kuingia bungeni
Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea (kushoto) akiwa na Mbunge wa Busega, Raphael Chegeni walipokuwa wakiingia bungeni Dodoma

RAIS DKT. MAGUFULI AHUDHURIA SHEREHE ZA UAPISHO WA RAIS WA UGANDA YOWERI MUSEVENI KATIKA VIWANJA VYA KOLOLO JIJINI KAMPALA

$
0
0

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili kwenye Uwanja wa Kololo jijini Kampala kuhudhuria sherehe za uapisho wa Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Kaguta Museveni.
 Raiswa Uganda Yoweri Kaguta Museveni akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kuwasili  kwenye viwanja hivyo.  
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais mstaafu wa awamu ya Pili Alhaji Ali Hassani Mwinyi kwenye viwanja vya Kololo jijini Kampala Uganda. Rais Mstaafu Mwinyi alihudhuria pia sherehe za uapisho wa Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Kaguta Museveni.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete kwenye viwanja vya Kololo jijini Kampala Uganda. Rais Mstaafu Kikwete pia alihudhuria sherehe za uapisho wa Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Kaguta Museveni.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na viongozi wa mataifa mbalimbali katika viwanja vya Kololo jijini Kampala.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mmoja wa viongozi wa dini wa Taifa la Uganda katika viwanja vya Kololo jijini Kampala. 
Raiswa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akijadiliana jambo kwa furaha na Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt.
Jakaya Kikwete pamoja na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya
kuapishwa kwa Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni katika viwanja vya  Kololo jijini Kampala Uganda. Picha na IKULU.

NHIF LINDI YAWAPA ELIMU YA TOTO AFYA KADI AKINA MAMA WA HALMASHAURI YA (W) LIWALE

$
0
0
1 
Meneja wa Bima ya Afya Mkoa wa Lindi akitoa elimu ya mpango mpya na wa gharama nafuu utakaomuwezesha mzazi kumlipia bima ya Afya mtoto chini ya miaka 18 unaojulikana TOTO AFYA KADI,kwenye kliniki ya mama na mtoto (RCH) Hospitali ya Wilaya ya Liwale mkoani Lindi.
2 
Kaimu mganga mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Liwale akitoa rai kwa akina mama walioudhuria kliniki kwa kuchangamkia fursa kwani ni mpango wenye manufaa zaidi na una uwigo wa mafao kwa 50,400 tu.
3 
Akina mama wakifuatilia elimu ya kitita cha mafao yanayotolewa kwenye mpango wa Toto afya kadi kutoka kwa meneja wa NHIF Lindi hayupo pichani.

MeTL YAKANUSHA KUFICHA SUKARI, YAELEZA HALI HALISI

$
0
0
industrial sugar
Kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL) imekanusha taarifa ambayo ilitolewa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa kampuni hiyo imeficha sukari tani 2,990 katika Bandari Kavu (ICD) ya PMM iliyopo Vingunguti, Dar es Salaam.

Taarifa hiyo imekuja baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutembelea ICD na kukuta tani 2,990 ambazo aliambiwa kuwa ni mali ya Mohammed Enterprises jambo ambalo halikuwa na usahihi bali ni mali ya Tanzania Commodities Trading inayomilikiwa na Murtaza Dewji.

Kwaa mujibu wa Murtaza Dewji ambaye ndiyo mmiliki wa sukari hiyo amesema kuwa sukari hiyo iliingia nchini kwa kufata utaratibu wote kama jinsi inavyotakiwa na anashangazwa kwanini hakufatwa ili kutoa maelezo kuhusu sukari hiyo.

“Tulifuata taratibu zote zikiwepo mamlaka husika za nchi kma bodi ya sukari, Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) na vyombo vyote vya ulinzi na usalama,” amesema Murtaza.

Akifafanua zaidi amesema kuwa sukari hiyo ilikuwa njiani kuelekea nchini Uganda na vielelezo vyote vipo lakini kutokana na uhaba wa sukari nchini, serikali iliagiza mzigo huo kubaki nchini na kuingiza sokoni ili kumaliza tatizo hilo ambapo ulitakiwa kuanza kuingia sokoni kati ya Mei, 12 na Mei, 13.

Aidha ameelezea kuwa ni jambo la kawaida kuagiza sukari kutoka Dubai kwani hutumia siku 7 pekee kufika nchini tofauti na sukari kutoka Brazil ambayo hutumia siku 50 hadi 60 ikiwa njiani hadi kufika nchini.

“Wafanyabiashara wote wanaojua biashara walioko karibu na Dubai hufanya hivyo na sisi sio wa kwanza kuagiza sukari kutoka kwa wauzaji wa Dubai,” amesema Murtaza.

Pia Murtaza amewatoa hofu Watanzania kuhusu uhaba wa sukari kwa kusema kuwa tayari sukari imeagizwa na ndani ya wiki mbili kutakuwa na sukari ya uhakika nchini hivyo kuwataka kuondoa hofu iliyokuwapo hapo awali.
Kibali halali cha TFDA hiki hapa chini

TANZANIA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO MKUU WA WAKADIRIAJI MAJENZI, AFRIKA UTAKAOFANYIKA MWEZI AGOSTI 2016 JIJINI DAR

$
0
0
 Rais wa Chama cha Wakadiriaji Majenzi Tanzania (TIQS), Samuel Marwa (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo (hawapo pichani), kuhusu Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano mkuu wa wakadiriaji majenzi, Afrika utakaofanyika Agosti 2016. Kutoka kulia ni Mjumbe wa chama hicho, Neema Shabani na Bahati Mbambe.
 Rais wa Chama cha Wakadiriaji Majenzi Tanzania (TIQS), Samuel Marwa (katikati), akisisitiza jambo katika mkutano huo. Kutoka kushoto ni Mjumbe wa chama hicho, Joseph Mhonda, Katibu wa chama hicho, Bernard Ndakidemi, Mjumbe wa Chama hicho, Bahati Mbambe na Mjumbe, Neema Shaban.
 Mjumbe wa Chama hicho, Bahati Mbambe (kulia), akisisitiza jambo.
 Mjumbe wa Chama hicho, Neema Shabani akisisitiza jambo kwenye mkutano huo.
 Mjumbe wa chama hicho, Joseph Mhonda akitoa ufafanuzi kadhaa baada ya waandishi wa habari kuuliza maswali.
 Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
---
Na Dotto Mwaibale

CHAMA Cha Wakadiriaji Majengo Tanzania (TIQS) kwa kushirikiana na Chama cha wakadiriaji majenzi Afrika (AAQS), watakuwa wenyeji wa mkutano mkuu wa Wakadiriaji Majenzi wa Afrika utakaofanyika tarehe 18 na 19 Agosti 2016 jijini Dar es Salaam.

