Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all 11654 articles
Browse latest View live

RAIS DKT. MAGUFULI AMTEUA NDG. ALLY SALUM HAPI KUWA MKUU WA WILAYA YA KINONDONI

$
0
0

VIWANGO VYA KUBADILISHA PESA

$
0
0

TAARIFA KWA UMMA: UFAFANUZI JUU YA UVUMI KUHUSU HALI YA MFUKO WA TAIFA WA HIFADHI YA JAMII (NSSF)

$
0
0
Hivi karibuni kumekuwa na taarifa mbalimbali zisizo rasmi kuhusu hali na mwenendo wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF). Baadhi ya taarifa hizo zimekuwa zikieleza kwamba mali za Mfuko huo zimetumiwa vibaya na hivyo kuathiri mafao kwa wanachama. Taarifa hizi zimesababisha hofu na taharuki miongoni mwa wanachama wa NSSF na wadau wa Sekta ya Hifadhi ya jamii kwa ujumla kwa kuhofia usalama wa wa fedha na mafao yao.

Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) inapenda kuwaondoa hofu wanachama wote wa Mfuko wa NSSF na Wananchi kwa ujumla na kuwahakikishi kwamba Mfuko wa NSSF upo katika hali nzuri kifedha na unaendelea kulipa mafao ya wanachama kama kawaida. Kama mnavyofahamu, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko alikwishateuliwa na anaendelea na majukumu ya kusimamia shughuli zote za Mfuko. Vilevile, taratibu za kupata Bodi mpya ya Wadhamini ya Mfuko huo zipo katika hatua za mwisho.

Aidha, SSRA kwa kushirikiana na Benki Kuu ya Tanzania kwa mamlaka waliyopewa chini ya Kifungu cha 6(2) (c) cha Sheria Na.8 ya mwaka 2008 ikisomwa pamoja na kifungu cha 40 na cha 48 wanaendelea kufanya kaguzi za Mifuko yote ukiwemo Mfuko wa NSSF kwa lengo la kuhakikisha kwamba muda wote Mifuko yote inakuwa katika hali nzuri kwa maslahi ya wanachama na taifa kwa ujumla.

Mwisho, Mamlaka inapenda kuwaondoa wasiwasi wanachama walioathirika na taarifa hizi pamoja na wanachama wote wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na kuwahakikishia kwamba fedha na mafao yao yapo salama na Mamlaka inazifanyia kazi kero zao kwa bidii kubwa. Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii S.L.P 31846 Tovuti: www.ssra.go.tz Dar es Salaam.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii S.L.P 31846 Tovuti: www.ssra.go.tz Dar es Salaam

SERIKALI KUCHUNGUZA MKATABA WA JENGO LA MACHINGA COMPLEX

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaa, Paul Makonda (kulia), akikagua vizimba katika Jengo la Machinga Complex Dar es Salaam jana, baada ya kufanyika kikao cha kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa kilichoketi jana kujadili uendeshaji wa biashara wa katika jengo hilo pamoja na kamati ya mkoa iliyoundwa kuchunguza mkataba wa jengo.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaa, Paul Makonda akizungumza na wafanyabiashara katika Jengo la Machinga Complex Dar es Salaam jana, kuhusu uendeshaji wa jengo hilo.
 Makonda akiwasili katika viwanja vya Jengo la Machinga Complex kuzungumza na wafanyabiashara na wadau wengine. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi wengine ni viongozi wa jengo hilo.
Makonda akiangalia Uwanja wa Karume akiwa jengo la Machinga Complex.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, CP Simon Sirro akimuaga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda baada ya kumaliza kuzungumza na wananchi.

Na Dotto Mwaibale

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameagiza kufanyika kwa uchunguzi katika ujenzi wa jengo la Machinga Ciomplex ili kubaini uhalali wa mkataba uliotumika kujenga jengo hilo.

Aidha, amebainisha kuwa jengo la Machinga Complex kwa sasa linadaiwa zaidi ya Sh bilioni 36 kiasi ambacho ni mara tatu ya thamani halisi ya jengo hilo ambayo ni Sh 12 ambazo zinatakiwa kulipwa na wafanyabiashara wa jengo hilo.

Makonda aliyasema hayo Dar es Salaam  jana wakati alipotembelea jengo hilo lililopo Manispaa ya Ilala ili kujionea mazingira ya kufanyia biashara. Alisema kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa itaanza kufanya uchambuzi wa mikataba ili kupata uhalali wa gharama na kujua kiwango kinachostahili kulipwa na wafanyabiashara hao.

Alisema kamati hiyo ya ulinzi na usalama imekubali kutengeza kamati ndogo itakayoanza kazi leo ya kuchambua na kuanza mikataba.

“Ingekuwa vyema tungekuwa na mkutano wa kuwasikilizeni na kujua kero zenu, lakini tunayo sababu moja ya msingi ya kutowasikiliza , kwanza tunatafuta uhalali na utaratibu wa jengo hili lilivyojengwa.

Katika maelezo ya awali tuliyoyapata jengo hili uko mkanganyiko mkubwa,  inawezekana ni miongoni mwa mradi mkubwa uliofanyiwa ufisadi Tanzania, sasa hatuwezi kukaa kusikiliza habari ya kizimba change, kwanza tupate uhalali wa mkataba uliopelekea kujenga jengo hili,” alisema Makonda.

Alisema kamati ya wafanyabiashara wa soko hilo itakayoundwa chini ya usimamizi wake itaanza kazi ya kuchunguza ili kubaini uhalali wa mkataba na kujua kama waliongia mikataba hiyo walikuwa sahihi.

Makonda alitoa rai kwa wafanyabiashara kuwa rai ya Rais Magufuli ni kuwapigania wanyonge na kuhakikish awanatoka sehemu moja kwenda nyingine, hivyo wasaidiza wake kwa kupenda au kutokupenda wana jukumu la kuhakikisha wanafanikisha hilo.

Hivi karibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, George Simbachawene aliifuta bodi inayosimamia jengo hilo na kumsimamisha kazi meneja anayesimamia jengo hilo na kumtaka kwenda katika ofisi za jiji kwa ajili ya kumpangia kazi nyingine.

Katika hatua nyingine, Simbachawene alilikabidhi jengo hilo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa ajili ya kuandaa mpango wa kuwaingiza wafanyabiashara bila masharti huku ukiangaliwa utaratibu mpya kwa wafanyabiashara hao.
Katika mkutano wake na Jumuiya ya Wafanyabiashara nchini, Simbachawene alisema, jengo hilo limekuwa likitumiwa kinyume na lengo ambalo walitakiwa wafanyabiashara kulitumia kwa gharama kidogo lakini limekuwa likitumiwa na watu wengine tofauti na wafanyabiashara jambo ambalo limesababisha kushindwa kulipa deni linalodaiwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).

MABADILIKO YA UELEKEO WA BARABARA KATIKATI YA JIJI LA DAR ES SALAAM KUANZIA SIKU YA TAREHE 28/04/2014. TRAFFIC CIRCULATION AT CBD

$
0
0
 1. Kipande cha Mtaa wa Samora kuanzia Mnara wa Askari (Askari Monument) hadi Clock Tower, kutakuwa na mabadiliko ambayo magari yatakuwa yanaelekea Clock Tower badala ya Askari Monument.

2. Barabara ya Sokoine kuanzia Station hadi Makutano ya Mtaa wa Maktaba Posta Ya Zamani Magari yatakuwa yanaelekea Uelekeo mmoja wa Station Posta ya Zamani tofauti na ilivyo sasa Posta ya Zamani kwenda Station.

3. Barabara ya Kivukoni Kuanzia Posta ya Zamani hadi Ferry itakuwa barabara ya mielekeo miwili (Two Ways).

4. Barabara ya Samora kuanzia Mnara wa Askari hadi Ocean Road Hospitali itakuwa ni barabara ya mielekeo miwili.

5. Daladala Zote zitakazotokea barabara za Maktaba zitakunja kulia pembeni ya Jengo la NBC na hadi Makutano ya Mkwepu na kukunja kushoto kuingia Sokoine pale Posta ya Zamani na baadaye kukunja kushoto kuingia Makataba na kurudi Posta Mpya .

Key:

1. RANGI YA NJANO - Njia ya Uelekeo Mmoja {One Way}.

2. RANGI YA BLUE MPAUKO - Njia ya Mielekeo Miwili {Two Way}

3. RANGI YA KIJANI - Mitaa ya Kutembea kwa Miguu Magari marufuku {Walking Streets}

4. RANGI NYEKUNDU - Barabara za kupita Daladala

5. RANGI YA BLUU ILIYOIVA - Barabara za DART

6. DUARA ZA NJANO - Mzunguko {Roundabout}

7. MSALABA WA KIJANI - Makutano yenye Taa za kuongozea Magari {Singnalized Intersection}

Kwa Maelezo zaidi Wasiliana na Ofisi za DART

UBUNGO PLAZA GHOROFA YA KWANZA.

AU.

OFISI YA MHANDISI WA MANISPAA YA ILALA NA SHOPRITE SUPERMARKET JIRANI NA KAMATA

Ni muhimu kwa waendesha magari wote kujua habari hii muhimu !!!!

Hasa mimi ninayesoma sasa

Mtaarifu mwingine juu ya mabadiliko haya kuondoa usumbufu ifikapo siku ya Jumatatu 28/04/2014.

RAIS DKT. MAGUFULI AMUAPISHA MATHIAS MEINRAD CHIKAWE KUWA BALOZI MPYA WA TANZANIA NCHINI JAPAN

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mathias Meinrad Chikawe kuwa Balozi mpya wa Tanzania nchini Japan, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. Magufuli akimpongeza Mathias Meinrad Chikawe mara baada ya kumuapisha kuwa  Balozi Mpya wa Tanzania nchini Japani.
Balozi mpya wa Tanzania nchini Japan Mathias Chikawe akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kuamuapisha Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Balozi mpya wa Tanzania nchini Japan Mathias Chikawe pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU.

RAIS DKT. MAGUFULI AZINDUA RASMI DARAJA LA KIGAMBONI, ALIBATIZA JINA LA DARAJA LA NYERERE

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akikata utepe huku viongozi wengine wakiushikilia kuashiria uzinduzi rasmi wa Daraja la Kigamboni katika wilaya mpya ya Kigamboni jijini Dar es salaam leo Aprili 19, 2016. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipata picha ya kumbukumbu viongozi wengine baada ya  uzinduzi rasmi wa Daraja la Kigamboni katika wilaya mpya ya Kigamboni jijini Dar es salaam leo Aprili 19, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiteta jambo na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Dkt Ramadhani Dau wakati wa  uzinduzi rasmi wa Daraja la Kigamboni katika wilaya mpya ya Kigamboni jijini Dar es salaam leo Aprili 19, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli na viongozi wengine wakitembea juu ya Daraja la Kigamboni baada ya kulizindua katika wilaya mpya ya Kigamboni jijini Dar es salaam leo Aprili 19, 2016. PICHA NA IKULU.

DENMARK YATOA MSAADA WA VIFAA VYA MUZIKI KWA TAASISI YA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO (TaSUBA)

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sanaa Wizara ya Habari ,Utamaduni, Sanaa,na Michezo Leah Kihimbi akizindua mradi wa vyombo vya muziki kati ya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) na Kituo cha Utamaduni na Maendeleo cha Watu wa Denmark (CKU), uzinduzi huo ulifanyika katika Chuo cha Sanaa mjini Bagamoyo mkoani Pwani jana.
 Msimamizi wa program wa Kituo cha Utamaduni na Maendeleo Denmark (CKU) hapa Nchini,Mandolin Kahindi akielezea utekelezaji wa mpango wa utamaduni na ubunifu Tanzania inayotekelezwa na kituo hicho kwa ushirikiano na ubalozi wa Denmark nchini Tanzania.
 Kaimu Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni (TaSUba) , Michael Kadindena akitoa neno la shukrani wakati wa hafla hiyo.
 Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sanaa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa,na Michezo, Leah Kihimbi akipiga kinanda wakati wa uzinduzi wa mradi wa vyombo vya muziki kati ya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) na Kituo cha Utamaduni na Maendeleo cha Watu wa Denmark (CKU), uzinduzi huo ulifanyika katika Chuo cha sanaa Bagamoyo jana. Wanaoshudia katikati ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni (TaSUba) Michael Kadindena kulia ni Mratibu wa Mradi huo, Melkiades Banyanka.
 Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sanaa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Leah Kihimbi akipuliza Tarumbeta ambacho ni moja ya vifaa vya muziki vilivyotolewa na Kituo cha utamaduni na maendeleo cha Denmark (CKU).
Meza kuu, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sanaa Kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Leah Kihimbi (katikati) akiwa pamoja na viongozi wengine wakifuatilia burudani kutoka kwa wanafunzi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) wakati wa uzinduzi wa mradi huo.
 Wanafunzi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) wakitoa burudani.
Wanafunzi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA), pamoja na wageni waalikwa wakishuudia kwa uzinduzi wa mradi huo.
 Wanafunzi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA),pamoja na wageni waalikwa wakishuudia kwa uzinduzi wa mradi huo.
Picha ya pamoja.
---
KITUO cha Utamaduni na Maendeleo cha Denmark (CKU), kimetoa msaada wa vifaa vya muziki katika Tasisi ya sanaa na utamaduni Bagamoyo (TASUBA) vyenye thamani ya shilingi milioni 80 za kitanzania.