Katika hatua nyingine chama hicho kimemuomba Rais John Magufuli,awape kazi katika miradi ya ujenzi, ili aweze kupunguza upotevu wa fedha unaotokana udanganyifu unaofanywa na baadhi ya watu.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi Rais wa TIQS, Samweli Marwa alisema kuwa, wamesikia kilio cha Rais kuhusu ufisadi unaotokea katika miradi mbalimbali ya ujenzi hapanchini, na kusababishia hasara kubwa Serikali.

‘’Sisi tuko tayari kutumia taaluma yetu, ilikumsaidia RaisMagufuli, kwani watu wamezidi kudanganya kwa lengo la kujinufaisha wenyewe’’ alisema.

Marwa alisema, Rais akiwatumia wao wataweza kupunguza gharama za ujenzi, pamoja na kujua gharama kabla ya kuingia mikataba mbalimbali.

Alisema kuwa, huduma ya ukadiriaji majengo ni nguzo muhimu katika kuchangia ufanisi na udhibiti wa gharama za ujenzi, ikiwa pamoja na ukamilishaji kwa muda wa miradi na kupata thamani ya fedha.

Marwa alisemawao kazi yao, wanatathmini kabla ya kujenga hivyo Rais atakuwa na uhuru wa kukubali mradi au lah, endapoataonagharamaimekuwakubwa.

Wakati huo huo Chama hicho, kimemuomba Magufuli kuwa mgeni rasmi katika mkutano Mkuu wa Afrika wa wakadiriaji majengo unaotarajia kufanyika Agosti 18 na 19 Jijini Dar es Salaam.

Marwa alisema kuwa, kwa kutambua umuhimu wakazi yao katika Taifa hili, wameona ni vema kama Rais angekuwepo katika mkutano huo iliaweze kujua mambo mbalimbali yahusuyo chama hicho.

Alisemakuwa, mada Kuu katika mkutano huo ni’ kufikiaMalengo endelevu(SDGs)-
mchango wahuduma za ukadiriaji majengo’ yanayokusudia kuondoa umaskini, kupambana na udhalimu, kuleta usawa pamoja na kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.

SWAHILI TV R.I.P. ANDREW NICKY SANGA FROM HOUSTON, TEXAS PART 1

$
0
0

MRADI MAALUM WA SERIKALI YA MAREKANI KUWASAIDIA WASICHANA WENGI ZAIDI WA KITANZANIA KUPATA ELIMU BORA

$
0
0
Nchi za Tanzania na Malawi zitapokea fedha kama nchi za kwanza za kipaumbele chini ya mradi maalumu wa kuwasaidia watoto wa kike kupata elimu bora ujulikanao kama “Let Girls Learn” uliozinduliwa na Rais wa Marekani Barack Obama na mkewe, Mama Michelle Obama mwaka 2015. Kwa hali hiyo, Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) kuanzia tarehe 10 -12 Mei 2016 katika hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam, liliendesha warsha iliyowakutanisha wataalamu mbalimbali wa maendeleo ya kimataifa wa ndani na nje ya nchi, wafadhili na viongozi wa kiserikali kutoka Tanzania na Malawi ili kubuni kwa pamoja mikakati na mbinu zitakazowasaidia wasichana katika nchi hizi kupata elimu bora.

“Mradi huu unawaweka wasichana kama walengwa wakuu na kitovu cha jitihada zetu za kuboresha elimu na maendeleo duniani kote,” alisema Susan Markham, Mratibu Mwandamizi wa Usawa wa Jinsia na Uwezeshaji wa Wanawake wa USAID. “Kwa kuelekeza jitihada zetu katika kushughulikia mahitaji maalumu ya wasichana, tunaweza kutatua kwa ufanisi zaidi vingi ya vikwazo vinavyowakwamisha wasiweze kupata elimu wanayostahili kuipata.”

Japokuwa nchini Tanzania watoto wa kike na wa kiume huandikishwa katika shule za msingi kwa uwiano ulio sawa, kuna pengo kubwa baina yao katika kiwango chao cha kumaliza shule za sekondari. Miongoni mwa vijana wenye umri wa kati ya miaka 20 na 24 ni aslimia 20 tu ya vijana wa kike ndio wameweza kumaliza elimu ya sekondari ikilinganishwa na zaidi ya asilimia 32 ya vijana wa kiume. Aidha, takwimu za Idadi ya Watu Kiumri na Afya ( Tanzania’s Demographic Health Survey Data) za mwaka 2010 zinaonyesha kuwa asilimia 20 ya wanawake katika umri huo hawakuwa na elimu kabisa ikilinganisha na chini ya asilimia 10 kwa wanaume.

Katika warsha hiyo washiriki walijadili kuhusu njia mbalimbali za kubadilisha mitazamo katika ngazi ya mtu mmoja mmoja, jamii na taasisi kuhusu thamani ya watoto wa kike;kujenga na kuimarisha mazingira yatakayowawezesha watoto wa kike kwenda shule; na kubaini njia za kuwawezesha watoto wa kike kufanya maamuzi kuhusu maisha yao na kutoa mchango muhimu katika jamii zao. Mikakati iliyoandaliwa katika warsha hii itakuwa msingi wa miradi ya baadaye katika nchi za Tanzania na Malawi katika kuwasaidia watoto wa kike kupata elimu bora kwa ufanisi na kujenga tabia zitakazowawezesha kuwa na afya njema.