Mbali na kununua vifaa vya muziki, sehemu ya fedha hizo pia zitatumika katika matengenezo na usimamizi wa vifaa hivyo kwa kipindi cha mwaka mmoja wa mradi huo.

Akizungumza jana wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani Msimamizi wa program CKU hapa Nchini,Mandolin Kahindi anasema kuwa ni moja fursa ya kuendeleza utamaduni na maendeleo ya kiuchumi.

Alisema kuwa msaada huo ni utekelezaji wa mpango wa utamaduni na ubunifu Tanzania inayotekelezwa na kituo hicho kwa ushirikiano na ubalozi wa Denmark nchini Tanzania.

"Unajua mpango wa kuanza kutoa msaada Tasuba ulianza mwaka 2014 baada ya CKU kukitembelea chuo hicho na kuelezwa kinakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa vifaa vya muziki vya kufundishia na kujifunzia"alisema.

Alifafanua kuwa mpango huu wa kusaidia uliazinduliwa rasmi juni mwaka jana ililenga kutengeneza fursa za kiuchumi kupitia jukwaa la sanaa na ubunifu ambapo watanzania watajipambanua kupitia kushiriki shughuli mbalimbali za kitamaduni na kujipatia kipato.

Kwa upande wa Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sanaa Kutoka Wizara ya Habari, utamaduni, sanaa na michezo Leah Kihimbi alisema kuwa amefurahi kupata msaada huo katika chuo cha sanaa lengo likiwa ni kuendeleza vipaji hapa nchini.

"Katika chuo hiki ni kweli kulikuwa na uhaba wa vifaa vya kufundishia lakini sasa tumepokea msaada kutoka katika Danish Centre for Culture and Development(CKU) kuweza kuwasaidia wanafunzi katika chuo hiki.

Aliongeza na kusema kuwa ni jambo la kuigwa kwa tasisi nyingine lengo ni kuweza kusaidia vyuo mbalimbali hapa nchini.

MAONESHO YA NNE YA MADINI YA KIMATAIFA ARUSHA GEM FAIR YAFUNGULIWA JIJINI ARUSHA

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Arusha,Fadhili Nkurlu akifungua maonesho ya kimataifa ya madini ya Arusha Gem Fair kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Felix Ntibenda leo katika hoteli ya Mount Meru. Kaimu Kamishna wa Madini nchini,Mhandisi Ally Samaje akizungumza wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo,alisistiza nia ya serikali kupambana na utoroshwaji wa madini nje ya nchi.Mwenyekiti wa kamati ya Arusha Gem Fair,Peter Pereira akitoa neno la utanguliza wakati wa ufunguzi wa maonesho ya madini yanayohudhuriwa na waoneshaji na wanunuzi zaidi ya 400 kutoka sehemu mbalimbali duniani.Baadhi ya watumishi wa Wizara ya Nishati na Madini wakiwa kwenye maonesho ya madini jijini Arusha.Wadau wa sekta ya madini wakimsikiliza Mkuu wa wilaya.Wadau wa sekta ya madini wakimsikiliza Mkuu wa wilaya.Wanunuzi wa madini wakiangalia aina mbalimbali za madini kabla ya kununua.Madini aina ya TanzaniteMadini ya aina mbalimbali ambayo ni kati ya yanayooneshwa kwaajili ya kutafutiwa soko.Mkurugenzi wa kampuni ya Ruvu Gemstone Mining Company Limited,Dimitris Mantheakis(kushoto)akiwa na wateja wanaongalia aina za madini.

VIJANA ZAIDI YA 300 JIJINI DAR ES SALAM WANUFAIKA NA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI YA AIRTEL FURSA

$
0
0
 Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi akizungumza wakati wa mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, yaliyofanyika kwenye Ukumbi Urafiki jijini Dar es Salaam jana, ambapo vijana watatu kati ya 300 waliohudhuria walichaguliwa na kuwezeshwa vitendea kazi kutokana na biashara wanazozifanya.
 Mkufunzi kutoka Mpango wa Anzisha na Boresha Biashara yako (SIYB) ulio chini Shirika la Kazi Duniani (ILO), Fidelis Madaha akitoa mada wakati wa mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, yaliyofanyika kwenye Ukumbi Urafiki jijini Dar es Salaam jana, ambapo vijana watatu kati ya 300 waliohudhuria walichaguliwa na kuwezeshwa vitendea kazi kutokana na biashara wanazozifanya.
Msanii Mrisho Mpoto (kulia), akitoa mada wakati wa mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, yaliyofanyika kwenye Ukumbi Urafiki jijini Dar es Salaam jana, ambapo vijana watatu kati ya 300 waliohudhuria walichaguliwa na kuwezeshwa vitendea kazi kutokana na biashara wanazozifanya. Kushoto ni Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi.
---
*Vijana Watatu wamewezeshwa vitendea kazi katika warsha ya mafunzo ya ujasiriamali ya Airtel Fursa

Katika jitihada za kusaidia maendeleo, kuinua ujuzi na kujenga ajira katika Jamii ya kitanzania, Airtel Tanzania imeandaa warsha nyingine ya mafunzo ya ujasiriamali kwa zaidi ya vijana 300 na kuwapatia ujuzi muhimu katika kibiashara ili waweza kujiajiri na kuendesha maisha yao ya kila siku.

Warsha hiyo ilifanyika jana katika ukumbi wa Urafiki Social Hall, Shekilango jijini Dar es Salaam.

Katika warsha hiyo, kijana Stephano Gimase ambaye alikuwa ni miongoni mwa vijana aliyeweza kushiriki na kuelezea biashara yake ya ufugaji wa kuku mbele ya jopo la washauri na washiriki wengine wa warsha hiyo alibahatika kuwezeshwa kwa kupatiwa vitendea kazi kwa ajili ya biashara yake pamoja na kubadilisha maisha yake baada ya mchujo mkali katika warsha hiyo.

Vijana wengine waliohudhuria walionyesha shukrani kwa kampuni ya simu ya Airtel na kuahidi kutumia ujuzi waliopata katika warsha hiyo kwa manufaa yao wenyewe.

"Airtel imetambua changamoto ambazo vijana tunakumbana nazo katika maisha yetu ya kila siku. Sisi vijana tupo tayari kufanya kazi kwa bidii ili kufikia malengo yetu lakini hatuna ujuzi muhimu na zana ili kujenga biashara zetu. Airtel imeliona tatizo hili na kuchukua jukumu hili na kutusaidia sisi vijana, aliongea Yvonne Obeth mmoja wa vijana waliohudhuria.

"Leo hii tumepata stadi za msingi za ujasiriamali, nimejifunza umuhimu wa kutunza kumbukumbu bila kujali udogo wa biashara yangu. Sasa hivi ninajua jinsi ya kuweka vitabu yangu vya akaunti, jinsi ya kutafuta soko la bidhaa zangu hasa kwa kutumia teknolojia ili niweze kufikia wateja zaidi.

Kwa kifupi, warsha hii imekuwa mwangaza wa mafanikio wa maisha yangu. "aliongeza Obeth

Meneja kwa huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi alisema " Hii ni sehemu ya kurudisha fadhila zetu kwa jamii kwa kuunda fursa na kutengeza ajira kwa vijana. Kwani kijana akiwa na ujuzi wa mambo mbali mbali ni faida kwake na ananafasi kubwa ya kutengeneza ajira yake na Jamii inayomzunguka. Tunahitaji kuwawezesha vijana na kubadili mawazo yao kutoka kutaka kuajiriwa na kujiajiri wao wenyewe.

Kwa upande wake Stephano Gimase ambaye ni miongoni mwa vijana watatu walioweza kuwezeshwa na Airtel Fursa katika warsha hiyo na kupatiwa vitendea kazi, aliwashukuru Airtel kwa kuboresha biashara yake “ nimefurahi kupata Fursa hii kubwa ya kupatia vifaa na vitengea kazi, kwangu mimi huu ni muujiza, nimekuja kupata mafunzo lakini nimebahatika kuzaadiwa msaada mkubwa kwaajili ya kuinua biashara yangu. Nawashukuru sana Airtel kwa kuendelea kuwafikia vijana wengi ikiwa ni pamoja na mimi leo.

"Hadi sasa Airtel Fursa imeweza kufikia vijana zaidi ya 3,600 hapa nchini kupitia mafunzo haya ya elimu ya ujasiriamali."

FOLENI, MAFURIKO KUWA HISTORIA HALMASHAURI YA MANISPAA YA KINONDONI, DAR

$
0
0
 Hayo yamesemwa leo Jumatano tarehe 20 Aprili 2016 na Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Mh. Boniface Jackob wakati wa hafla ya kusaini Mkataba Na Kampuni ya MS/H.P GAUFF INGENIEURE GMBH&CO, KG -JBB ambayo ni mtaalam Mwelekezi (Consultant) atakayetoa Huduma za ushauri elekezi (Consultant services) katika, usimamizi wa ujenzi wa Miradi ya DMDP (Dar es Salaam, Metropolitan, Development Project) itakayotekelezwa ndani ndani ya Manispaa ya Kinondoni wenye thamani ya URO 4.678580 Na USD 402833 utakaodumu hadi mwisho wa muda wa utekelezaji wa miradi hiyo.

Mtaalam huyu mwelekezi atakuwa Na jukumu la kuhakikisha kazi zitakazofanyika zinakuwa katika mpangilio uliokubalika, (Designing) Na kwa kuzingatia ubora Na thamani ya miradi (Value for Money) ili wananchi wote wa Manispaa ya Kinondoni Na jiji la Dar es Salaam, wanufaike Na miradi hiyo kama ilivyokusudiwa katika malengo yake.

Halmashauri ya Kinondoni ina miradi 11 inayogusa maeneo ya Ujenzi wa Barabara za Halmashauri kwa kiwango cha lami zinazolenga kupunguza msongamano (Local Roads) Uboreshaji wa Miundombinu katika maeneo yasiyopangwa (Infrastructural upgrading in unplanned Settlements) Ujenzi wa mifereji ya maji ya mvua (Storm Water Drainage) Uimarishaji wa mifumo ya Mapato ya utawala Bora ya taasisi (Institutional Strengthen) Na Usimamizi wa taka ngumu (Solid waste Management).
 Kwa mujibu wa upembuzi yakinifu uliofanywa na wataalamu waelekezi (Consultants), Kati ya miradi yote 11 ya awamu ya kwanza na awamu ya pili, miradi 5 ya Barabara itakayotekelezwa katika awamu ya kwanza wakati wowote kuanzia sasa ambayo haihitaji ulipaji wa fidia katika utekelezaji na barabara 6 zitajengwa baada ya Manispaa kulipa fidia katika maeneo ya miradi, zote kwa ujumla zina urefu wa Kilometa 20.75 Na zitagharimu Tsh 26,552,114/= na fidia ya Tsh 6,672,251,760/=.

Mradi wa Uboreshaji wa maeneo yasiyopangwa utagusa kata 3 za Mburahati, Tandale Na Mwananyamala utakaohusisha uwekaji wa Huduma muhimu kwa kuboresha Miundombinu ya barabara, taa za barabarani, taka ngumu, njia za waenda kwa miguu Na maji safi utakaogharimu Tsh 1,264,576/= na fidia ya Tsh 180,413,275/=.
 Aidha mradi wa Ujenzi wa mto Sinza (Mto Ng'ombe) wenye urefu wa Kilometa 7 kuanzia chuo cha maji Dar es salaam hadi mto Msimbazi kupitia kata 6 za Ubungo, Sinza, Mwananyamala, Ndugumbi, Magomeni na Hananasif umelenga kuuwezesha mto huo kupitisha maji kwa urahisi Na kuepusha mafuriko Na utagharimu Tsh 20,100,000/= Na utahitaji fidia ya Tsh 4,054,499,410/=.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe. Boniface Jacob amewahakikishia wananchi wote wa Manispaa ya Kinondoni kuwa kwa kushirikiana Na Baraza lake la Madiwani na Serikali kuu na wadau wengine wakiwemo waheshimiwa wabunge, watafanya kila jitihada ya kutafuta fedha za kulipia fidia ili miradi hiyo ambayo inahitaji fidia ianze kutekelezwa na kukamilika kwa wakati ili kuwapunguzia wananchi kero ya msongamano uliopo ndani ya jiji la Dar es Salaam.