Zaidi ya wasichana milioni 62 duniani kote hawaendi shule hivyo kuleta hasara kubwa kwa familia, jamii na nchi zao. Wasichana wanaokwenda shule hatimaye hupata kipato kikubwa zaidi, hupata watoto wakiwa katika umri mkubwa zaidi na wana uwezekano mdogo zaidi wa kupata maambukizo ya VVU/UKIMWI. Kila mwaka ambao mtoto wa kike anaendelea kubaki shuleni, kipato chake huongezeka kwa asilimia 25 na kupunguza uwezekano wa vifo vya watoto wachanga kwa hadi asilimia 10. Isitoshe, wanawake wenye elimu huwekeza asilimia 90 ya vipato vyao kwa familia zao na wana uwezekano wa zaidi ya mara mbili kuwapeleka watoto wao shule.

Mradi huu ni matokeo ya jitihada za serikali ya Marekani kwa ujumla wake ukijengwa na kuimarishwa kupitia utaalamu na rasilimali za USAID, Ikulu ya Marekani, Shirika la Wafanyakazi wa Kujitolea wa Kimarekani (Peace Corps) na Wizara ya Mambo Nje ya Marekani. Aidha, warsha ya wiki hii inadhihirisha dhamira ya dhati ya serikali ya Marekani kusaidia maendeleo ya Tanzania na Malawi na kuziwezesha serikali zao kufikia malengo ya kuongeza upatikanaji na kukuza ubora wa elimu na mifumo yake na hatimaye kupata matokeo mazuri kielimu.

“Tunafahamu kuwa ukimuelimisha mtoto wa kike, unajenga familia yenye afya bora zaidi, unajenga jamii imara zaidi na hatimaye taifa imara linaloweza kukabiliana kikamilifu na changamoto kadha wa kadha,” alisema Kaimu Mkurugenzi wa USAID nchini Tanzania Daniel Moore. “Ni kwa sababu hiyo uwekezaji katika kuboresha uwezo wa watoto wa kike kupata elimu ni uwekezaji muhimu zaidi tunaoweza kuufanya katika kuhakikisha maendeleo endelevu nchini Tanzania, Malawi na kwingineko duniani.”

SERIKALI YATOA BILIONI 2.3 KUWALIPA WAFANYAKAZI WA NIDA

$
0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO


SERIKALI YATOA BILIONI 2.3 KUWALIPA WAFANYAKAZI WA NIDA

SERIKALI imeipatia Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Shilingi Billioni 2.3 (Bilioni mbili na milioni mia tatu) kwa ajili ya kuwalipa waliokuwa watumishi wa muda wa mamlaka hiyo, wapatao 597, waliosimamishwa kazi hivi karibuni.

Malipo hayo yanahusisha mishahara yao ya miezi minne, ukiwemo mshahara wa mwezi mmoja wa notisi ya kusimamishwa kazi, pamoja na malimbikizo ya madeni yao katika mifuko ya hifadhi ya jamii.Kabla ya NIDA kuwalipa watumishi hao fedha hizo, Wizara ya Fedha na Mipango iliamua kufanya uhakiki ili kujiridhisha kama madai hayo yalikuwa sahihi.

Uhakiki huo ulihusisha mahojiano ya ana kwa ana na watumishi hao pamoja na kupitia nyaraka mbalimbali zikiwemo majalada, mikataba ya ajira, madaftari ya mahudhurio, taarifa za kazi za kila siku na namba zao za akaunti za benki zilizokuwa zikitumika kulipa mishahara.

Katika uhakiki huo imebainika kuwa kulikuwa na kasoro ama changamoto kadhaa zikiwemo za kimikataba kati ya NIDA na watumishi hao.Wakati wa zoezi hilo, jumla ya watumishi 597 walipaswa kuhakikiwa lakini majina ya watumishi yaliyowasilishwa kuhakikiwa ana kwa ana kutoka NIDA, Tanzania bara yalikuwa 565.Hata hivyo, watumishi 516 pekee ndio waliojitokeza katika zoezi hilo na wengine 49 hawakujitokeza.

Watumishi wa muda 32 kutoka NIDA Tanzania Zanzibar, wanaofanya jumla ya watumishi wa Mamlaka hiyo waliosimamishwa kazi kufikia 597, walihakikiwa kwa kupitia majalada yao yaliyoko ofisi za NIDA Makao Makuu, na kubaini mikataba yao haikuwa na kasoro.

Kwa mantiki hiyo watumishi 427 kutoka Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar ndio waliokidhi vigezo vya kulipwa stahili zao za kuachishwa kazi.Aidha, watumishi wengine 121, walibainika kuwa na kasoro mbalimbali ambazo zinapaswa kurekebishwa na Menejimenti ya NIDA kabla ya kufanya malipo hayo.

Baadhi ya kasoro zilizobainika katika uhakiki huo ni pamoja na kukosekana kwa mikataba na majalada yao katika Ofisi ya mwajiri, kukosekana majina yao kwenye daftari la mahudhurio kazini, kuwa na utata kwenye mikataba (kutofautiana tarehe na sahihi za wahusika), kufanana kwa namba za majarada, na kukosekana kwa barua za kusitishwa kazi.

Wizara ya Fedha na Mipango imemaliza kazi yake ya uhakiki na kwamba jukumu la kuwalipa watumishi wa NIDA wanaostahili limeachwa mikononi mwa menejimenti ya NIDA.

Imetolewa na:

Benny Mwaipaja
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO
13 Mei, 2016

MKONGWE WA DANSI NCHINI, ZAHIR ALLY ZORO ATAKA MUZIKI WA DANSI KUFUFULIWA MKOANI MWANZA

$
0
0
Mwanamuziki Mkongwe wa Muziki wa dansi nchini Tanzania, Zahir Ally Zorro (Kushoto) akizungumza na George Binagi @BMG (Kulia).
---
Mwanamuziki mkongwe wa dansi nchini, Zahir Ally Zorro, amewahimiza wadau wa muziki wa dansi Mkoani Mwanza, kuwaunganisha wanamuziki wa muziki huo ili kuurudisha kwenye chati kama zamani.

Alitoa kauli hiyo jana Jijini Mwanza, wakati akizungumza na BMG, ambapo alisema muziki wa dansi nchini umepotea sokoni hivyo jitihada zote zinafanyika ili kuurudisha katika soko, akitolea mfano Mkoani Mwanza ambapo kuna uhaba wa band za muziki wa dansi.

"Muziki wa dansi upo na tunajitahidi kuurudisha katika soko. Mwanza kuna vijana wengi wanafanya muziki wa dansi, wanaposhindwa kusikilizwa na media inauma sana hivyo ni vyema wakaunganishwa pamoja kwa ajili ya maendeleo ya muziki wa Mwanza". Alisema Zorro.

Mbali na hayo, Zorro ambae alianza muziki tangu mwaka 1968, yuko Jijini Mwanza kikazi ambapo leo jumamosi May 14,2016 atakuwa na show kali ndani ya Kilimanjaro Club iliyopo Nyegezi, atakapokuwa akinyukana na wenyeji wake Twiga Band.
Picha na Iman Hezron

BLOGGERS WATINGA BUNGENI KWA MWALIKO WA WAZIRI NAPE

$
0
0
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (aliyevaa tai) akiwa katika picha  ya pamoja na wamiliki wa Blogs  (Bloggers) aliowaalika wakati wa kuwasilisha hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa Fedha wa 2016/2017, bungeni Dodoma. Kushoto ni Naibu Waziri wa wizara hiyo,Annastazia  Wambura. (PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Baadhi ya Bloggers wakiwa bungeni wakati wa Bajeti ya wizara hiyo
 Waziri Kivuli wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Joseph Mbilinyi 'Mr Sugu' akisoma taarifa ya maoni ya upinzani kuhusu wizara hiyo.
 Baadhi ya Bloggers wakisikiliza mwenendo wa bunge. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Muda wa Chama cha Wamiliki wa Bloggers Tanzania (TBN).
 Nape akiwa na Bloggers pamoja na wasanii bungeni Dodoma.
 Nape akiwa na Bloggers.
 Nape akisalimiana na Blogger Salum Mwinyimkuu.
Mmiliki wa Blog ya Fullshangwe, John Bukuku (kushoto) na Mmiliki wa Matukio360 Blog Salum Mwinyimkuu wakiwa na mwandishi wa habari wa Raia Tanzania, Sharifa Malira.

NIKI WA PILI AKIZUNGUMZIA JINSI GANI TIGO MUSIC WANAVYOSAIDIA WASANII WA KIZAZI KIPYA TANZANIA

$
0
0

RAIS MAGUFULI AFANYA ZIARA YA GHAFLA TERMINAL ONE JNIA 13.05.2016

$
0
0

SHUKURANI TOKA KWA FAMILIA YA ANKAL KUFUATIA MSIBA WA MWANAE MAGGID

$
0
0
Familia ya Ankal Muhidin Issa Michuzi
  inapenda kutoa  shukrani nyingi sana sana kwa ndugu, jamaa,
majirani, marafiki na wafanyakazi wenzie kwa kujitoa kwa hali na mali katika wakati huu mgumu wa msiba wa mawanae Maggid (pichani) aliyefariki huko Durban, Afrika Kusini Jumapili ya wiki iliyopita  na kuzikwa katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam juzi Jumamosi.

Ni vigumu mno kumshukuru mtu mmoja mmoja kutokana na wingi wenu na kwa jinsi kila mmoja wenu alivyojitoa na kuonesha upendo wa dhati kabla na baada ya mazishi. Tunaweza kujaza kurasa 200 kama hizi na tusiwe tumehitimisha robo tu ya shukrani zetu kwa kila mmoja wenu.

Hivyo tunaomba radhi kwa yoyote ambaye hatutomtaja, kwani wafadhili wetu nyie mko wengi mno.

Pamoja  na hayo shukrani za kipekee ziwaendee Mheshimiwa Rais  Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Mama Janeth Magufuli na familia yao yote, Rais Mstaafu wa awamu ya Nne Dkt.  Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete na familia yao yote,  Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi na familia yake yote, Rais Mstafu wa awamu ya Tatu Mzee Benjamin William Mkapa na Mama Anna Mkapa na  familia yao yote, Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba na Familia yake yote, Katibu Mkuu Kiongozi  Mhandisi Allan Kijazi, Katibu Mkuu Ikulu Mhe. Peter Ilomo, Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu Mhe. Ombeni Sefue  pamoja na wafanyakazi wenzie wote wa baba mfiwa kwa kuwa karibu naye katika wakati wote, na kuhakikisha kuwa  kila kitu katika msiba huu kinaenda sawasawa. 

TUNAWAOMBEA KWA MOLA AWAPE BARAKA ZAKE ZOTE...

Salamu zingine za kipekee ziwaendee watumishi  wote wa Ubalozi wetu Afrika kusini mjini Pretoria ambao wakiwa chini ya Brigedia Jenerali Kimaryo na Afisa wa Ubalozi kaka Awesi walisimamia maswala yote ya kuusafirisha mwili kutoka Durban kuja Dar es salaam. 

MOLA AWAONGEZEE PALE MTAPOPUNGUKIWA...

Vile vile shukrani za kipeke ziwaendee Viongozi na wanachama wa Jumuiya ya Watanzania waishio Durban pamoja na Muslim Burial Society ya hapo hapo Durban ambao walihakikisha mwili wa marehemu unahifadhiwa, unakafiniwa na unasafirishwa kwa heshima zote.  ALLAH AWAJAALIE KATIKA KILA JAMBO...

Kwa Uongozi wa msikiti wa Maamur uliopo Upanga Dar es salaam pia familia inatoa shukurani  za kipekee kwa yote mliotutendea ikiwa ni pamoja na mwongozo wa kidini katika wakati wote wa msiba na mazishi.
Tutakuwa watovu wa fadhila endapo kama hatutatoa shukurani za kipekee kwa magrupu ya WhatsApp yote ambayo baba  mfiwa Ankal ni mwanachama.

Shukurani hizi maalum ziwaendee Ma-Admin na wanachama wa Kariakoo Family Group (KFG), Dar es salaam Old Friends (DOF), Ma Best Group (MBG), Wanahabari, Tasnia ya Habari, Uongozi, Siasa na Matukio Mix, The New Team, TSJ Alumni, Zama Zile, The Brain Team, Jazz Fans, The Kop in Tanzania, LFC Bongo, Uswazi Academia, Tanzania Bloggers Network (TBN), The Legends Family, SID Tanzania Chapter, Mawasiliano, Team Michuzi, Amani Kwanza Group, Photojournalists TZ, PPAT Members, P Mamas,
RUBY 15, Warembo wa KA, Mambachoz Group, Ndanshau Group, Empress Group kwa Fundi Mussa na wengi wengine wote katika Social media wakiongozwa na  Jamii Forum na VIJIMAMBO BLOG ya Marekani. 