BARABARA ZITAKAZO NUFAIKA KWA KUJENGWA KIWANGO CHA LAMI

1.Sokoni Makumbusho Km 1.3
2.MMK 1.2
3.Nzasa Km 1.2
4.Tanesco - Soko la samaki mMsasani Km 1.5
5.Mikocheni viwandani Km 1.75
6.Makanya - Sinza Km 5.1
7.Tandale - Mwananyamala Km 0.8
8.Simu 2000 Sinza Km 1.3
9.Kilimani Manzese Km 1.3
10.Korogwe - Kirungule Kimara Km 3.0
11.Kilongawima Km 1.8

SURFACE DRAINAGE, (MFEREJI WA MAJI) ujenzi wa mto ng'ombe, kutoka Ubungo Chuo Kikuu to Magomeni

MHANDISI MANISPAA YA ILALA JIJINI DAR ES SALAAM NA WASAIDIZI WAKE WATUMBULIWA MAJIPU

$
0
0
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko, akizungumza na wanahabari kuhusu kumvua madaraka Mhandisi wa Manispaa hiyo kwa kufanyakazi chini ya kiwango pamoja na wasaidizi wake wawili.
---
Na Dotto Mwaibale

MANISPAA ya Ilala jijini Dar es Salaam imemvua madaraka Mkuu wa Idara ya ujenzi, Mhandisi Japhery Bwigane na wasaidizi wake wawili kwa tuhuma za kusimamia ujenzi wa barabara za manispaa hiyo kwa kujengwa chini ya kiwango.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam wakati akitoa taarifa hiyo, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko aliwataja maofisa wengine wa idara hiyo waliosimamishwa kuwa ni Siajari Mahili na Daniel Kirigiti ambao wamehamishwa idara hiyo ili kupisha uchunguzi unaoendelea.

Kuyeko alisema kikao cha Baraza la Madiwani kimefikia uamuzi huo baada ya manispaa kujiridhisha kuwa maofisa hao wamechangia kwa kiasi kikubwa ujenzi wa barabara mbovu ndani ya manispaa hiyo.

Alisema baada ya kuingia madarakani kwa miezi mitatu walijaribu kutafuta kero ndani ya manispaa ya Ilala ambapo walibaini idara ya ujenzi ina malalamiko mengi kutoka kwa madiwani wa kata mbalimbali kwa sababu ya kusimamia ujenzi wa barabara chini ya kiwango na hakuna hatua stahiki zilizochukuliwa na maofisa hao.

Alisema madiwani hao walimlalamikia Mhandisi Bwigane kuwa amekuwa akikaidi wito wao wa kujadili ujenzi wa barabara mbovu pindi zinapobainika jambo ambalo limesababisha manispaa hiyo kuwa na barabara nyingi mbovu.

Jitihada za gazeti hili za kumtafuta Mhandisi Bwigane ili kuzungumzia kusimamishwa kwake kazi hazikuzaa matunda baada ya kupigiwa simu yake na wakati wote kuwa imefungwa.

UVCCM YAMNG'OA KAMANDA WA VIJANA WILAYA YA ARUMERU MKOANI ARUSHA

$
0
0
 Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha Lengay Ole Sabaya akitoa tamko kwa waandishi wa habari jana jijini Arusha,ambapo amemtaja Mathias Manga na washirika wake kuwa ni tatizo kubwa ndani ya chama na kwamba kama akiendelea kuwepo ni Dhahiri kuwa anaweza kukisambaratisha chama hicho kutokana na kugawa makundi kwa vijana wa chama hicho kutokana na fedha zake.(Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
 Katibu hamasa Mkoa wa Arusha Lucas Msomi akisisitiza jambo katika kikao na waandishi wa habari
Baraza la vijana mkoa wa Arusha la Chama cha Mapinduzi UVCCM limetangaza kumvua ukamanda wa vijana wilaya ya Arumeru bw. Mathias Manga kutokana na kukiujumu chama kwa muda mrefu hali ambayo imekuwa ikididimiza jitihada za kurejesha imani ya chama hicho.
---
Bw. Manga ambaye ni mafanyabiashara maarufu wa madini Mkoani Arusha amekuwa akituhumiwa kwa muda mrefu kuwa namhausiano ya karibu ya aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Ukawa Edward Lowassa na kusahau kufanya majukumu ya kichama ambayo yamempa uongozi wa Ukamanda wa vijana wilaya.

Akitoa maelezo ya tamko hilo mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha, Lengay Ole Sabaya amemtaja Mathias Manga na washirika wake kuwa ni tatizo kubwa ndani ya chama na kwamba kama akiendelea kuwepo ni dhahiri kuwa anaweza kukisambaratisha chama hicho kutokana na kugawa makundi kwa vijana wa chama hicho kutokana na fedha zake.

Aliongeza kuwa kutokana na kumvua ukamanda kamanda huyo UVCCM Mkoani hapa haitakuwa tayari kushiriki kikao chochote cha kamati ya siasa ambapo Manga atashiriki kama mjumbe katika kikao hicho.

"Sitashiriki kwa namna yeyote na vijana wangu kwenye kikao cha kamati ya siasa Mkoa ama kikao kingine ambacho kitanikutanisha na Mathias Manga na nawataka wanachama wa chama cha mapinduzi kuona kama ni halali kwa huyu aliyeitwa kamanda wa vijana kuendelea kushikilia kadi yao," Alisema Ole Sabaya

Akitoa onyo kwa makamanda wilaya ya Arusha mjini,Longido na Monduli kujipima na kujitathimini kabla ya kufikia uamuzi kama bado wanafaa kuendelea na hadhi ya ukamanda wa wilaya ama laa,na wakijiona hawatoshi tunawashauri wakae pembeni mapema kabla ya kutumbuliwa jipu.

Baraza linakiomba chama cha Mapinduzi kupitia tathini ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana wale wote walioshiriki kukihujumu chama kuanzia ngazi ya matawi, kata, wilaya na Mkoa washughulikiwe kwa mujibu wa taratibu za kimaadili kabla ya uchaguzi wa chama 2017 vinginevyo wakiachwa watashiriki tena kufanya uhasi dhidi ya chama sanjari na kupandikiza mamluki.

Hata hivyo mwenyekiti huyo ametengua uteuzi wa wajumbe watano wa baraza katika nafasi za kuteuliwa ilidumu toka mwaka 2012 na kuunda kamati mpya chini ya mwenyekiti Lengai Ole Sabaya huku akiwataka viongozi wa chama hicho kumuunga mkono Rais JohnPombe Magufuli kwa jitihada zake za kupeperusha bendera ya chama na kufanya kazi kwa uadilifu na kubeba kauli ya HAPA KAZI TU.