TUMEHEMEWA MNO NA KUFARIJIKA SANA  KWA MICHANGO YENU
YA HALI NA MALI. WE ARE HUMBLED. MBARIKIWE SANA, SANA, SANA...
Mwisho, lakini sio kwa umuhimu bali kwa nafasi na mpangilio, tunatoa shukrani za kipekee kwa shirikia la ndege la Emirates kwa kufanikisha usafiri wa mwili wa marehemu, hali kadhalika kampuni mahiri ya SWISSPORT kwa kusaidia logostics zote katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es salaam.

HATUNA CHA KUWALIPA ZAIDI YA KUTOA SHUKURANI NA KUSEMA ASANTE SANA NA KUWAOMBEA KWA MOLA KILA MMOJA WENU AWABARIKI KATIKA SHUGHULI ZENU ZOTE...

Inna Lillahi wa inna ilaihi raji'un.

MAZISHI YA MTOTO WA ANKAL MICHUZI, MAGGID MICHUZI

$
0
0
Mwili wa marehemu ukiingizwa katika msikiti wa Maamur Upanga jijini Dar es salaam leo tayari kwa kuswaliwa kabla ya mazishi.
Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete (kushoto) akimfariji  baba wa marehemu Ankal Issa Michuzi. 
Mama wa marehemu (aliyevaa nguo nyeupe) akiwa na ndugu wa karibu wakiomboleza. 
Baba wa marehemu akiwa na viongozi wa dini wakiombea mwili wa marehemu dua.
Mke wa Rais mama Janeth Magufuli (kulia) akiwa na ndugu wa marehemu. 
Baba wa marehemu Ankal Issa Michuzi akipata chakula.
Mke wa Rais mama Janeth Magufuli (kulia) akiwasili msibani Wazo hill akiwa  na baba wa marehemu Ankal Issa Michuzi.
Baba wa marehemu akiwa na Balozi Cisco Mtiro na baadhi ya waombolezaji.
Baba wa marehemu (mwenye kofia), Ankal Issa Michuzi akipewa pole na baadhi ya waombolezaji mara baada ya maziko ya mtoto wake Maggid Muhidin Michuzi (18) yaliyofanyika katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam leo.
Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba akimpa pole Issa Michuzi.
Rais Mstaa mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete akimfariji Ankal Issa Michuzi.
Issa Michuzi (mwenye kofia) akifuatiwa na Rais mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete,  kulia kwake ni Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba na Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu Mhe Ombeni Sefue. Kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi  John Kijazi, Katibu Mkuu Ikulu Mhe. Peter Ilomo wakati maziko.
Waumini wakiomba dua.
Baba wa marehemu Issa Michuzi (katikati) akiwa na huzuni akiwa na Rais mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete,  kulia kwake ni Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde 
Baba mkubwa wa marehemu, Ismail Issa Michuzi akitoa shukrani kwa walioshiriki mazishi ya mtoto wao.
Mroki Mroki ambaye aliyekuwa MC akitoa ya muongozo wakati wa mazishi.
Waombolezaji wakiweka udongo kwenye kaburi la marehemu.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Mhandisi John Kijazi akiweka udongo.
Waziri Mkuu mstaafu Jaji  Joseph Sinde Warioba akiweka udongo kaburini.
Rais mstaafu Jakaya Kikwete akiweka udongo kaburini.
Baba wa marehemu Ankal  Issa Michuzi akiweka udongo kaburini.
Mwili wa marehemu ukiwekwa kaburini.
Mwili ukiwasili makaburini.
Rais mstaafu Jakaya Kikwete akimpa pole baba wa marehemu, Ankal  Issa Michuzi. Kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi  John Kijazi. Picha zote na Francis Dande.

TAASISI YA KARIMJEE JIVANJEE YATOA TSH. 10 MIL KWA TAASISI YA TUSHIKAMANE PAMOJA FOUNDATION

$
0
0
 Meneja wa Taasisi ya Karimjee Jivanjee, Devotha Rubama (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi Mwenyekiti wa Taasisi ya Tushikamane Pamoja inayoshughulika na kutoa huduma kwa wazee, Rose Mwapachu wakati wa hafla ya kuchangisha fedha kuisaidia taasisi hiyo jijini Dar es Salaam jana (katikati) ni Meneja Mahusiano na Mauzo wa Toyota Tanzania, Kadiva William
Meneja wa Taasisi ya Karimjee Jivanjee, Devotha Rubama (katikati) akisalimiana na Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi wakati wa hafla ya kuchangisha fedha kuisaidia taasisi Tushikamane Pamoja jijini Dar es Salaam jana (kulia) ni Meneja Mahusiano na Mauzo wa Toyota Tanzania, Kadiva William. Taasisi ya Karimjee Jivanjee ilichangia shilingi milioni 10.

SWAHILI TV ZAIDI YA MILIONI MIA MOJA TSHS. ZILIVYOCHANGWA KWA KING DREW

$
0
0

DK. MENGI ATOA DARASA KWA WASHIRIKI WA CHUO CHA ULINZI CHA TAIFA

$
0
0
Dk. Reginald Mengi saini
Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Ltd, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Dk. Reginald Mengi akisaini kitabu cha wageni alipowasili kwenye Chuo cha Ulinzi cha Taifa kilichopo Kunduchi, jijini Dar es Salaam Mei 16, 2016 kwa ajili ya kutoa muhadhara kwa washiriki wa kozi ya mbinu za kiusalama katika chuo hicho.(Picha zote na Modewjiblog)

IMELEZWA jukumu la ulinzi na usalama kwa dunia ya sasa halimo kwenye mikono ya polisi na wanajeshi pekee bali ni la kila mtu katika nafasi aliyopo kama amani na demokrasia inatakiwa kuendelea kuwapo.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Chuo cha Ulinzi cha Taifa, Meja Jenerali Yacoub Mohamed wakati akizungumza na Modewjiblogofisini kwake baada ya mhadhahara ulioshirikisha wataalamu wa masuala ya habari kutoka sekta binafsi na umma ambao wanachukua kozi ya mbinu za usalama chuoni hapo.