MHE. DKT JAKAYA MRISHO KIKWETE AKUTANA NA WANAFUNZI NA WANACHAMA WA CCM WAISHIO JIJINI BEIJING - CHINA

$
0
0
Picha ya Pamoja
Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi {CCM} na Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Jakaya Mrisho akizungumza jambo mbele ya Wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya elimu ya juu(hawapo pichani), katika Ukumbi wa Grand uliopo katika Makazi ya Viongozi ya Diaoyutai State Guesthouse jijini Beijin, nchini China
Mmoja wa Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi wa Tawi la Beijing ambae pia ni Mwanafunzi,akizungumza jambo mbele ya Wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya elimu ya juu(hawapo pichani), katika Ukumbi wa Grand uliopo katika Makazi ya Viongozi ya Diaoyutai State Guesthouse jijini Beijin, nchini China,ambapo Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi {CCM} na Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Jakaya Mrisho alikuwa mgeni rasmi .
Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi {CCM} na Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Jakaya Mrisho Kikwete jana tarehe 20th April 2016 alikutana na Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi wa Tawi la Beijing ambao ni Wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya elimu ya juu, katika Ukumbi wa Grand uliopo katika Makazi ya Viongozi ya Diaoyutai State Guesthouse jijini Beijin, nchini China.

Wakisoma risala yao, Wanafunzi hao kutoka vyuo mbalimbali vilivyopo Beijin na miji ya karibu kama vile Tianjin walimuhakikishia Mheshimiwa Dkt. Kikwete kuwa wao ni waaminifu na wazalendo kwa Taifa lao na kwamba wako tayari kurudi nyumbani na kutumia elimu zao katika kuhakikisha kuwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii yanafikiwa.

Katika mazungumzo na Wanachama hao, Mhe Kikwete amewakumbusha jukumu kubwa lililo mbele yao la kujenga Chama na kulijenga Taifa la Tanzania, katika hotuba yake ameeleza kuwa China imefanya Mapinduzi makubwa katika maendeleo na kuboresha ustawi wa watu wa nchi hiyo, hivyo kuwataka kujifunza na kuchukua maarifa ya China na kuyatumia wakirudi nchini ili kufanikisha Mapinduzi makubwa ya Kiuchumi na maendeleo kwa ujumla.

Mheshimiwa Kikwete na Ujumbe wake wanatarajia kutembelea Jimbo la Fu Zhou hapo kesho na kushuhudia maendeleo makubwa yaliyosimamiwa na Katibu Mkuu wa CCP na Rais wa Serikali ya watu wa China Mhe Xi Jinping, pamoja na kufanya mazungumzo muhimu na Viongozi wa Chama Cha Kikomunisti cha China {CCP} katika jimbo hilo.

KATIBU MKUU WIZARA YA HABARI UTALII UTAMADUNI NA MICHEZO ZANZIBAR AKABIDHIWA OFISI RASMI

$
0
0

 Katibu Mkuu Wizara ya Habari  Utalii Utamaduni na Michezo Omar Hassan
Omar kushoto akikabithiwa nyaraka  na Katibu Mkuu Mstaafu Ali Mwinyikai  katika makabidhiano ya Ofisi yaliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya  Habari Utalii Utamaduni na Michezo  Kikwajuni Mjini Unguja.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari  Utalii Utamaduni na Michezo Omar Hassan  Omar kushoto na Katibu Mkuu Mstaafu Ali Mwinyikai wakitiliana saini  katika makabidhiano ya Ofisi yaliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Habari  Utalii Utamaduni na Michezo  Kikwajuni Mjini Unguja.
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utalii Utamaduni na Michezo Amina  Ameri Issa kulia akikabidhiwa nyaraka na Naibu Katibu Mkuu Mstaafu Issa  Mlingoti katika makabidhiano ya Ofisi yaliofanyika katika ukumbi wa  Wizara ya Habari  Utalii Utamaduni  na Michezo  Kikwajuni Mjini Unguja
 Katibu Mkuu Wizara ya Habari  Utalii Utamaduni na Michezo Omar Hassan  Omar akitoa nasaha zake kwa Wakurugenzi na Watendaji mbali mbali  waliohudhuria katika makabidhiano ya Ofisi yaliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Habari  Utalii Utamaduni  na Michezo  Kikwajuni Mjini Unguja
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utalii Utamaduni na Michezo Omar Hassan Omar mwenye koti na tai akiwa katika Picha ya pamoja na Naibu  katibu Mkuu wa Wizara hiyo Amina Ameri Issa pamoja na Wakurugenzi na  Watendaji wa Wizara ya Habari Utalii Utamaduni na Michezo Kikwajuni  Mjini Unguja. PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.

MAFANIKIO YA ZIARA YA WAFANYABIASHARA WA OMAN NCHINI

$
0
0
Na Immaculate Makilika – MAELEZO, DAR.

Tanzania na Oman zimesaini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano baina ya Tanzania Chambers of Commerce na Oman Chambers of Commerce ili kuanzisha Kampuni ya Oman Tanzania Investment (OTIC) kwa lengo la kutafuta fursa za uwekezaji zilizoko Tanzania na Oman.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Bibi. Mindi Kasiga amesema kuwa mkataba huo ni matokeo ya ziara ya siku tatu ya Waziri Viwanda na biashara wa Oman , Dkt. Ally Mohamed Al Sunaidy, pamoja na ujumbe wa wafanyabiashara 108 na maafisa wa Serikali ya Oman iliyofanyika nchini mwezi Aprili mwaka huu.

Amesema lengo la ziara hiyo lilikua kuwawezesha wafanyabishara wa Oman na Tanzania kushiriki kongamamo la biashara la uwekezaji lililowawezesha wafanya bishara hao kubaini fursa za uwekezaji zilizoko nchini Tanzania na Oman.

Amesema tayari Serikali ya Oman imeonesha nia ya kuwekeza katika kiwanda cha Sukari cha Kagera kilichopo mjini Morogoro ambacho kitazalisha tani laki nne za sukari itakayouzwa hapa nchini huku Tanzania ikitarajia kuzalisha spiriti na hamira itakayouzwa nchini Oman pamoja na nchi za Mashariki ya kati.‘’ Wafanyabishara wetu na wale wa Oman kupitia makubaliano haya watanufaika na fursa za uwekezaji kwa kupata mikopo mbalimbali na tayari mtaji wa Dola za Marekani milioni 25 zitatumika kwa wawekezaji hao’’ Amesema Bibi. Kasiga.

Aidha,amesema Wafanyabiashara kutoka Oman tayari wameonesha nia ya kuwekeza katika sekta mbalimbali ikiwemo madini, viwanda na biashara, kilimo, utalii pamoja na ujenzi wa nyumba za kisasa katika miji ya Dar es Salaam na Zanzibar.Ameongeza kuwa uwekezaji utaongeza ajira akitoa mfano wa kiwanda cha Sukari cha Kagera kitakachozalisha ajira 500 pamoja na kuongeza wigo wa soko.