“Zamani mambo ya usalama yalikuwa ya wanajeshi na Polisi lakini kwasasa mambo ni tofauti, kila mmoja anatakiwa kuhakikisha anakuwa mlinzi ili uwepo usalama wa kutosha kwahiyo tunaamini washiriki wakirudi vituoni kwao watazingatia usalama.

“Wote wanaokuja hapa wanakuwa ni viongozi au viongozi watarajiwa na kama sasa tuna wanafunzi 38, 12 sio Watanzania ni kutoka Kenya, Rwanda, Burundi, Malawi, Namibia, Botswana, Afrika Kusini, Zambia, Nigeria na China,” aliongeza Meja Jenerali Mohamed.

Wataalamu walioendesha mihadhara hiyo ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Ltd, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Dk. Reginald Mengi ambaye amepata nafasi ya kutoa elimu kuhusu habari kwa sekta binafsi na Mkuu wa Shirika la Utangazaji nchini (TBC) na mwanazuoni Dk. Ayoub Rioba ambaye aliwasilisha sekta ya umma.

Akielezea ujio wa Dk. Mengi chuoni hapo, alisema wamekuwa na taratibu wa kukaribisha watu mbalimbali ambao wanawaona wana uwezo wa kuelezea uzoefu wao katika mambo mbalimbali ambayo yanaweza kuwa na faida kwa washirika.

Alisema chuo chao kimekuwa hakina walimu wa kudumu hivyo pamoja na kutumia watu mbalimbali kama walivyofanya kwa Dk. Mengi pia wamekuwa wakiwatumia walimu wa vyuo vikuu ili kutoa elimu ambayo itawasaidia washiriki katika masomo yao ambayo wanayapata chuoni hapo.

“Chuo chetu hakina walimu wa moja kwa moja kwahiyo huwa tunatumia walimu kutoka vyuo vikuu vya hapa nchini lakini pia huwa tunakaribisha watu maarufu wanakuja ku’share’ uwezo wao kwa washiriki ambao wanakuwa wapo masomoni.

“Dk. Mengi ameshafika hapa chuoni mara tatu na sio mtu wa kwanza kuja alishakuja Pius Msekwa, Mawaziri, Katibu Mkuu kiongozi na hata jana tulikuwa na (Dkt. Ayoub) Rioba,” alisema Meja Jenerali Mohamed.
Dk Mengi na Meja Jenerali Yacoub Mohamed
Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Ltd, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Dk. Reginald Mengi akisalimiana Mkuu wa Chuo cha Ulinzi cha Taifa, Meja Jenerali Yacoub Mohamed (kulia) mara baada ya kuwasili chuoni hapo kutoa muhadhara kuhusu nafasi ya vyombo vya habari katika kuhakikisha usalama wa taifa kwa washiriki wa kozi ya mbinu za kiusalama Mei 16, 2016 jijini Dar es Salaam.

Alisema chuo hicho hupokea washiriki ambao ni viongozi katika ofisi wanazofanyia kazi na hupokea washiriki kutoka nchi mbalimbali ambapo hupatiwa elimu kuhusu usalama ili wanapotoka chuoni hapo wakafanye kazi kwa umakini ili wasiweze kuwa sababu ya kupoteza usalama katika maeneo yanayowazunguka.

Katika mada yake iliyozungumza kuhusu wajibu wa vyombo vya habari binafsi katika usalama wa Taifa, Dk. Mengi alisema vyombo visipokuwa makini vikawajibika kitaaluma vinaweza kusababisha migogoro itakayohatarisha usalama wa taifa.

Akielezea uzoefu wake kama mmiliki wa vyombo vya habari binafsi alisema usalama ni jambo la muhimu kwa kila mtu bila kujali ana nafasi gani katika nchi hivyo ni wajibu wa kila mtu kushiriki katika kuimarisha usalama.

Alisema vyombo vya habari wanahakikisha habari zinazotolewa zinakuwa hazina madhara ambayo yanaweza kusababisha upotevu wa amani lakini kusimamia misingi na maadili ya uandishi wa habari.
Brigadia Jenerali Yohana Mabongo
Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Ltd, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Dk. Reginald Mengi (kushoto) akisalimiana na Katibu wa Chuo cha Ulinzi cha Taifa, Brigadia Jenerali Yohano Mabongo mara baada ya kuwasili chuoni hapo.

“Kama kuna utulivu, mshikamano na usalama wa taifa kuna faida kwa taifa na hilo linaweza kusaidia kukuza kwa uchumi wa nchi ambao pia utakuwa na faida kwa kila mwananchi,
“Vyombo vya habari vinatakiwa kufuata maadili ya kazi yake kuupasha umma habari na kutoa elimu bila kuathiri hali ya amani na utulivu kwa sababu tunaelewa kuwa pamoja na kutoa habari lakini pia ni wajibu wetu kuhakikisha kuna usalama nchini,” alisema Dk. Mengi.
Yacoub Mohamed NDC
Mkuu wa Chuo cha Ulinzi cha Taifa, Meja Jenerali Yacoub Mohamed akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Ltd ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Dk. Reginald Mengi (hayupo pichani) kutoa muhadhara kuhusu nafasi ya vyombo vya habari katika kuhakikisha usalama wa taifa kwa washiriki wa kozi ya mbinu za kiusalama chuoni hapo.
Dk. Reginald Mengi 1
Mwenyekiti Mtendaji wa Makapuni ya IPP Ltd, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Dk. Reginald Mengi akitoa muhadhara kuhusu nafasi ya vyombo vya habari katika kuhakikisha usalama wa taifa kwa washiriki wa kozi ya mbinu za kiusalama (hawapo pichani) katika Chuo cha Ulinzi cha Taifa kilichopo Kunduchi, jijini Dar es Salaam Mei 16, 2016.
Reginald Mengi NDC
Mwenyekiti Mtendaji wa IPP ltd, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Dk. Reginald Mengi akitoa muhadhara kuhusu nafasi ya vyombo vya habari katika kuhakikisha usalama wa taifa kwa washiriki wa kozi ya mbinu za kiusalama katika Chuo cha Ulinzi cha Taifa kilichopo Kunduchi, jijini Dar es Salaam.
Meja Jenerali Yacoub Mohamed
Mkuu wa Chuo cha Ulinzi cha Taifa, Meja Jenerali Yacoub Mohamed akitoa historia fupi ya chuo hicho kwa waandishi wa habari (hawapo pichani).
Dk. Reginald Mengi akiaga
Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP Ltd, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Dk. Reginald Mengi akiagana na Mkuu wa Chuo cha Ulinzi cha Taifa, Meja Jenerali Yacoub Mohamed (kulia) mara baada ya kutoa muhadhara kuhusu nafasi ya vyombo vya habari katika kuhakikisha usalama wa taifa kwa washiriki wa kozi ya mbinu za kiusalama (hawapo pichani) katika chuo hicho kilichopo Kunduchi, jijini Dar es Salaam.
National Defence College
Muonekano wa mbele wa Jengo la Chuo cha Ulinzi cha Taifa kilichopo Kunduchi, jijini Dar es Salaam.

AIRTEL YAZINDUA KAMPENI YA MR. MONEY KUPITIA HUDUMA YA AIRTEL MONEY

$
0
0
Meneja wa Msoko wa Airtel Money, Moses James (katikati), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, wakati wa hafla ya kutambulisha huduma mpya ya Mr. Money, itakayomwezesha mtumiaji wa Airtel Money kurahisisha matumizi ya huduma za kifedha kupitia simu ya mkononi. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando na Meneja wa Airtel Money, Asupya Nalingigwa.
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juzi usiku, wakati wa hafla ya kutambulisha huduma mpya ya Mr. Money, itakayomwezesha mtumiaji wa Airtel Money kurahisisha matumizi ya huduma za kifedha kupitia simu ya mkononi. Kulia ni na Meneja wa Airtel Money, Asupya Nalingigwa na Meneja wa Msoko wa Airtel Money, Moses James.
Sehemu ya wafanyakazi wa Airtel Tanzania wakifuatilia jambo, wakati wa hafla ya kutambulisha huduma mpya ya Mr. Money, itakayomwezesha mtumiaji wa Airtel Money kurahisisha matumizi ya huduma za kifedha kupitia simu ya mkononi, iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.
Meneja wa Msoko wa Airtel Money, Moses James akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, wakati wa hafla ya kutambulisha huduma mpya ya Mr. Money, itakayomwezesha mtumiaji wa Airtel Money kurahisisha matumizi ya huduma za kifedha kupitia simu ya mkononi.
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juzi usiku, wakati wa hafla ya kutambulisha huduma mpya ya Mr. Money, itakayomwezesha mtumiaji wa Airtel Money kurahisisha matumizi ya huduma za kifedha kupitia simu ya mkononi.
---
Mr. money amezinduliwa kuleta urahisi na Uhakika kwa watumiaji wa Airtel Money

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imetambulisha na kuzindua kampeni yake mpya kwa wateja kupitia huduma yake yake yakifedha kwa njia ya Mtandao ya Airtel Money

Kampeni hiyo imezinduliwa katika ukumbi wa burudani/club wa Maisha basement jana usiku mbele ya waandishi wa habari na watangazaji wa vipindi vya redio toka redio mbalimbali huku Meneja wa huduma ya Airtel Money Moses Alphonce akitoa sababu za ujio wa Mr. Money kwamba amekuja na habari za unafuu urahisi na usalama unaopatikana kupitia huduma ya Airtel Money sasa ambapo huwezi kupata kwingine.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa Mr Money Meneja huyo alisema "Mr. Money anasema ‘tumia Airtel Money kwa kuwa ndio nafuu na hakika kuliko mitandao yote’ Kutuma pesa popote nchini ni BURE na kwa uhakika Lipia BILI kama LUKU na ujipatie nyongeza za unit za umeme, hii ni kwa Airtel money TU.

Au lipia Ving’amuzi kwa uhakika na kwa raha bila usumbufu.

Pia Ongeza salio popote ulipo kwa uhakika, utapata bonasi ya muda wa maongezi BURE.

Ukiwa na airtel money unaweza kufanya mengi Zaidi.

Piga *150*60# SASA ujinonee.

TRA YAFUNGUA MAFUNZO YA AWAMU YA PILI KWA WAFANYAKAZI WAKE.

$
0
0
 Mkuu wa chuo cha Kodi (TRA), Profesa Isaya Jairo  akizungumza  wakati wa hafla kufungua mafunzo ya awamu yapili ya wafanyakazi wa mamlaka ya mapato Tanzania(TRA) Amesema kuwa wameamua kuanzisha mpango huo kwa kushirikiana na Mamlaka ya mapato  ili kufundisha wafanyakazi wa TRA maadili na nyenzo za utendaji kazini  pamoja na kuendesha mafunzo ya dini ili kuwafanya wafanyakazi wawe wacha Mungu katika kazi zao.
 Kaimu Mkurugenzi Rasilimali Watu na Utawala wa TRA, Victor Kimaro akizungumza na wafanyakazi wa malaka ya Mapato Tanzania(TRA) wakati  wa kufungua mafunzo ya awamu ya pili kwa wafanyakazi wake 200. Pia amewataka wafanyakazi wote wanatakiwa wafanye kazi kwa maadili hususani upande wa ukusanyaji kodi na Chuo hicho kimewafundisha wafanyakazi hao kufanya kazi kwa ushindani katika maeneo ya kazi ili kuliletea taifa maendeleo yaliyokusudiwa.
 Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata akizungumza na wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) jijini Dar es Salaam leowakati wa kufungua mafunzo ya maadili kwa wafanyakazi wa TRA ambao wamefanya usaili na kufanikiwa kufunzu kusoma mafunzo hayo kwa wafanyakazi kwaajili ya kujifunza mambo mtambuka ya tasinia ya TRA. Lengo la kuwapa mafunzo hayo ni kutaka kuijenga Mamlaka ya Mapato (TRA) mpya.Kulia ni Mkuu wa chuo cha Kodi (TRA), Isaya Jairo na Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Rasiliamali watu na utawala katika chuo cha Kodi(TRA), Victor Kimaro wakiwa katika mkutano wa kufungua mafunzo ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA).
 Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata  akizungumza na wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA)leo jijini Dar es Salaam.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata na  Mkuu wa chuo cha Kodi (TRA), Profesa Isaya Jairo wakikata utepe kuzindua ripoti ya mafunzo kwa wanafunzi wa malaka ya Mapato Tanzania jijini Dar es Salaam leo.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata (Katikati walioshika vitabu ),Mkuu wa chuo cha Kodi (TRA), Profesa Isaya Jairo(Kulia) na Kaimu Mkurugenzi Rasilimali Watu na Utawala wa TRA, Victor Kimaro (kushoto) wakionyesha vitabu vya mafunzo kwa wafanyakazi wa TRA jijini Dar es Salaam leo.

 Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata  akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa TRA jijini Dar es Salaam leo. Wafanyakazi hao ndio wanaohudhulia mafunzo hayo.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata  amesema kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) imebakiza Tsh. Trilioni 2.363 ili kufikia lengo  walilojiwekea la kukusanya mapato ya trilioni 12.363 katika  mwaka wa fedha 2015/16, ambapo hadi sasa imekusanya kiasi cha Tsh. Trilioni 10. Ameyasema hayo wakati wa  hafla ya uzinduzi  wa awamu ya pili ya mpango wa mafunzo kwa wafanyakazi waliopo kwenye fursa ya ajira za taasisi hiyo.
Mkuu wa chuo cha Kodi (TRA), Profesa Isaya Jairo.
Kaimu Mkurugenzi Rasilimali Watu na Utawala wa TRA, Victor Kimaro akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo.

ZAIDI YA TANI 70 ZA SUKARI ZILIZOSALIMISHWA NA WAFANYABISHARA WAKUBWA ARUSHA ZAGAWIWA KWA WANANCHI KWA BEI NAFUU

$
0
0

Na Woinde Shizza, Arusha. 
Jumla ya tani 78 za sukari ambazo zilisalimishwa na baadhi ya wafanya biashara wa kubwa wa sukari katika jiji la Arusha zimegaiwa kwa wananchi wa wilaya ya Arusha mjini ambao walikuwa wanakabiliwa na tatizo kubwa la ukosefu wa sukari.

Sukari hiyo ambayo ilisalimishwa na wafanyabiashara wakubwa ambao ni Neema Investment imegaiwa katika jumla ya kata 25 zilizopo katika wilaya ya Arusha mjini huku kila kata ikiwa inapatiwa mifuko 1000 kwa ajili ya wananchi wake.


Akiongea na waandishi wa habari kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Arusha, Afisa tarafa wa kata ya Suye Felician Mtahengerwa alisema kuwa sukari sukari hiyo inayogaiwa kwa wananchi ni ile ambayo iliingizwa hapa mkoani na baadhi ya wafanya biashara wakubwa na kuisalimisha katika ofisi ya mkuuwa mkoa kama agizo lilivyotolewa.

Alisema kuwa mkuu wa mkoa wa Arusha alisema kuwa mfanya biashara yeyote wa sukari ambaye anaingiza sukari mkoani hapa anapaswa kutoa taarifa katika ofisi yake kabla ya kufanya kitu chochote ikiwemo kabla ya kuuza sukari hiyo ivyo wafanyabishara hawa waliisalimisha sukari hiyo na ndio ambayo inagaiwa kwa kufuata utaratibu.

Alisema awali walishagawa sukari tani 45 na sasa ivi wanagawa tani zingine 33 ambazo zimetoka kwa mfanyabishara Neema intaprasesi ambayo yeye aliingiza sukari hii mara baada ya serekali kutoa agizo hivyo aliamua kuisalimisha kwa kutoa taarifa katika ofisi ya mkuu wa mkoa na sasa ivi ndio wameigawa.


“Kuna utaratibu wa wafanyabishara wakubwa wanapoingiza sukar I tu hapa mkoani kutoa taarifa sehemu husika ili sukari ile iweze kugaiwa kwa kufuata utaratibu hivyo huyu alitoa taarifa na ndio maana tumekuja hapa kuungana nae kuakikisha kila kata inapata sukari mifuko 1000 ambayo itauzwa kwa bei halili ya serekali ambayo imeelekezwa”alisema Mtahengerwa.


Alisema kuwa utaratibu huu unaotumika wa kugawa sukari utaendelea hivi hivi na hata sukari ambayo imeagizwa na waziri mkuu iwapo itafika utaratibu huu huu ndio utatumika adi pale tatizo la sukari litakapo malizika kabisa

Alitoa wito kwa wafanyabiashara wakubwa ambao wanaingiza sukari kutoa taarifa katika ofisi husika kwani wakiingiza bila kutoa taarifa iwapo wakibainika watachukuliwa hatua ya kisheria nikiwa ni pamoja na kutaifishiwa sukari yote.

Aidha pia aliwataka wafanya bishara wadogo wadogo ambao wamepata sukari hiyo kuuza kwakufuata bei elekezi kwani wanapokiuka agizo hilo iwapo watabainika wameuza kwa bei ya juu tofauti na bei elekezi sheria kali watachukuliwa ikiwemo ya kuwapeleka mahakamani.


Kwa upande wake mfanyabishara mkuu ambaye alijitambulisha kwa jina la Romanusi Mwacha alisema kuwa yeye kama mfanyabishara mkubwa ameamua kumuunga Rais Magufuli mkono kwa kuanza kuuza sukari kwa bei elekezi japo kuwa amepata hasara kubwa.

Alisema kuwa kama yeye amenunua sukari shilingi 1900 kilo na bado ajaweka bei ya usafiri kutoka aliponunua dar adi hapa lakini kutokana na agizo la serekali ameamua kulifuata na kumuunga magufuli mkono na ndio maana pamoja yakuwa amenunua bei gali lakini anauza bei raisi kwa kilo shilingi 1700 ili mfanyabiashara mdogo anaenunua aweze kwenda kumuuzia mlaji bei ya shilingi 1800 kama serekali ilivyoelekeza.

Aliwasihi wafanyabishara wengine ambao wameficha sukari wazitoe na wale ambao wanauza katika maduka ya reja reja wauze bei elikezi ili kutoweza kumuumiza mlaji ambaye ni mwananchi.
Viewing all 11654 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>