Katika hatua amesema kuwa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa itawapeleka watumishi 105 wa ngazi mbalimbali katika Balozi 35 zilizo katika nchi mbalimbali duniani na kuwarudisha nyumbani watumishi 79.Bibi Mindi, ametaja sababu za kurudishwa kwa watumishi hao kuwa ni pamoja kuisha kwa muda wao wa kuhudumu nje ya nchi ambao ni miaka minne(tour on duty) pamoja, kustaafu na sababu mbalimbali.Amezitaja Kada za watumishi wanaorudishwa nchini kuwa ni mabalozi, wahasibu, makatibu muhktasi na maofisa wa ngazi mbalimbali.

Hata hivyo, hadi kufikia sasa tayari mabalozi watatu wamerudishwa nchini ambao ni Balozi Peter Kalaghe aliyekuwa Uingereza, Balozi James Msekela aliyekuwa Italia na Balozi Batilda Burian aliyekuwa Japan kufuatia agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli alilolitoa Januari 25, 2016 kuitaka wizara hiyo kuwarudisha nchini mabalozi waliomaliza muda wao wa kuhudumu ili wapangiwe kazi nyingine.

RAIS DKT. MAGUFULI AZUNGUMZA NA KUWASHUKURU WENYEVITI, MAKATIBU WA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM WA MIKOA NA WILAYA ZA TANZANIA BARA NA VISIWANI

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia Wenyeviti, Makatibu wa Chama cha Mapinduzi wa mikoa na Wilaya za Tanzania bara na Visiwani Ikulu jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wenyeviti wa CCM wa Mikoa mbalimbali wakipiga makofi kumshangilia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati akitoa hotuba yake Ikulu jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wenyeviti wa CCM wa Mikoa mbalimbali wakipiga makofi kumshangilia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati akitoa hotuba yake Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza kwa makini taarifa zilizokuwa zikitolewa na baadhi ya Wenyeviti na Makatibu wa CCM kutoka mikoa mbalimbali nchini. Kulia kwake ni makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Makamu Mwenyekiti CCM Taifa Philip Mangula na Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mtwara Mohamed Sinani Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi Mzee Ally Mtopa Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono baadhi ya viongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM kutoka mikoa mbalimbali nchini mara baada ya kumaliza kuzungumza nao Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

LIJUE BASI LA MWENDO HARAKA

$
0
0
MRADI wa mabasi yatakayo kwenda mwendo wa haraka katika barabara teule mpya jijini Dar es Salaam unaweza kuwa na ufunguo wenye sulushisho dhidi ya foleni na misongamano ya magari jijini humu.

Matarajio ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam ni kwamba kuzinduliwa kwa mradi huu kutakuwa ndio mwisho wa tatizo sugu la foleni katika barabara zake nyembamba ambazo nyingi mtindo wake ulijengwa na Wakoloni zaidi ya miaka 100 iliyopita.

Pamoja na kuwahi kuwepo aina hii ya mabasi katika miaka ya 1980, sasa mabasi haya yamerudi tena katika ubora wa kipekee na tofauti hasa katika suala zima la uundwaji wake wa kuvutia zaidi na ulio na mapambo mengi kama vile televisheni, kiyoyozi, kamera za usalama(CCTV Camera) ambazo zitasaidia kuonyesha usalama ndani ya basi, endapo utatokea uhalifu wowote muhusika ataonekana mara moja. Pamoja na kuwepo vyote hivyo pia kuna na viti kwa ajili ya watu wenye mahitaji maalum ambao ni walemavu wa viungo pamoja na mama wajawazito.

TUANGALIE BAADHI YA SEHEMU KATIKA BASI HILI;

A. STELINGI - STEERING WHEEL

Mfumo wa stelingi ni ZF ya Ujerumani, wenye ubora wa kimataifa na unaozingatia usalama wa basi liendeshwapo barabarani muda wote. Pia kiti cha dereva kina uwezo wa kumpunguzia uchovu wa kukaa kwa muda mrefu ili kumsaidia kuwa makini aendeshapo basi husika ili kuepukana na ajali.

B. TAIRI - TYRE

Matairi bora yaliyothibitishwa na viwango vya kimataifa (ISO) ili kuweza kukabiliana na mabadiriko ya tabia nchi.

C. KIZIMIA MOTO - FIRE EXTINGUISHER

Mitungi maalum ya kuzimishia moto utokanao na vimiminika (mafuta), gasi, hitilafu za umeme n.k

D. INJINI - ENGINE

Aina ya injini ni CUMMINS iliyotengenezwa nchini Marekani (USA) ndio inayotumika katika mabasi yaendayo kwa haraka, injini hii kwa kiasi kikubwa imepunguza uchafuzi wa mazingira, imedhibiti uchafuzi wa mazingira (air pollution), makelele (noise pollution)

E. KAMERA ZA USALAMA - CCTV CAMERAS

Skrini ndogo yenye ukubwa wa inchi saba inayo dhibiti kamera 16 zilizomo ndani ya basi zinazo onesha yote yanayojiri ndani ya basi na kwa kupitia teknolojia iliyowekwa ndani ya kila basi yenye uwezo wa kutuma picha za matukio yote yanayojiri ndani ya basi liwapo barabarani kwenda kituo kikuu cha udhibiti na uchunguzi na matukio ya kihalifu na uharibifu wa samani.

F. VITI - SEATS

Ndani ya basi haki za walemavu, wazee, wajawazito zimezingatiwa kwa kutengewa viti maalum kulingana na mahitaji husika ikiwemo vikuju vya kushika kwenye bomba kwa abiria wanao simama.

TIGO WAKABIDHI MADAWATI 400 KWA WILAYA YA MWANGA KATIKA SHULE 8

$
0
0
 
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Meck Sadiki akikabidhi madawati 400 yenye thamani ya shilingi milioni 66   kwa mwenyekiti wa halmashauri ya Mwanga Theresia Msuya yaliotolewa na Kampuni ya Tigo, Kulia ni Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini George Lugata.
---
Aprili 20 2016 Mwanga: Kampuni ya Tigo Tanzania imetoa msaada wa madawati 400 yenye thamani ya shilingi milioni 66 kwa shule nane za msingi katika manispaa ya Mwanga, mkoa wa Kilimanjaro, ikiwa ni mchango wa kampuni hiyo katika kuisaidia serikali kukabiliana na upungufu wa madawati katika shule za msingi nchini.

Akizungumza leo katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika shule ya msingi Reli Juu katika manispaa ya Mwanga, Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini George Lugata amesema mchango huo ni sehemu ya utekelezaji wa dhamira ya kampuni hiyo ya kuunga mkono jitihada mbalimbali za kuleta maendeleo nchini.

“Mchango huu ni sehemu ya jitihada mbalimbali zinazofanywa na Tigo katika kusaidia utekelezaji wa miradi yenye tija kubwa kwa jamii. Tunaamini kwamba kupitia msaada huu, Tigo inatoa mchango wake katika kujenga viongozi wa baadaye wa taifa hili na wanataluuma mbalimbali wakiwamo madaktari, wahandisi na wengineo, "amesema Lugata.

Lugata amesema mwaka jana Tigo ilikabidhi msaada kama huo wa madawati katika shule za msingi katika mikoa ya Shinyanga, Mbeya Iringa na Morogoro na kuongeza kwamba kampuni hiyo itaendelea kutoa madawati zaidi sehemu mbalimbali nchini siku za zijazo.

Makabidhiano yalihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro mheshimiwa Meck Sadiki ambaye alisema madawati hayo 400 yataboresha mazingira ya kujifunzia kwa watoto katika Mkoa wa Kilimanjaro na kutoa wito kwa wadau wengine kuunga mkono zoezi hilo.

“Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa kampuni ya Tigo kwa kuwa mdau muhimu kwetu katika jitihada zinazoendelea za kujaribu kupunguza tatizo la ukosefu wa madawati ya kutosha katika shule za msingi za mkoa wetu wa Kilimanjaro. Ni dhahiri kwamba msaada huu wa madawati 400 yatawawezesha mamia ya wanafunzi wetu kupata sehemu za kukaa na hivyo kujipatia elimu zao katika mazingira bora zaidi,” alisema Sadiki

Madawati hayo yametolewa kwa shule za msingi nane kama ifuatavo, Mramba,Kawawa, Mwanga, Naweru, Kiboriloni, Lawate na Reli Juu.

RC MAKONDA AMWAPISHA MKUU WA WILAYA MPYA WA KINONDONI ALLY SALUM HAPI JIJINI DAR

$
0
0
Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mmbando, akizungumza wakati akielezea kuhusu hafla ya kumwapisha Mkuu wa Wilaya mpya wa Kinondoni, Ally Salum Hapi (wa pili kushoto), jijini Dar es Salaam leo. Wa tatu ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na wa nne ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Baadhi ya waalikwa, wafanyakazi wa Manispaa za jijini la Dar es Salaam na wageni waalikwa wakiwa katika hafla ya kumwapisha Mkuu wa Wilaya mpya wa Kinondoni, Ally Salum Hapi jijini Dar es Salaam leo. 

Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar es Salaam, wakiwa katika hafla ya kumwapisha Mkuu wa Wilaya mpya wa Kinondoni, Ally Salum Hapi jijini Dar es Salaam leo. 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akizungumza wakati wa kumwapisha Mkuu wa Wilaya mpya wa Kinondoni, Ally Salum Hapi (kulia), jijini Dar es Salaam leo. 
Mkuu wa Wilaya mpya wa Kinondoni, Ally Salum Hapi (kulia), akiwa na Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mmbando.
Wakuu wa Wilaya za Ilala, Raymond Mushi (kushoto) na wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema, wakiwa katika hafla hiyo ya kumwapisha Mkuu mpya wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Salum Hapi.
Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mmbando, akielezea kuhusu utaratibu wa kumwapisha Mkuu wa Wilaya mpya wa Kinondoni, Ally Salum Hapi (katikati), wakati wa hafla hiyo. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kushoto), akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi katika hafla hiyo. 

Mkuu wa Wilaya mpya wa Kinondoni, Ally Salum Hapi (kushoto), akijiandaa kuapa. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akiwa tayari kumwapisha.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akimwapisha Mkuu wa Wilaya mpya wa Kinondoni, Ally Salum Hapi (kushoto), jijini Dar es Salaam leo. 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akisaini hati ya kiapo wakati alipomwapisha Mkuu wa Wilaya mpya wa Kinondoni, Ally Salum Hapi (kushoto), jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mmbando.

Mkuu wa Wilaya mpya wa Kinondoni, Ally Salum Hapi (kushoto), akisaini hati ya kiapo chake, mara baada ya kuapishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kulia), jijini Dar es Salaam leo. 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kulia), akionesha Katiba ya Jamhuri ya Muungano (kushoto) na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambavyo alikuwa tayari kumkabidhi Mkuu wa Wilaya mpya wa Kinondoni, Ally Salum Hapi (kushoto), mara baada ya kumwapisha leo jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kulia), akimkabidhi Katiba ya Jamhuri ya Muungano na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), mara baada ya kumwapisha Mkuu wa Wilaya mpya wa Kinondoni, Ally Salum Hapi (kushoto), leo jijini Dar es Salaam. 

Mkuu wa Wilaya mpya wa Kinondoni, Ally Salum Hapi (kushoto), akiabidhiwa maua na Katibu Tawala Msaidizi (Utawala) wa Mkoa wa Dar es Salaam, Elly Mcha. Kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mmbando.  

Mkuu wa Wilaya mpya wa Kinondoni, Ally Salum Hapi (kushoto), akiabidhiwa maua na Katibu Tawala Msaidizi (Utawala) wa Mkoa wa Dar es Salaam, Elly Mcha. 

Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema akisoma salamu za Mkoa kwa Mkuu wa Wilaya mpya wa Kinondoni, Ally Salum Hapi.

Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema akimkabidhi kadi yenye salamu za Mkoa Mkuu wa Wilaya mpya wa Kinondoni, Ally Salum Hapi. 

Mkuu wa Wilaya mpya wa Kinondoni, Ally Salum Hapi, akizungumza mara baada ya kuapishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda. 

Baadhi ya wageni waliokuwepo katika hafla hiyo, wakisikiliza hotuba ya mkuu huyo wa wilaya. 

Baadhi ya wageni waliokuwepo katika hafla hiyo, wakisikiliza hotuba ya mkuu huyo wa wilaya.  

Baadhi ya wageni waliokuwepo katika hafla hiyo, wakisikiliza hotuba ya mkuu huyo wa wilaya.

Ofisa Habari wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Adrofina Ndandakizye, akichukua habari wakati wa hafla hiyo.

Mkuu wa Wilaya mpya wa Kinondoni, Ally Salum Hapi (kushoto), akipongezwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Viewing all 11654 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>